Je, Kuna miti ukiipanda huleta mikosi?

mfate42

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
3,768
4,259
Ndugu habarini za mchana, poleni na pilika pilika za kupambana na corona niende kwenye mada..

Je, ni kweli kuna baadhi ya miti ikipandwa maeneo ya nyumbani huleta mikosi, kutokuelewana, na ugomvi wa Mara kwa Mara? Kwa mfano Kuna mti unaitwa Mngazi ambao huwa una matawi yaliochanua mithili ya ngazi ngazi..

Nimeona watu wengi, hata juzi tu jirani yangu ameing'oa miti hiyo na nilipomuuliza kwanini anafanya hivyo akanijibu kuwa miti hiyo sio mizuri,..huleta mikosi na ugomvi kwenye familia..

Je, Hilo swala Lina ukweli wowote?..au ni imani tu za watu, maana mi mwenyewe nimeipanda mingi sana..kwenye eneo langu..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah pia inatumika sana upande wa gizani...miti inamaana kubwa na siri nyingi sana...mfano kule upareni upo mti ambao ukiuchoma na wale waliokaribu wakauvuta Moshi..basi hapo ngumi zitapigwa haijawahi tokea...mfano uchome pale magogoni.. wallah mbona utacheka kwa ngumi zitakazotokea...
 
Kuna mti unaitwa mpanga uzazi kwa kanda ya ziwa wanaujua vizuri, tulikuwaga tunaambiwa tuukate tukazembea huo mti unatenganisha familia ni ukweli imetokea home kwetu more than 14 years now familia ilitengana niko kinda bado

Sent using Jamii Forums mobile app


Ni imani tu mkuu...huu mti una asili ya mizizi mikubwa sana inayotambaa ardhini...kwahyo ukiupanda jua hata miaka 20 nyumba itakuja kuanguka...inaweka ufa mwishoww inaanguka..so wanashauri uupande mbali sana na nyumba!

Kwetu niliupanda mwaka 2000 had leo upo na mama na baba wapo pamoja!😅😅sijui lakini
 
ahhh bwana jiranii nilikuwa nakutani
😊😊😊😊😊😊
 
Haya mambo ya Imani

Hata kisayansi miti ina kemikali (chemicals) nyingi sana. Mwili wa binadam una "react" haraka sana kwa muingiliano wa "chemicals". Na chemicals huweza kuwa harufu, vumbi na au hata mvuke na moshi (fumes).

binadam pia tuna emit chemicals nyingi kwa njia ya harufu tunazoweza kuzinusa na hata tusizoweza kuzinusa (kwa range yetu ya kunusa) ndiyo maana hata wanyama utaona wana reactions mbali mbali kwa watu mbali mbali kwa nyakati mbali mbali.

miti nayo ina emit fumes aina nyingi zenye kemikali zinazowweza kutuathiri "mood" ya mtu kwa nanna moja au nyingine.

hili la miti si la kulidharau ni la kulifanyia kazi, lina ukweli mkubwa sana ndani yake.

Umeshawahi kuona mgaogao wa paka ukimuwekea paka anavyo react? Jiulize kwanini?
 
Huo mpanga uzazi niliwahi kuupanda home mzee akaniambia niukate nikatimiza wajibu .
 
Back
Top Bottom