Je, kuna madhara kupaki chombo kwa wiki 1 mpaka 2?

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
761
1,006
Habarini. Nina pikipiki ndogo ya HonLg 110,

Kwa Sasa nataka kusafiri kwa takribani wiki 1 au 2.

Hivyo nitaipaki ndani, haitoendeshwa kwa hizo wiki, kwani sijapata mtu mwaminifu wa kumwachia.

Je, kuna madhara yapi yatatokea au nizingatie yapi ili nikirudi niikute ikiwa nzima Kama nililivyoiacha?
 
Lengo sio kusafiri nayo,
Nataka niiache kwa wiki mbili bila kuendeshwa, je ina madhara?

Hii naitumia kwa mizunguko ya hapahapa mtaani.
Haina madhara kwa muda huo wa wiki mbili. Madhara yatatokea kwenye battery kuisha chaji kama imeshaanza kuchoka...Siyo ishu kubwa sana unaweza kuchomoa terminal moja..

Pia nakushauri Kama oil imetembea kilometa nyingi, ukirudi imwage uweke mpya..

Hakikisha matairi yana upepo wa kutosha...usiipaki sakafuni huku haina upepo kwenye tairi...siyo vizuri..

Ni hayo tu machache.
 
Changamoto huwa na battery kuharibika, disconnect terminal za battery. Otherwise kwa hizo wiki 2 utaikuta salama
 
Nani kakwambia kutoka Japan hadi hapa ni miezi mi3?
acha hiyo miezi mitatu
hata mwaka Gari au Lori lazima liwake sembuse hako katukutuku
km betri ipo chini wakusukume litawaka na itajicharge
miScania inawaka na imetoka Sweden ikakaa bandarini Yard
jamani acheni utani basi hata mimi baiskeli yangu haitaondoka
 
haina shida kuna mwamba alikua anaenda kozi anaacha pkpk ndani miez 6 akirud anapga starter anasepa (boxer 150) wiki 2 mtu asiguse kbsa ficha funguo kbsa ucje ckia ipo mtaroni
 
Back
Top Bottom