Je, Kuna dalili za ile nyongeza ya mishahara?

Je, Kuna dalili za ile nyongeza ya mishahara?

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,784
Reaction score
6,178
"Nasitisha ajira na nyongeza za mishahara kwa mwezi mmoja au mmoja na nusu HAITAZIDI MIEZI MIWILI"

Wakati huo ilikuwa ni juni 13 hata kama si mtaalamu wa hesabu lakini kwa haraka hadi ikifika sept 13 tayari imetimia miezi mitatu.

Swali langu; je mwezi huu nao watumishi wa uma wataendelea kusomeshwa hiyo namba ama watapewa increments yao kama sheria inavyosema au hapa kazi tu mafao uzeeni?

Na kama sivyo morali na ile ari ya kufanya kazi kwa moyo itakuwepo tena?

Unaruhusiwa kunitukana kama umeona nina kosa lolote.
 
Endelea kuota,wewe unaona meli zimepungua,serikali inahamia Dom,hiyo pesa itakuwepo kweli?
 
ndoto tena...na uchochezi..

nimemchochea nani?
 
Mkuu hapo kama upo serikalini kiajira imekula kwako.. Mnavodanganywa kuhusu wafanyakazi hewa basi ujue kazi bado mbichiiiiiiiii
Jana nikiwa wilaya ya chalinze, mkoa wa pwan nimeshuhudia kwa mamcjo yangu watumishi wakiombwa kuleta vyeti kwa uhakiki.. Ina maana ndo kumekucha…
Serikali bado ipo kwenye mazingaombwe na sarakasi tu
 
Hapa nilipo nina hasira maana mtu mzima kama mimi kudanganywa kweupeeeee inauma sana.
 
"Nasitisha ajira na nyongeza za mishahara kwa mwezi mmoja au mmoja na nusu HAITAZIDI MIEZI MIWILI"

Wakati huo ilikuwa ni juni 13 hata kama si mtaalamu wa hesabu lakini kwa haraka hadi ikifika sept 13 tayari imetimia miezi mitatu.

Swali langu; je mwezi huu nao watumishi wa uma wataendelea kusomeshwa hiyo namba ama watapewa increments yao kama sheria inavyosema au hapa kazi tu mafao uzeeni?

Na kama sivyo morali na ile ari ya kufanya kazi kwa moyo itakuwepo tena?

Unaruhusiwa kunitukana kama umeona nina kosa lolote.
Mbona umekimbilia kujihami kama utatukanwa! Umeuliza jambo zuri tu, ila umemalizia kijinga, mambo ya kusoma namba yanatoka wapi tena! Any way, naamini mwezi huu watumishi watainjoi sana.
 
Labda waphotocopy noti za ziada.hujasikia malalamiko kuwa fedha zimefichwa majumbani ?
 
Tatizo rais anafanya kaz sio yake yeye nw alitakiwa kuwa Mbunge na si rais
 
Kuna watu wanamchezesha mzee draft la kizungu kule..

Inahitaji akili ya ziada kutatua hizi changamoto
 
Labda ikifika dec ndo ataongeza kwa sasa ni muda wa matamko ya hovyohovyo.
 
Suala hili linatia hasira sana..
 
Back
Top Bottom