Je kuna umuhimu wowote kumuandalia Chakula mumeo wakati housegirl yupo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je kuna umuhimu wowote kumuandalia Chakula mumeo wakati housegirl yupo?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Akili Unazo!, Jul 24, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,814
  Likes Received: 2,520
  Trophy Points: 280
  Wakuu ebu nisaidieni kuna umuhimu wowote kumwandalia chakule mumeo wakati housegirl/houseboy yupo na analipwa kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kuanzia usafi hadi chakula kinaenda vizuri?
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  Hakyanani, kama mi ndo mumeo, acha kuniandalia hayo uone.
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Jul 24, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Chaku please usiniangushe darling eh
  Yote yafanya out of love sweetheart.. kama unampenda mumeo utamfanyia tu kwanza we mwenyewe unawezaukajikuta unasahau hata kama housegirl yupo!!

  Ila naye asiichukulie kama ni wajibu wako mpenzi.

  Everything U do, do it for LOVE!
   
 4. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Yes ni muhimu kwa mke kufanya hivyo kwa mumewe labda mke awe amesafiri, anaumwa, hayupo na labda siku fulani kachoka na kumuomba housegirl amsaidie.
  Anaweza pia akakusaidia usafi huyo mfanyakazi ila siyo chumbani mnapolala wanandoa, humo ni wewe tu kuwajibika.
  Hayo ni kati ya majukumu ya mwanamke kwenye mji wake.
   
 5. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  Thank you.
   
 6. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ha!ha!ha!ha!.......mkuu vipi tena?
   
 7. G

  Giroy Member

  #7
  Jul 24, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumuandalia mume chakula ni kazi ya mke,kufanya usafi wa nguo za mume ni kazi ya mke,kupanga chumba na kutandika kitanda,kumpelekea maji ya kuoga bafuni ni kazi yake pia.ukitaka kusaidiwa vyote hivyo bila sababu ya msingi unamtengenezea huyo msaidizi mazingira ya kukurithi.kaa chonyo wanawake wengine wameharibu ndoa zao kwa uzembe wakarithiwa.wewe usiwe moja wao.
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Swadaktaaaaaaa!
  1.Na kazi ya mume ni ipi?

  2.Je wanaokaa majuu huko mnafanyaje maana kila mtu anaenda kwenye mihangaiko kwa faida ya familia na hakuna cha hausigeli kwa walio wengi.

  3.Je mke akisafiri, ina maana mume hali, haogi, hatandiki kitanda, wala hafanyi usafi chumbani hadi mke arudi?
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  WoS, nadhani maelezo yake hili yako hapo kwen nyekundu

   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  MFUMO DUME huo. Mwanamke haolewi ili atumikishwe kazi. Kunatakiwa kusaidiana ama sivyo atakuwa kama Punda.
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nimekupata.
  Naomba unijibu maswali yangu hasa la kwanza....hapo nitaelewa na nitachangia zaidi
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280

  Hahaha, hapo nilimsaidia tu kwenye hilo cause it was a bit obvious, hayo mengine sijui mtizamo wake utakuwaje mwenye aliyepost lol!
   
 13. G

  Giroy Member

  #13
  Jul 24, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninachopingana nacho ni mazoea ya mume kuhudumiwa na h/ girl.mazingira kama hayo, huyo mdada kuwa karibu na mumeo,mara asante dada kwa chakula kizuri, wewe umelala tu,huo ni mfano.mimi mwenyewe namsaidia sana mke wangu.na akisafiri nadeki mwenyewe chumba changu,hiyo ndiyo heshima ya ndoa.mimi sitaki kukutana na mke wangu kitandani tu,upendo nikutumikiana hivo ndivo vionyo vinavyoleta ladha ktk ndoa.
   
 14. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  NDIYO.
  Hapa housegirl ndio anawajibika kuwaandalia wote wawili.

  Hapa housegirl ndio atamuandalia huyo mwanaume, kuhusu studio (Chumbani) yote mawili yawezekana yaani mume mwenyewe atandike kitanda au hata huyo housegirl.
  Ila mwanaume hapo usianze mambo mengine tofauti.
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kazi za mume katika uhusiano wenu wa ndoa Ndugu Giroy ni zipi

  asante ndugu

  Huu mjadala nao! Na msaidizi akiwa wa kiume inakuwaje?..utazoeana naye halafu inakuwaje maana unasema hausgeli ukimzoea basi na mengine ni possibility!
  Ninachotaka kuona ni mke na mume wakiwa na uhusiano mzuri bila kufanya mwingine mtumwa kwa visingizio vizivyo na msingi.
   
 16. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mazoea haya yakizidi housegirl anakuwa mke msaidizi.
   
 17. Violet

  Violet Member

  #17
  Jul 24, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yessssss ni muhimu kwa mwanamke kumwandalia mme chakula. Inaonyesha mapenzi. House girl ni kwa watoto na nyumba. Wanawake wa kizungu pia wanafanya hio, esp east europe.
   
 18. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #18
  Jul 24, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Je nakinyume chake yaani mume haruhusiwi au hatakiwi kuyafanya hayo!?

  Kumuandalia mke chakula, kufanya usafi wa nguo za mke na kuogesha watoto, kutandika kitanda, na kumpelekea mke maji ya kuoga bafuni si kazi yake pia?

  Kina dada mnalionaje jambo hilo si katika haki zenu kufanyiwa haya yote!?
   
 19. L

  Lizy JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 413
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 80
  Binafsi, sioni kama ni muhimu saana. Kama muda unaruhusu, yes 'mke anaweza' kumuandalia Mume chakula hata kama housegirl/houseboy yupo. Lakini kama muda hauruhusu, mfano mke pia ni muhangaikaji (kazi/kibarua/biashara) kama Mume, sidhani kama ni kosa chakula kikiandaliwa na housegirl/houseboy au Mume mwenyewe ajiandalie. Ikumbukwe hata huyu Mwanamke anatumia 'damu' na siyo 'kamashine' flani kasikochoka. So, wote Mume na Mke wana majukumu ya kuandaliana chakula pale inapobidi na kama wanao hao Maids,then why to pay a person for nothing.

  I bet kama ni Mume wa kurun na housegirl, hata kama mke atampikia, kumfulia na kumuosha, kama ni mchafu ni mchafu tu, atarun na maid kama kawa.

  Unless huyo Mume naye awe ameoa huyo Mke kwa kumtumikisha, otherwise sioni kwa nini mke mbali na kuhangaika huko na kule kama mumewe, then akifika nyumbani aanze tena sijui kupika na mengineyo, wakati mume sijui anaangalia TV or whatever, no way.
   
 20. M

  Mwanansuke Member

  #20
  Jul 25, 2009
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa Ushauri tu, rejea katika mafundisho ya kidini (labda uwe mpagani), wanume wanaaswa kuwapenda wake zao, na wake wanatakiwa kutii...chakula cha mumeo au nguo zake za ndani kwa mfano usimwachie house girl kufanya, siyo mfumo dume wanao kushauri wengine bali ni ishara ya heshma na kutii na inaonesha mumeo ulimkubali kwa yote.ina maana kama h/girl asingekuwepo msingekula au kuvaa nguo safi?
  wanaume pia kwa upendo wanafarijika sana wakiona mkewe akimjali hivi, na yeye siku zote atakupenda na kukuheshimu kama ni mtu mwenye akili timamu.....ukimwachia housegirl majukumu yote hayo hata yeye mwenyewe anakudharau kwanza anakuona tu kama mtu uliye kuja kwa ajili ya tendo la ndoa.ila kuna wakati ambao kwa mfano wote mpo ofcn mpaka late, jioni, hapa mnatakiwa kusaidiana kwa makubaliano lakini, sio lazima
   
Loading...