Je, kuna tofauti kati ya duka la dawa, duka la dawa baridi na pharmacy?

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Husika na kichwa cha habari hapo juu huwa nashindwa kutofautisha haya maduka au yote ni sawa huduma ndio tofauti na dawa tofauti au yote ni tofauti na huduma ni tofauti lakini dawa ni hizo hizo naombeni kueleweshwa.
 
Ni kitu kimoja mkuu
 
Tofauti ipo mkuu wa stendi.Ni hivi badala ya dawa baridi yalifanyika maboresho na kuita duka la dawa muhimu,Duka la dawa muhimu huuza dawa zile ambazo hazina ulazima wa andiko la daktari(ndio zile ziliitwa dawa baridi) lakini pharmacy inauza dawa zote ikimaanisha zile zinazohitaji idhini ya daktari kutumia(moto).

Informative shukrani
 
Hata duka la dawa muhimu huuza baadhi ya dawa ambazo lazma ziandikwe na Daktari japo sio zote
 
Asnte sana mkuu kwa ufafanuzi
Tofauti ipo mkuu wa stendi.Ni hivi badala ya dawa baridi yalifanyika maboresho na kuita duka la dawa muhimu,Duka la dawa muhimu huuza dawa zile ambazo hazina ulazima wa andiko la daktari(ndio zile ziliitwa dawa baridi) lakini pharmacy inauza dawa zote ikimaanisha zile zinazohitaji idhini ya daktari kutumia(moto).
 
Kumbe ..
Nilikut mabishano sehemu kuwa eti pharmacy kuna dawa unaweza pata ambazo duka la dawa la kawaida eti huzikuti
Hamna tofauti, zaidi ni urasimu uliohalalishwa na mamlaka inayothamini vyeti na wadhifa.
 
Tofauti ipo mkuu wa stendi.Ni hivi badala ya dawa baridi yalifanyika maboresho na kuita duka la dawa muhimu,Duka la dawa muhimu huuza dawa zile ambazo hazina ulazima wa andiko la daktari(ndio zile ziliitwa dawa baridi) lakini pharmacy inauza dawa zote ikimaanisha zile zinazohitaji idhini ya daktari kutumia(moto).
Asante kwa ufafanuzi mkuu. Inaonekana wewe una uelewa juu ya dawa. Je duka la dawa muhimu linauza tu over-the-counter drugs au linauza na prescription drugs?
 
Ni mbingu na ardhi japo kwa magumashi duka la dawa wanauza kila kitu kuanzia viagra mpaka wakina p2 na
 
Mzee wa Stand tayari umejibiwa ila ngoja nikutajie baadhi ya dawa ambazo hazihitaji prescription ya daktari.Panadol,asprin,dawa ya mba,bandeji,spirit,dawa za meno,dawa za vidonda,dawa za kuchua misuli nk

Pharmacy kubwa mfano SH Amon ya Mwanza ni dawa ambazo zinahitaji kupata kibali cha hospitali ulikotibiwa na mara nyingi wafanyakazi wake au wamiliki wake wana taaluma za ufamasia na unaweza taka dawa flani ukakataliwa.

Ila pamoja na yote ziko tena dawa zingine ambazo pharmacy za mitaani haziruhusiwi kuwa nazo ni hospitali kubwa tu na tena ziwe za rufaa mfano dawa moja inaitwa Epethidine hii dawa ni ya kupunguza maumivu makali ya mifupa ina vinasaba kidogo kama madawa ya kulevya.Hata hospitalini kwenyewe manesi wakikabidhiana wanapobadilishana zamu wanakabidhiana kwa sahihi.

Ila sasa haya maduka yetu ya dawa muhimu mitaani shauri ya tamaa yamejiingiza kuwa nao wanauza baadhi ya dawa ambazo hawastahili kuwa nazo ila ukweli ni kwamba dawa hizo zinatoka mahospitalini kwetu zinaiingia mitaani wewe ukienda hospitali unaambiwa nenda kanunue pharmacy flani.Ni uvunjifu wa sheria sababu kwanza hata wenyewe wenye maduka hayo wanatumia vyeti vya maduka makubwa.

Wenye maduka hayo mnisamehe huo ndio ukweli sijawachongea ila mnatusaidia kwa kweli ila kuweni wawazi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom