Je, kuna mkono wa mtu mkubwa sana katika jaribio la kutoa uhai wa Tundu Lissu?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,483
30,155
Kwenye taaluma ya sheria kuna kitu kinaitwa "circumstantial evidence" au kwa kiswahili tunaita ushahidi wa mazingira, ambao unaweza kumtia hatiani mtuhumiwa

Hivi inawezakanaje Bwana yule kutamka hadharani kuwa Mbunge Tundu Lissu amelitelekeza jimbo la Singida Mashariki na hivi sasa ndiyo limepata Mbunge safi, ambaye ni Miraji Mtaturu wa CCM??

Anaendelea kueleza kuwa jimbo hilo hivi sasa ndiyo litapata maendeleo ya haraka haraka baada ya "kuporwa" Tundu Lissu wa upinzani na hivi sasa kukabidhiwa Miraji Mtaturu wa CCM!

Hivi tangu lini maendeleo ya majimboni nchini kwetu yameanza kupangiwa bajeti na Ikulu badala ya Bunge??

Hivi ni nani katika dunia hii ambaye hajui kilichomsibu Mbunge Tundu Lissu, takribani miaka miwili iliyopita, baada ya kumiminiwa risasi zaidi ya 30 kwenye gari lake na risasi 16 kumwingia mwilini mwake, katika jaribio la kumwua, ambapo alinusurika kimuujiza na hadi hivi Leo anaendelea na matibabu huko ubelgiji??

Katika mazingira ambayo Jeshi la Polisi halijafanya juhudi zozote za kuwatafuta wale waliotekeleza mpango huo wa kidhalimu, hivi anapotokea mtu na kusema kuwa Tundu Lissu amelitelekeza jimbo hilo, hivi tunaweza kumuelewa vipi mtu huyo??

Katika hali ya kawaida kwa binadamu yoyote alipaswa "a-sympathize" na hali aliyonayo Tundu Lissu hivi sasa, kwa hiyo ni ajabu kusikia Bwana yule akitamka hadharani kuwa Tundu Lissu eti amelitelekeza jimbo lake la Singida Mashariki na hivyo kumlazimu Spika Ndugai afanye utaratibu wa kuweza kumpata Mbunge mwingine!

Ni kutokana na muujiza wa Mungu pekee ambao umeendelea kumpa uhai Tundu Lissu hadi hivi Leo na naendelea kuamini kuwa lipo kusudi maalum la Mungu la kuendelea kumpa uhai Tundu Lissu hadi hivi leo na hivyo hadi hilo kusudi litimie na hivyo tumwombe Mungu wetu azidi kutujaalia uhai ili tuweze kushuhudia hicho kitu "so special" ambacho Mungu mwenyewe amekipanga kwa mja wake huyu

Mungu ibariki Tanzania
 
Wapinzani tunaposema kuwa utawala huu wa awamu ya tano unafanya ubaguzi wa dhahiri katiika kupeleka maendeleo katika majimbo ambayo wawakilishi wake ni wa CCM na majimbo ambayo wamechagua upinzani yanaambulia patupu ushahidi "beyond reasonable doubt" ni haya matamshi ya Rais Magufuli

Na tunamsikia Rais wetu kwenye majukwaa ya kisiasa akituhadaa watanzania kuwa maendeleo hayana vyama!
 
Na walaaniwe wote walioshiriki kwenye jaribio la kumuua Tundu Lissu. Wao na vizazi vyao hata kizazi cha tatu na cha nne.
Inaonesha wale wote waliopanga, amrisha na kutekeleza majaribio yale ya mauwaji dhidi ya Lissu watapukutika baada ya mwingine na itaendelea kuwa hivyo.

Kibaya zaidi ni hapo picha nzima itakavyopakiwa kwenye U tube bora tu mtu ajifie mbele kabla ya siku inayokuja ya kiama na kumeza chungu.
 
Mungu huwa hadhihikawi........

Kule kwenda kanisani kila Jumpili wakati wewe ndiye "mastermind" wa matukio mengi ya uhalifu wa nchi hii, hakika Mungu ataonyesha ukuuu na utukufu wake
 
White imepanga bajeti ilikunya fidia kwa kipindi cha walichomkosa lissu usile siasa zako za kienyeji raisi amefanya busara sana
 
Wapinzani tunaposema kuwa utawala huu wa awamu ya tano unafanya ubaguzi wa dhahiri katiika kupeleka maendeleo katika majimbo ambayo wawakilishi wake ni wa CCM na majimbo ambayo wamechagua upinzani yanaambulia patupu ushahidi "beyond reasonable doubt" ni haya matamshi ya Rais Magufuli

Na tunamsikia Rais wetu kwenye majukwaa ya kisiasa akituhadaa watanzania kuwa maendeleo hayana vyama!
Uzuri wa watu wa karne hii wanajitambua na hawataki malumbano wana wasiliana kila siku, wanashawishiana na maamuzi yao yanabakia ndani ya mioyo yao kwa ajili ya kuepuka malumbano ambayo hayana tija.

Wako kimya kwa kujua wakiwa na maamuzi sahihi miyoyoni mwao, hawataki kushiriki katika gulio la kunua na kuuza ungovi.
 
Utawala wowote unaonyamazia maovu hata ukajenga mabarabara yote utaendelea kukosolewa Na kuchukiwa tu.haiwezekani rais aliyeapa kuilinda katiba yetu ashangilie uporaji wa haki za RAIA kuchagua mbunge wao Na kupachika MTU wasiyemchagua wao kuwa mbunge wao.hili jambo la lissu limechafua utawala wa awamu ya tano sana.hapa duniani tunapita tu.hizi siasa zisilete uadui Ni hatari sana, haya madaraka Ni ya muda tu.
 
Hata enzi zile za utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini, nchi hiyo walijenga miundo mbinu, ambayo hakuna nchi yoyote barani humu iliyoweza kuwashinda

Hata hivyo katika siasa zake za kibaguzi, nchi hiyo ilitengwa na dunia nzima
 
Na bila shaka bwana yule ndie alieagiza Lissu ashughulikiwe.
Unajuwa majina waliyotumia kina Nape, Makambas, Kinana & co yanadhihirisha uhalisia wa kiongozi huyo.
Nina imani kuwa waliopita kama BM au JK lazima kwa mfumo wa kiafrika wamehusika na operations mbalimbali za kuhujumu maisha ya watu. Lakini kwa nini wao hawatajwi katika lolote?
Hawana ushamba wa kufanya mambo bila kufikiri, matendo yao yanabaki kuwa in the line of duty.
Huyu jamaa ni unyama, chuki na ukatili na ndio maana hajifichi kuonyesha moyo wake ukoje.
 
Back
Top Bottom