FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,416
- 7,828
Habari!
Kwa kipindi kirefu tumekuwa tukifuatilia sakata hili kati ya Marekani na Uturuki kuhusiana na mpango wa ndege za kivita za kizazi cha tano za F-35 ambapo Marekani iliiondoa Uturuki katika mpango huo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutokana na Uturuki 'kujisajili' katika mpango wa kijeshi na taifa la Urusi, mpango unaohusisha mifumo ya ulinzi wa anga ya 'S-400' na pengine toleo lijalo la 'S-500'.
Kumekuwa na mjadala mpana sana kuhusiana na hili na pia wamesikika viongozi mbalimbali akiwemo Seneta Lindsey Graham, mtu wa karibu sana huyu wa Rais Donald Trump na ameweka wazi jitihada za kuirudisha Uturuki katika mpango wa F-35 na pia amepinga kuhusu hatua zozote za vikwazo dhidi ya taifa hilo kutokana na manunuzi yake ya mifumo ya anga ya S-400 kutoka Urusi.
Kwa upande wa Idara ya Ulinzi na Usalama ya Marekani kupitia Waziri wa Ulinzi, Mark Esper imeweka wazi kuwa Uturuki itahitajika kujiondoa 'kabisa' katika mpango wa S-400 wa Urusi kabla ya kurejeshwa katika mpango wao wa F-35 na hili ni kutokana na masuala ya kiulinzi na kiusalama ambayo wamekuwa wakiyaweka wazi.
Ikumbukwe kuwa kuondolewa kwa Uturuki katika mpango huo kutapelekea hasara ya takribani Dola Bilioni 9 kutokana na mikataba mbalimbali inayohusisha vifaa mbalimbali vya uundwaji wa ndege hizo.
Hiyo ni kwa kifupi tu lakini tujadili hili;
Je, kuna haja ya Marekani kuirudisha Uturuki katika mpango wake wa ndege za F-35?
Kwanini anadhani kuna haja hiyo?
Na kama ni hapana, pia kwa nini unafikiri hivyo?
Karibu!