Je, Kuna Ukomo Wa Muda Kudai Mirathi?

Je, Kuna Ukomo Wa Muda Kudai Mirathi?

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
855
Wanajamvi, ni takribani miaka 30 sasa tangu mzee wangu atangulie mbele za haki. Kwa kipindi chote hicho haki zake (mirathi) ambazo kimsingi huamia kwa watoto na mjane wa marehemu hazikuchukuliwa kutokana na sababu mbalimbali hasa za kifamilia na kiasi fulani uzembe wa wakubwa wangu kuwa wazito katika kufuatilia.

Mwaka 2008, ilikuja barua toka ofisi (polisi) ambako mzee wangu alikuwa akifanyia kazi, ikitoa maelekezo kwa familia kukaa na kuteua msimamizi wa mirathi, na mahitaji mengine kama vile cheti cha kifo, kiapo cha mjane kuwa hajaolewa, na picha za watoto chini ya umri wa miaka 18 kwa wakati huo baada ya kufariki kwa mzee.

Sasa hadi barua hiyo inafika, mama yetu mpendwa naye alishafariki miaka 14 iliyopita yaani kama miaka 10 tangu mzee wetu afariki. Hadi naandika hivi sasa, zoezi zima la mirathi halijafanyika, hadi sasa naandika haya, watoto wote wa marehemu walishavuka umri wa miaka 18, yaani hakuna ambaye ni mtoto tena.

Kwa maelezo hayo hapo juu, je, inawezekana mirathi hiyo ikafuatiliwa tena kwa kipindi hiki yaani miaka 30 tangu kufariki kwa mzee wetu (hasa ikizingatiwa mjane wa marehemu naye alishafariki na hasa ikizingatiwa hakuna mtoto wa marehemu aliye chini ya miaka 18)?

Je, mirathi kama mirathi hufikia kiwango gani cha pesa kwa watumishi wa umma katika jeshi la polisi?

Naombeni ushauri na maelezo ya kina.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom