Je, kufanya mapenzi ni tiba ya saratani?

Je, kufanya mapenzi ni tiba ya saratani?

baptist

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2013
Posts
434
Reaction score
279
141030095906_many_partners_512x288_bbc.jpg

​

Kulala na wanawake wengi kunapunguza hatari ya kupatikana na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo,kulingana na utafiti.

Katika utafiti uliochapishwa katika jarida la saratani,Watafiti kutoka chuo kikuu cha Montreal wamebaini kwamba ikilinganishwa na wanaume walio na mpenzi mmoja katika maisha yao yote,kulala na zaidi ya wanawake 20 kunapunguza uwezekano wa kupatikana na ugonjwa huo kwa asilimia 28.

Wanaume 3,208 walishiriki katika utafiti huo ambapo kati yao Wanaume 1,590 walipatikana na ugonjwa huo kati ya Septemba mwaka 2005 na Agosti mwaka 2009.

Kwa jumla watafiti hao walibaini kwamba wanaume wenye saratani ya kibofu cha mkojo kuna uwezekano mara mbili kwa wao kuwa na watu wa familia zao wenye saratani.

Hatahivyo ushahidi unaonyesha kwamba idadi kubwa ya wapenzi wa kike miongoni mwa wanaume inapunguza tishio la ugonjwa huo.

Mwanamume anapojamiana na zaidi ya wanawake 20 katika maisha yake,tisho la kupata ugonjwa huo linapoungua kwa asilimia 28 mbali na asilimia 19 kwa aina yoyote ya ugonjwa wa saratani.

Utafiti huo pia umebaini kwamba mmoja kati ya wanaume wanne wa kiafrika hupatikana na saratani

CHANZO: BBC
 
Dah tafiti hizi zinahamasisha ngono kwa kwenda mbele
 
kumbeeee.... nitafute wawili wa mwisho nikamilishe number!!!!
 
Iwe ni kweli au si kweli by default napingana na utafiti kwa nguvu zote. Usiniulize kwanini!
 
Lakini hawa hawa wanaume ndio wasambazaji wa cervical cancer kutoka kwa mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine
 
Mhh! hapa watu wamepata kisingizio cha kuongeza michepuko..
 
Kulala na wanawake wengi kunapunguza hatari
ya kupatikana na ugonjwa wa saratani ya kibofu
cha mkojo,kulingana na utafiti.
Katika utafiti uliochapishwa katika jarida la
saratani,Watafiti kutoka chuo kikuu cha Montreal
wamebaini kwamba ikilinganishwa na wanaume
walio na mpenzi mmoja katika maisha yao yote,kulala
na zaidi ya wanawake 20 kunapunguza uwezekano wa
kupatikana na ugonjwa huo kwa asilimia 28.
Wanaume 3,208 walishiriki katika utafiti huo ambapo
kati yao Wanaume 1,590 walipatikana na ugonjwa
huo kati ya Septemba mwaka 2005 na Agosti mwaka
2009.
Kwa jumla watafiti hao walibaini kwamba wanaume
wenye saratani ya kibofu cha mkojo kuna uwezekano
mara mbili kwa wao kuwa na watu wa familia zao
wenye saratani.
Hatahivyo ushahidi unaonyesha kwamba idadi kubwa
ya wapenzi wa kike miongoni mwa wanaume
inapunguza tishio la ugonjwa huo.
Mwanamume anapojamiana na zaidi ya wanawake 20
katika maisha yake,tisho la kupata ugonjwa huo
linapoungua kwa asilimia 28 mbali na asilimia 19 kwa
aina yoyote ya ugonjwa wa saratani.
Utafiti huo pia umebaini kwamba mmoja kati ya
wanaume wanne wa kiafrika hupatikana na saratani
Source; BBC Swahili
BBC waongo. Kujamiiana na wanawake wengi husababisha kansa ya urethra kwa wanaume
 
Mbona huo utafiti hauoneshi ni kwa namna gani hao wanawake wengi wanapunguza hiyo cancer?!
 
Mbona huo utafiti hauoneshi ni kwa namna gani hao wanawake wengi wanapunguza hiyo cancer?!

moja ya sababu zinazosababisha saratani ya shingo ya kizazi kwa mwanamke ni kuwa na wenza wengi au mwenza kuwa na mahusiano na wanawake wengi, historia ya saratani kwa familia yake, kuugua fungus kwa muda mrefu na kuanza ngono chini ya umri wa miaka 18
 
Basi kwa Afrika wanaume hawataugua huo ugonjwaaa,maana kwa kuchepuka mahodari kuliko hata kusaka mavumba
 
Basi kwa Afrika wanaume hawataugua huo ugonjwaaa,maana kwa kuchepuka mahodari kuliko hata kusaka mavumba

Hahhahahahha umeuwa, kuna magonjwa mengine tiba zake hadi raha aisee..
 
Back
Top Bottom