Je, Kuna ulazima mke kumpa mme maji ya kuoga?

MANKWI G

Member
Joined
May 15, 2015
Posts
27
Reaction score
3
Wanajamvi poleni na majukumu,

Jambo hili lilinipa utata baada ya kuona mji fulani mme na mke wanagombana kisa mke jana hakumpa mme wake maji ya kuoga.

Swali langu, Je kuna ulazma mke ampe maji ya kuoga mme wake?
 
Upo uwezekano huo,tukiangalia zaidi upande wa mila na desturi za jamii za ki-Afrika!
 
Kama ndo utaratibu wa maisha waliyojiwekea ama kawaida yao ama kutokana na mila na destuli zao ni sawa wala lisikushangaze!
 
Kama wamezoeshana ivo ni lazima ndio.labda kue kuna sababu ndo hatampelekea maji bafuni,eg:kuumwa
Ila ka hamnaga utaratibu huo sioni ka ni lazima
 
Upo uwezekano huo,tukiangalia zaidi upande wa mila na desturi za jamii za ki-Afrika!

Mila na desturi hizi ndizo zinafanya wanaume wengi wanashindwa kuoa wasomi....!!! Hivi unategemea mkeo awe ni professor then aache kupitia articles zake akupelekee maji bafuni???
 
sasa unakuta bafuni kuna bomba,showerr,jacuz
au vyovyote vile
hapo utampelekea nini sasa???
labda taulo ukimsubir na kich....i

ila kama maji ni ya kununua(hala hala kimara)
lazima upeleke na ndoo
 
Kwani ameoa articles? Get to the point. There are gender roles which in most cases zinakuwa determined na mila na tamaduni za jamii husika.

Hata akiwa profesa lazima kama ndo utaratibu wao, ni muhimu kuyaongea pia kabla ya kuingia kwenye makubaliano ya maisha.

Kigezo cha usomi siyo ishu kabisa kwa mwanamke anyejitambua maana elimu inamsaidia kutambua mazingira anayoishi, mila, wajibu wake na njia sahihi za kushawishi mabadiliko katika maeneo anayoona yana mapungufu!
 
Mila my foot mbona kutafuta hamsemi mila. Ingekuwa ni mazoea wasingegombana hilo lidume linataka tu kuweka mfumo dume. Hivi hiimianaume mbona inapenda madeko hivyo jmn? Tumerudi wote umeweka miguu juu unaangalia tv mie nakimbizana na watoto naa da chakula bado unataka nikuwekee maji. Wewe chunga sana siku nitakuumiza walah
 
Haya mambo ya shower, jacuz yametuharibia tamaduni zetu. Zamani ukitoka bafuni umanukia iriki na mdalasini.
 
Njoo Tanga weye
.
Mila my foot mbona kutafuta hamsemi mila. Ingekuwa ni mazoea wasingegombana hilo lidume linataka tu kuweka mfumo dume. Hivi hiimianaume mbona inapenda madeko hivyo jmn? Tumerudi wote umeweka miguu juu unaangalia tv mie nakimbizana na watoto naa da chakula bado unataka nikuwekee maji. Wewe chunga sana siku nitakuumiza walah
Usirudie tena...

Kwani ameoa articles? Get to the point. There are gender roles which in most cases zinakuwa determined na mila na tamaduni za jamii husika.

Hata akiwa profesa lazima kama ndo utaratibu wao, ni muhimu kuyaongea pia kabla ya kuingia kwenye makubaliano ya maisha.

Kigezo cha usomi siyo ishu kabisa kwa mwanamke anyejitambua maana elimu inamsaidia kutambua mazingira anayoishi, mila, wajibu wake na njia sahihi za kushawishi mabadiliko katika maeneo anayoona yana mapungufu!

Hata malkia Elizabeth ana mjali mumewe
 
Ni majukumu tu, kila mtu ana yake. Mjusi akiingia ndani utasikia baba fulani njoo nafwa!
 
Mila na desturi hizi ndizo zinafanya wanaume wengi wanashindwa kuoa wasomi....!!! Hivi unategemea mkeo awe ni professor then aache kupitia articles zake akupelekee maji bafuni???
role conflict
 
Tuliza munkari. Halafu elewa maana ya "mila na desturi" kisha elewa maana ya "elimu". Tafadhali usichanganye yote hayo pamoja na hisia zako binafsi!
 
umuhimu upo kulingana na mazingira mnayoishi, na jinsi kila mmoja alivyofundwa kwao
kama mwanaume anajua ni kazi ya mke kumtengea maji usipofanya hivyo italete shida ila kuna wengine wanaona ni sawa.
kwa mfano miji ambayo kuna baridi na hamna bafu lenye heater ndani lazma umchemshie maji sasa kama umechemsha unategemea aje ayategue ajipelekee bafuni nop utapooza na kumtengea vile vile.
kuna vitu vingine ni vidogo sana haina haja ya kubishana, kwani ukibeba maji kumpelekea mumeo bafuni unapungua wapi
 
Mila my foot mbona kutafuta hamsemi mila. Ingekuwa ni mazoea wasingegombana hilo lidume linataka tu kuweka mfumo dume. Hivi hiimianaume mbona inapenda madeko hivyo jmn? Tumerudi wote umeweka miguu juu unaangalia tv mie nakimbizana na watoto naa da chakula bado unataka nikuwekee maji. Wewe chunga sana siku nitakuumiza walah

Hahahaa. Ndio wake zetu wa kisasa hawa. Walimu wataendelea kubamba soko
 
Back
Top Bottom