Je, kuna kiumbe mwingine mwenye uwezo kama mwanadamu? Part 1

Dunia yakoo

Senior Member
Nov 23, 2019
139
214
images (1).jpg

Wale ambao hawawezi kukumbuka historia, ndiyo ambao kimakosa wanarudia makosa ya kihistoria” - George Santayana

Rais wa 40 wa taifa la Marekani, mwenye daraja la 33 kwenye asasi ya Freemasons na pia mwanachama wa asasi nyingine ya siri inayokwenda kwa jina la Knights of Malta na mwenye damu ya kifalme ya kishetani, Ronald Reagan mara kwa mara amekuwa akizungumzia ni namna gani dunia nzima itaweza kuungana endapo patakuwepo na kitisho cha uvamizi wa viumbe kutoka sayari nyingine.

Kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1987, Septemba 21 alisema;
“Katika hali yetu kubwa ya chuki na utengano tuliyo nayo hivi sasa, mara kwa mara tunasahau ni kiasi gani binaadam tumeungana. Huenda tunahitaji kitu kutoka nje, kitisho cha ulimwengu kitakacho tufanya sisi kuweza kutambua umoja huu tulio nao. Nimekuwa nikifikiria ni namna gani tofauti zetu zitatoweka pale ambapo tutakuwa tunapambana na kitisho cha viumbe kutoka nje ya sayari yetu”.

Mwaka 1988 Mei 5, White House, kwenye chumba kilicho jaa waandishi wa habari, Reagan alisema,
“Nimekuwa nikijiuliza mwenyewe kwamba itakuwaje kama sisi sote hapa duniani tukagundua ya kuwa kuna kitisho dhidi yetu kutoka nje ya dunia yetu … nguvu ya kutoka kwenye sayari nyingine. Je si mara moja tu tutaweza kutambua kuwa hatuna tofauti yoyote baina yetu, kwamba wote tu binadamu, wananchi wa dunia na je, hatutaungana kupambana na kitisho hicho?”
Wazo hili la kuwa kuna au kutakuwa na kitisho kutoka nje ya dunia yetu, nje ya mfumo wetu wa jua, yaani nje ya galaxy ya Milk Way, raisi huyu amekuwa akilitaja mara kwa mara wakati na baada ya uongozi wake.

Henry Kissinger Kwenye mkutano wa Bilderberger, Evians, Ufaransa mwaka 1992 alisema,
“Leo hii Marekani itakasirishwa endapo Umoja wa Mataifa utaingia Los Angeles kutuliza amani. Lakini kesho watafurahia kitu hicho! Hii ni kweli hasa endapo wataambiwa kuna kitisho kutoka nje ya sayari yetu kinacho tishia uhai wetu.”
“Itakuwa hivyo kwa watu wote wa dunia ambapo wataomba msaada wa kupambana na kitisho hicho. Kitu kimoja ambacho kila mtu anakiogopa ni kile ambacho hakifahamiki. Walimwengu watakapo letewa kitisho hicho, haki zao za msingi wataziachia na kuzikabidhi kwa serikali ya dunia ambayo itawahakikishia usalama wao.”

Katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani vyombo kadhaa vya habari na mitandao ya kijamii vilikuwa vikiripoti kuwa wananchi wa Marekani wangelipendelea kumpa Obama ushindi kwenye uchaguzi huo kama shujaa ambaye mwenye uwezo wa kuliokoa taifa hilo kwenye shambulizi la viumbe wasio julikana kutoka kwenye sayari nyingine. Asilimia 72 ya wananchi wataifa hilo wanaamini juu ya kuwepo kwa viumbe hao na uwezekano wa kutokea kitisho hicho.

Kwenye miaka ya karibuni neno ‘UFO’ (Unidentified flying object) limechukua kasi kwenye vyombo vya habari, hasa nchi za Magharibi, Asia, na Marekani. Vyombo hivi mwonekano wake ni duara lakini pia vinaweza kuwa na umbo jingine tofauti na hilo kama tutakavyo ona. Taarifa zisizo rasmi kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari na maelezo ya watafiti mbalimbali kwenye suala hili ni kuwa UFO hutumika kama chombo cha anga cha kusafiria kwa viumbe hao wasio julikana kutoka sayari ya mbali. Lakini tabia yake ni tofauti sana na vyombo vyetu vya anga.

UFO haionekani kuathiriwa na nguvu za mvutano, inakwenda kwa mwendo kasi mkubwa sana ambao hakuna vyombo vyetu vya kusafiria vilivyo pata kurikodiwa kuwa na mwendo kasi huo, huweza kubadili mwelekeo wake katika nukta yoyote ya safari yake, na inaweza kutoweka machoni pa mtazamaji ndani ya sekunde na asijue ameona nini.

Baadhi ya vyombo vikubwa vya habari, wanasiasa, wasomi, wanafunzi na viongozi wanauchukulia huu mtazamo mpya wa nafasi yetu na sayari yetu kwenye ulimwengu utatuletea amani ya kidunia ambayo haijapata kuwepo, umoja na udugu na maendeleo makubwa. Lakini kwa upande mwingine hasa watafiti huru na wasomi kadhalika wanaamini kuwa huu mtazamo mpya utatupeleka kwenye wakati mgumu na changamoto nzito tulizo pata kukutana nazo kwenye sayari yetu hii.

UFO kweli zipo au ni aina fulani ya udanganyifu?
Asilimia 72 ya wananchi wa Marekani wanaamini juu ya kuwepo kwa uhai nje ya sayari yetu na kwamba kuna viumbe wengine wanaishi huko. Asilimia 48 wanaamini juu ya kuwepo kwa UFO na asilimia 15 wanaamini kuwa wameona UFO. Asilimia 2-3 wanaamini kuwa wamewahi kutekwa na viumbe hao na kuingizwa kwenye UFO na baadaye kurejesha walipo kuwa.

Kuhusiana na UFO kumekuwepo na taarifa nyingi mno, kutoka kwenye magazeti mpaka majarida. Vijitabu na mavitabu. Kutoka kwenye taarifa za watu waliona UFO, walio waona viumbe hao, mpaka wale walio kamata na kupakiwa kwenye UFO. Wakati mwingine inakuwa ni vigumu kuzithibitisha taarifa hizo, wakati mwingine taarifa zinakuzwa kubwa kushinda tukio lenyewe, wakati mwingine kwa makusudi zinakuwa ni taarifa za kutengeneza au zenye upotoshaji.

Lakini bado kuna wakati tukio moja linakuwa na mashahidi zaidi ya mmoja, linakuwa limeacha ushahidi wenye kuonekana, ushahidi unao weza kuugusa kwa mkono, ushahidi ambao ni zaidi ya maneno ya shuhuda.Wale ambao hawawezi kukumbuka historia, ndiyo ambao kimakosa wanarudia makosa ya kihistoria” - George Santayana

Rais wa 40 wa taifa la Marekani, mwenye daraja la 33 kwenye asasi ya Freemasons na pia mwanachama wa asasi nyingine ya siri inayokwenda kwa jina la Knights of Malta na mwenye damu ya kifalme ya kishetani, Ronald Reagan mara kwa mara amekuwa akizungumzia ni namna gani dunia nzima itaweza kuungana endapo patakuwepo na kitisho cha uvamizi wa viumbe kutoka sayari nyingine.

Kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1987, Septemba 21 alisema;

“Katika hali yetu kubwa ya chuki na utengano tuliyo nayo hivi sasa, mara kwa mara tunasahau ni kiasi gani binaadam tumeungana. Huenda tunahitaji kitu kutoka nje, kitisho cha ulimwengu kitakacho tufanya sisi kuweza kutambua umoja huu tulio nao. Nimekuwa nikifikiria ni namna gani tofauti zetu zitatoweka pale ambapo tutakuwa tunapambana na kitisho cha viumbe kutoka nje ya sayari yetu”.

Mwaka 1988 Mei 5, White House, kwenye chumba kilicho jaa waandishi wa habari, Reagan alisema,
“Nimekuwa nikijiuliza mwenyewe kwamba itakuwaje kama sisi sote hapa duniani tukagundua ya kuwa kuna kitisho dhidi yetu kutoka nje ya dunia yetu … nguvu ya kutoka kwenye sayari nyingine. Je si mara moja tu tutaweza kutambua kuwa hatuna tofauti yoyote baina yetu, kwamba wote tu binadamu, wananchi wa dunia na je, hatutaungana kupambana na kitisho hicho?”

Wazo hili la kuwa kuna au kutakuwa na kitisho kutoka nje ya dunia yetu, nje ya mfumo wetu wa jua, yaani nje ya galaxy ya Milk Way, raisi huyu amekuwa akilitaja mara kwa mara wakati na baada ya uongozi wake.

Henry Kissinger Kwenye mkutano wa Bilderberger, Evians, Ufaransa mwaka 1992 alisema,
“Leo hii Marekani itakasirishwa endapo Umoja wa Mataifa utaingia Los Angeles kutuliza amani. Lakini kesho watafurahia kitu hicho! Hii ni kweli hasa endapo wataambiwa kuna kitisho kutoka nje ya sayari yetu kinacho tishia uhai wetu.”
“Itakuwa hivyo kwa watu wote wa dunia ambapo wataomba msaada wa kupambana na kitisho hicho. Kitu kimoja ambacho kila mtu anakiogopa ni kile ambacho hakifahamiki. Walimwengu watakapo letewa kitisho hicho, haki zao za msingi wataziachia na kuzikabidhi kwa serikali ya dunia ambayo itawahakikishia usalama wao.”

Katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani vyombo kadhaa vya habari na mitandao ya kijamii vimekuwa vikiripoti kuwa wananchi wa Marekani wangelipendelea kumpa Obama ushindi kwenye uchaguzi huo kama shujaa ambaye mwenye uwezo wa kuliokoa taifa hilo kwenye shambulizi la viumbe wasio julikana kutoka kwenye sayari nyingine. Asilimia 72 ya wananchi wataifa hilo wanaamini juu ya kuwepo kwa viumbe hao na uwezekano wa kutokea kitisho hicho.

Kwenye miaka ya karibuni neno ‘UFO’ (Unidentified flying object) limechukua kasi kwenye vyombo vya habari, hasa nchi za Magharibi, Asia, na Marekani. Vyombo hivi mwonekano wake ni duara lakini pia vinaweza kuwa na umbo jingine tofauti na hilo kama tutakavyo ona. Taarifa zisizo rasmi kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari na maelezo ya watafiti mbalimbali kwenye suala hili ni kuwa UFO hutumika kama chombo cha anga cha kusafiria kwa viumbe hao wasio julikana kutoka sayari ya mbali. Lakini tabia yake ni tofauti sana na vyombo vyetu vya anga.

UFO haionekani kuathiriwa na nguvu za mvutano, inakwenda kwa mwendo kasi mkubwa sana ambao hakuna vyombo vyetu vya kusafiria vilivyo pata kurikodiwa kuwa na mwendo kasi huo, huweza kubadili mwelekeo wake katika nukta yoyote ya safari yake, na inaweza kutoweka machoni pa mtazamaji ndani ya sekunde na asijue ameona nini.

Baadhi ya vyombo vikubwa vya habari, wanasiasa, wasomi, wanafunzi na viongozi wanauchukulia huu mtazamo mpya wa nafasi yetu na sayari yetu kwenye ulimwengu utatuletea amani ya kidunia ambayo haijapata kuwepo, umoja na udugu na maendeleo makubwa. Lakini kwa upande mwingine hasa watafiti huru na wasomi kadhalika wanaamini kuwa huu mtazamo mpya utatupeleka kwenye wakati mgumu na changamoto nzito tulizo pata kukutana nazo kwenye sayari yetu hii.

UFO kweli zipo au ni aina fulani ya udanganyifu?
Asilimia 72 ya wananchi wa Marekani wanaamini juu ya kuwepo kwa uhai nje ya sayari yetu na kwamba kuna viumbe wengine wanaishi huko. Asilimia 48 wanaamini juu ya kuwepo kwa UFO na asilimia 15 wanaamini kuwa wameona UFO. Asilimia 2-3 wanaamini kuwa wamewahi kutekwa na viumbe hao na kuingizwa kwenye UFO na baadaye kurejesha walipo kuwa.

Kuhusiana na UFO kumekuwepo na taarifa nyingi mno, kutoka kwenye magazeti mpaka majarida. Vijitabu na mavitabu. Kutoka kwenye taarifa za watu waliona UFO, walio waona viumbe hao, mpaka wale walio kamata na kupakiwa kwenye UFO. Wakati mwingine inakuwa ni vigumu kuzithibitisha taarifa hizo, wakati mwingine taarifa zinakuzwa kubwa kushinda tukio lenyewe, wakati mwingine kwa makusudi zinakuwa ni taarifa za kutengeneza au zenye upotoshaji. Lakini bado kuna wakati tukio moja linakuwa na mashahidi zaidi ya mmoja, linakuwa limeacha ushahidi wenye kuonekana, ushahidi unao weza kuugusa kwa mkono, ushahidi ambao ni zaidi ya maneno ya shuhuda. Inaendeles
 
wengine wamekuwa wakihusisha habari hizi kama porojo za vijiweni tu.. wengine bhangi n.k.

lakini ukweli ni kwaba hawa viumbe wapo..

ulimwengu wote huu, mabilion ya sayari yote hayo, alafu useme tupo wenyewe tu!!
Sio kweli.

Safari za Anga anazofanya binadamu kwa wakati huu ni sawa na mtu kutoka chumbani kwake kwenda uani..
hiyo ina maana kwamba hata Seluthi ya ulimwengu bado hatujaifikia/kuujua.

Nb. kama habari hizi ni porojo ama bangi kama wengine wasemavyo, Christopher Clumbus nae ni mtunga porojo...
make katika safari zake aliwaona kitu kama tunavyovijadili hapa.

wenye dunia yao wanakuwa sana kwamba hivi vipi, ila hataki tujue.
na siku tukijua..dunia itataharuki kitu ambacho wenye dunia hawataki kitokee.
 
Kiongozi nimekuelewa point yako
 
Hizo ni porojo tu, za watu walio shiba kuishi wakivembewa wanakuwa na Hallucinations, na wajinga wataamini! kwa nini hao Aliens wapatikane USA tu? tena kwenye jangwa, sisi huku Africa hawaji kwa nini? huku ndiyo pangekuwa zaidi kwa sabab ya Pyramids za Misri, ambazo viumbe wa juu hutumia kutua Duniani km rada ya mwongozo! Mt. Moriah ndo viumbe saba vya kale vilitua pale, pangekuwa rahisi kwao hao Aliens kutumia njia zilezile kuingia Duniani, hata km ni kupotea njia kidogo na kuangukia East Africa siyo mbaya.

Vitisho vya matajiri tu hivyo wanatengeneza Robot wanadanganya ni ALIENS, kwa nini huko USA watekwe wazungu tu na wesi wapo wengi hawatekwi? kama wapo kweli na Elim yao ya sayansi ni kubwa kuliko yetu, wanaogopa nini kuungana na sisi? wakati hatujawapiga vita? wema woote huu tulio nao, kwa mfano atue mbagala na ndege yake ya kuganda hewani maarufu km kisahani, atapokelewa vizuri tu na mke anapewa bure!
 
Back
Top Bottom