Je, kilichotokea Malawi kinajirudia Zambia ambapo Rais anatimuliwa?

Kaunda alipigwa kwenye sanduku la kura na Fredrick Chiluba.

Fredrick Chiluba akapigwa kwenye sanduku la kura na Levy Mwanawasa

Rupiah Banda akapigwa kwenye sanduku la kura na Michael Chilufya Sata.

Edgar Lungu anachapwa kwenye Sanduku la kura na Hakaindi Hichilema.

Lakini Zambia pia ndiyo nchi pekee ambayo marais wawili walifia madarakani na warithi wao walikuja kuondolewa madarakani kwa sanduku la kura.
 
Tunachojifunza ktk mchezo huu wa Siasa ni Rafiki na mshirika wako wa leo katika mapambano ya mabadiliko ndiye adui wako wa kesho. Ushirika wenye nguvu wa vyama vya upinzani, uliwezesha chama kikongwe cha UNIP kuondoka madarakani 1981 na kukipoteza kabisa ktk medani kwa kutaifishwa mali zake. Sio hivyo tu na Kaunda alifilisiwa na kuwekwa kizuizini kwa kisingizio cha ufisadi akiwa madarakani bila kujali mchango wake kwa Uhuru wa Zambia. Tangu hapo hakujawa na chama chenye kuaminiwa ktk siasa za Zambia, wala malalamko ya ufisadi hayajawahi kuisha. Hakuna tena UNIP lakini waliokuwa kioo cha kuona maovu ya UNIP wanaendelea kuparurana. Hii ndio SIASA.
 
Issue sio wapinzani kuingia madarakani, je wanauwezo wa kuongoza nchi Kama kujiongoza wao tu ni shida wamebaki kusalitiana,kutengana na kuunda magenge ya kula ruzuku zao
 
Kazi kweli kweli. Afrika inaamka. Yalitokea kwa Mugabe, Yahya Jammeh, Lauerent Kabila, Idris Edby na sasa Zambia.
 
Mwananchi wa Jamhuri ya JF wewe ungependezwa iweje? Dhana na upendavyo yaweza isitokee na isiwe sahihi.
Jee wenye kutaka mabadiliko wanataka yaweje na kuna wenye uwezo wa kubadilisha na kuongoza hayo mabadiliko unavyo penda yatokee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu: Tanzania hatuna tume huru ya uchaguzi. Vinginevyo kingelikuwa kimewaka mda mrefu.
 
Zambia is a bit unique, political parties uses tribal hegemony and urban centers' communities for political mobilazation.

Whoever takes power shall face the very people who supported him.

Betrayal is a political currency in Zambia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapa tunajifunza sisi ccm tuhakikishe mizizi inazama chini zaidi maana upepo wa kimbunga unapobadilika na kuwa wa kisulisuli unaweza ng'oa mbuyu legelege..
 
Swali la msingi ni je'baada ya vyama tawala kuondolewa hususan Zambia na Malawi nchi imeonyesha kupiga hatua baada hayo mabadiliko,au ni yaleyale?
 
Lakini natamani kupata mlejesho baada ya upinzani kuchuka dola huko malawi hali imekua je?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…