Je, Kikwete kubebeshwa tuhuma!?

BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
80,661
Likes
117,913
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
80,661 117,913 280
Na Saed Kubenea
MwanaHALISI

UWEZEKANO wa Rais Jakaya Kikwete kugombea bila mpinzani ndani ya chama chake, umeanza kutoweka, MwanaHALISI limeelezwa.

Mkakati mpya wa kumuhusisha na kashfa mbalimbali na hivyo kufanya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuona umuhimu wa kuwa na mgombea mwingine, tayari umeandaliwa.

Gazeti hili lina taarifa kwamba wapinzani wa Kikwete, ndani ya chama chake, wanaandaa taarifa za kusambaza katika vyombo vya habari na vipeperushi kueleza kuwa “hata Kikwete ana kashfa; hafai.”

“Kinacholengwa ni kuonyesha kuwa watuhumiwa wa ufisadi ni pamoja na Kikwete na kwamba kinachohitajika ni kuwaweka wote mbele ya wapigakura ili wachague wanayemtaka,” ameeleza mtoa taarifa.
Mtoa taarifa anasema kutakuwa na kashfa mbili kuu ambamo Kikwete atahusishwa.

Kwanza, atabebeshwa kashifa ya mkataba wa kuzalisha umeme wa kampuni ya IPTL ambao ni moja ya mikataba inayokamua uchumi wa nchi kwa kiwango kikubwa.
Taarifa zinasema itatangazwa, “kwa njia zozote zile,” kwamba Kikwete alishiriki kufanikisha mkataba wa IPTL wakati akiwa waziri wa nishati na madini.
Pili, Kikwete atabebeshwa tuhuma kwamba ameshindwa kushughulikia kile alichoita “mpasuko” wa Zanzibar na hivyo kusababisha mazingira yanayoweza kuvunja Muungano wa Tanzania.

Kwa mwaka mmoja sasa wanaoitwa wapinzani wa Kikwete ndani ya CCM wamekuwa wale waliotuhumiwa ufisadi.
Imekuwa ikiripotiwa mara kwa mara kuwa wabunge waliotuhumiwa ufisadi, hadi wengine kufikia hatua ya kujiuzulu nafasi zao serikalini, wamekuwa wakilalamika kuwa Rais Kikwete aliwatelekekeza.

Wanaofahamika kwa kutuhumiwa ufisadi hadi sasa ni aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, mawaziri watatu wa zamani Andrew Chenge, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi.
Mbunge mmoja kutoka kambi ya Lowassa amekiri kufahamu mbinu hizo na ameliambia gazeti hili, “Huu ndiyo mkakati wa kambi ya upinzani ndani ya CCM. Kama kila mmoja ni mchafu basi tuwaachie wananchi wenyewe wachague.”

Mkakati wa sasa umekuja baada ya kufumuka kwa taarifa za siri zilizomo ndani ya ripoti ya Kamati ya rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi iliyoundwa na CCM kutafuta chanzo cha mpasuko katika Bunge na Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Taarifa zinasema ndani ya ripoti ya Kamati ya Mwinyi, kuna tuhuma nzito walizoshushiwa Lowassa na Rostam kuhusu ushiriki wao katika kuleta mpasuko ndani ya Bunge na serikali.

Imeelezwa hatua ya sasa ya kumkabili Kikwete katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, inatokana na hasira za marafiki na wapambe wa watuhumiwa wanaoona shutuma dhidi ya wenzao zinalenga kuwamaliza kisiasa.
MwanaHALISI lina taarifa kwamba waziri mmoja mwandamizi katika serikali ya Rais Kikwete ndiye aliyemwaga tuhuma tisa, kwa maandishi, mbele ya Kamati ya Mwinyi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka makao makuu ya CCM, Lumumba na ikulu, karibu tuhuma zote tisa zimeelekezwa kwa Lowassa na swahiba wake mkuu Rostam.
Kwa mfano, miongoni mwa tuhuma walizotwishwa Lowassa na Rostam kwa pamoja, ni ile inayowahusisha na kutumia vyombo vya habari, wahariri wa magazeti na waandishi wa habari mmojammoja, kuandika habari na makala zinazolenga kuvuruga serikali.

Sehemu ya taarifa ya waziri kwa Kamati inasema, kwa muda wa miaka miwili sasa, Lowassa na Rostam wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kuvuruga serikali.
Na kwa kila tuhuma ambayo waziri huyo alitoa, alihitimisha kwa kusema ana ushahidi na anachowasilisha.

Tuhuma nyingine ambayo Lowassa na Rostam wanatuhumiwa kwa pamoja, ni ile ya “kushughulikia” wabunge wenzao katika majimbo ya uchaguzi wanayotoka, kwa kudai kuwa ndio walishiriki “kuwaangusha.”

Tuhuma nyingine ni kwamba Lowassa na Rostam wamekusanya makundi ya watu mbalimbali, wakiwamo wabunge, viongozi wandamizi katika chama na serikali, kwa lengo la kujenga makundi ya kuwatetea kutoka katika kashfa za ufisadi zinazowakabili.

Baadhi ya mawaziri na wabunge wanaotajwa kuunga mkono Lowassa na Rostam ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba; mbunge wa Nyamagana, Laurence Masha; mbunge wa Ukonga, Makongoro Mahanga; mbunge wa Songea Mjini, Emmanuel Nchimbi na mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba.

Kamati ya Mwinyi imeelezwa pia kwamba Lowassa amekuwa kiongozi wa kwanza nchini kujiuzulu, lakini papo hapo akaongoza harakati za kujenga makundi ya kujisafisha.
Taaarifa zinasema hilo la Lowassa kujenga mtandao wa kujisafisha lilitajwa na wabunge wengi na kuhoji, mbona Dk. Hassy Kitine na Iddi Simba walijiuzulu lakini hawakuwahi kuunda makundi ya kujisafisha.
Mtoa taarifa kwa Kamati ya Mwinyi alijenga hoja nyingine nzito mbele ya Kamati hiyo.

Alimtuhumu Lowassa kushindwa kuchukua hatua madhubuti kulinda serikali wakati wa sakata la Richmond; badala yake anatumia nguvu kubwa kujitakasa.
Alisema Kikwete alitimiza ahadi yake ya kumpa Lowassa nafasi ya pili ya juu katika uongozi wa nchi na kumfanya Rostam mweka hazina wa CCM; lakini akadai kuwa walizitumia vibaya nafasi hizo.

Mbunge mmoja aliyeongea na Kamati ya Mwinyi amenukuliwa akisema, “Katika mazingira haya, nani wa kulaumiwa? Lowassa ametoboa mwenyewe jahazi lake na Rostam ameondolewa kutokana na tuhuma zinazomkabili.”
Mbunge huyo ameongeza kuwa Rais Kikwete aliona ni vema Rostam akakaa pembeni “ili kusafisha chama.”

Kwa vyovyote vile, Rostam asingekubaliwa kuendelea na wadhifa wake wa mshika mkoba wa CCM, kutokana na kukabiliwa na lundo la tuhuma.
Maelezo ya waziri mbele ya Kamati yanashabihiana, kwa kiwango kikubwa, na yale yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Biashara na Uwekezaji, sasa Nishati na Madini, William Shelukindo.

Shelukindo aliiambia Kamati ya Mwinyi kuwa Kamati yake ilifanya juhudi za kutaka serikali ijisafishe katika sakata la Richmond, lakini ilikosa ushirikiano kutoka kwa Lowassa.

Kwa mujibu wa taarifa, bunge lilitaka serikali ieleze hatua zilizofikiwa katika kushughulikia mchakato wa zabuni ya Richmond, lakini Lowassa kwa muda wote wa miezi tisa, anadaiwa kugoma kutoa taarifa.

Taarifa za ndani ya Kamati ya Mwinyi zinasema baadhi ya wabunge walieleza kuwa Lowassa amekuwa mbinafsi kupindukia na kwamba vurugu na minyukano inayotokea bungeni imesababishwa na ubinafsi wake.
Gazeti hili limeambiwa kuwa kwenye hitimisho la ripoti yake, Kamati ya Mwinyi inamtaka Spika Samwel Sitta kuwa “makini.”

Haikufahamika haraka ni kuwa makini katika lipi na wapi.
 
R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
2,776
Likes
16
Points
135
R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
2,776 16 135
Mi nadhani hapa kichwa cha habri kingekuwa Tuhuma za Kikwete kuwekwa wazi, Kwani kama ni IPTL ni kweli alihusika, na kama ni kuwazuga Wazanzibar kwamba analeta muafaka huku akimtumia mshika kibendera wake Makamba akiwapiga vijembe kwamba Simba haiwezeki kugawa ushindi kwa yanga alifanya!
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,036
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,036 280
Hivi MwanaHalisi wanaweza kuanza stori ya mbele na kitu kingine zaidi ya kina Lowassa na Rostam?
 
B

Bobby

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2008
Messages
1,823
Likes
397
Points
180
B

Bobby

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2008
1,823 397 180
Mi nadhani hapa kichwa cha habri kingekuwa Tuhuma za Kikwete kuwekwa wazi, Kwani kama ni IPTL ni kweli alihusika, na kama ni kuwazuga Wazanzibar kwamba analeta muafaka huku akimtumia mshika kibendera wake Makamba akiwapiga vijembe kwamba Simba haiwezeki kugawa ushindi kwa yanga alifanya!
Ni kweli maana kama kashfa anazo nyingi huyu baba wa bagamoyo. Mojawapo ni hayo mahekalu 14 au ikulu kama wanakijiji wanavyoiita yalijyoengwa kijijini kwake hivi kuna mtu anafahamu yamejengwa kwa gharama ya nani? Maana 14 presidential houses sio kitu cha kubeza sasa amewezaje kusave kiasi hicho mpaka akaweza kujenga? By the way na hili gorofa jipya Msamvu Morogoro ambako kijana wake almost kila w'end anaenda kukagua ujenzi, huyu mkulu kapata wapi hizo pesa jamani?
 
M

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2008
Messages
241
Likes
0
Points
0
M

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2008
241 0 0

Wewe na Kubenea/MwanaHALISI lenu moja. Hamna jipya kila siku ni uongo tu. Kila kukicha Lowasa, Rostam etc. hamna habari nyingine tukazisoma ?? Ukikasirika kunywa sumu.
 
N

Nanu

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Messages
1,224
Likes
9
Points
135
N

Nanu

JF-Expert Member
Joined May 29, 2009
1,224 9 135
Hivi MwanaHalisi wanaweza kuanza stori ya mbele na kitu kingine zaidi ya kina Lowassa na Rostam?
Nadhani ni wakati muafaka sasa Saeed kuwa na uwanda mwingine wa habari maana hata gazeti lake ataliuwa mwenyewe kwani kila wakati habari ya Lowasa na Rostam ndiyo zinatawala MwanaHalisi. Nadhani kuna scandal nyingi zaidi na ambazo ni hatari kwa nchi na Watanzania ambazo Saeed angesaidia kufanya uchunguzi na kuzitoa kwa jamii ambayo itasaidia kukomesha zisiendelee au kupeleka uwajibikaji ufaao kwa vyombo husika. Swala la EPA iliyopita na ambayo inaendelea sasa hivi yahitaji kuangaliwa, nyumba za BoT za gavana na msaidizi wake, repoti ya tume iliyochunguza majengo Dar es Salaam, Umiliki wa CCM wa sehemu zote za wazi zilizotengwa zamani kwa ajili ya huduma za jamii ikiwemo michezo, swala la Loliondo, swala la radar, swala la Samaki wa Magufuli, viwanja vya ufukweni, machinga complex, magari 200 ya CCM na sheria ya gharama za uchaguzi, chakula cha misaada, mirahaba ya madini, uharibifu wa miundo mbinu na mazingira kwa wachimbaji wa dhahabu, misamaha ya kodi kwa wachimbaji wakubwa, etc,etc. Tunahitaji habari zingine pia. Sisemi asiandike ya Richmond, la hasha, lakini na zingine ziwe kwenye headline pia. Saeed think about it, it is my view, that this has been tooo much!!!!!!!!
 
M

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2008
Messages
241
Likes
0
Points
0
M

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2008
241 0 0
Hivi MwanaHalisi wanaweza kuanza stori ya mbele na kitu kingine zaidi ya kina Lowassa na Rostam?
Kubenea ....Mbunge mtarajiwa wa Mafia kwa tiketi ya CUF kwa hiyo usishangae
 
M

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2008
Messages
241
Likes
0
Points
0
M

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2008
241 0 0
Nadhani ni wakati muafaka sasa Saeed kuwa na uwanda mwingine wa habari maana hata gazeti lake ataliuwa mwenyewe kwani kila wakati habari ya Lowasa na Rostam ndiyo zinatawala MwanaHalisi. Nadhani kuna scandal nyingi zaidi na ambazo ni hatari kwa nchi na Watanzania ambazo Saeed angesaidia kufanya uchunguzi na kuzitoa kwa jamii ambayo itasaidia kukomesha zisiendelee au kupeleka uwajibikaji ufaao kwa vyombo husika. Swala la EPA iliyopita na ambayo inaendelea sasa hivi yahitaji kuangaliwa, nyumba za BoT za gavana na msaidizi wake, repoti ya tume iliyochunguza majengo Dar es Salaam, Umiliki wa CCM wa sehemu zote za wazi zilizotengwa zamani kwa ajili ya huduma za jamii ikiwemo michezo, swala la Loliondo, swala la radar, swala la Samaki wa Magufuli, viwanja vya ufukweni, machinga complex, magari 200 ya CCM na sheria ya gharama za uchaguzi, chakula cha misaada, mirahaba ya madini, uharibifu wa miundo mbinu na mazingira kwa wachimbaji wa dhahabu, misamaha ya kodi kwa wachimbaji wakubwa, etc,etc. Tunahitaji habari zingine pia. Sisemi asiandike ya Richmond, la hasha, lakini na zingine ziwe kwenye headline pia. Saeed think about it, it is my view, that this has been tooo much!!!!!!!!
Niulize swali la kizushi tu...Hivi kukodi helicopter moja kwa siku ni shilingi ngapi za ki TZ ????
 
Obi

Obi

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2009
Messages
376
Likes
5
Points
35
Obi

Obi

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2009
376 5 35
Nafikiri Saeed Kubenea hana quality ya kuwa mwandishi wa habari. Tunahitaji watu makini kwenye tasnia hii ya uandishi wa habari na Saeed sio makini hana jipya.
 
M

mgololafinyonge

Member
Joined
Jan 7, 2010
Messages
20
Likes
0
Points
0
M

mgololafinyonge

Member
Joined Jan 7, 2010
20 0 0
Nadhani ni wakati muafaka sasa Saeed kuwa na uwanda mwingine wa habari maana hata gazeti lake ataliuwa mwenyewe kwani kila wakati habari ya Lowasa na Rostam ndiyo zinatawala MwanaHalisi. Nadhani kuna scandal nyingi zaidi na ambazo ni hatari kwa nchi na Watanzania ambazo Saeed angesaidia kufanya uchunguzi na kuzitoa kwa jamii ambayo itasaidia kukomesha zisiendelee au kupeleka uwajibikaji ufaao kwa vyombo husika. Swala la EPA iliyopita na ambayo inaendelea sasa hivi yahitaji kuangaliwa, nyumba za BoT za gavana na msaidizi wake, repoti ya tume iliyochunguza majengo Dar es Salaam, Umiliki wa CCM wa sehemu zote za wazi zilizotengwa zamani kwa ajili ya huduma za jamii ikiwemo michezo, swala la Loliondo, swala la radar, swala la Samaki wa Magufuli, viwanja vya ufukweni, machinga complex, magari 200 ya CCM na sheria ya gharama za uchaguzi, chakula cha misaada, mirahaba ya madini, uharibifu wa miundo mbinu na mazingira kwa wachimbaji wa dhahabu, misamaha ya kodi kwa wachimbaji wakubwa, etc,etc. Tunahitaji habari zingine pia. Sisemi asiandike ya Richmond, la hasha, lakini na zingine ziwe kwenye headline pia. Saeed think about it, it is my view, that this has been tooo much!!!!!!!!
Ni kweli saeed think twice we really want to know about Lowassa na Rostam but kuna habari nyingi tunahitaji kujua kuhusu nchi hii more than Lowassa na Rostam lkini wewe kila siku Lowassa na Rostam unaanza kufanya tuanze kudoubt your proffession kwasababu umejua ukiandika Lowassa na Rostam unauza?or umetumwa tu kuwaandika hao? or your there to for revenge? kuna msukumo mwingine sio tu kutaka watu tujue hadithi ni hela or revenge.Tunahitaji kujua kuhusu TRL na other burning issue from you im really tied sorry for that
 
B

Bobby

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2008
Messages
1,823
Likes
397
Points
180
B

Bobby

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2008
1,823 397 180
Wewe na Kubenea/MwanaHALISI lenu moja. Hamna jipya kila siku ni uongo tu. Kila kukicha Lowasa, Rostam etc. hamna habari nyingine tukazisoma ?? Ukikasirika kunywa sumu.
Me nadhani wewe mzee kibiongo ndio umekasirika sijuwi ni umri au vipi anyway umesamehewa bure. Ulishindwa nini kujibu hoja au kukaa kimya badala ya kunishambulia na kutokwa na mate bila sababu? Nilichokiandika hapo ninadata zote sikusikia kwa mtu so unapaswa kunijibu kwa hoja kama wewe pia ni gret sinka or otherwise funga vidola vyako visiguse keyboard. Mimi si Mwanahalisi/Kubenea kama unavyolazimisha nina uhuru wa kutoa maoni kama ulio nao wewe huwezi kunipangia cha kucomment period.Sumu utakunywa ww si mimi.
 
M

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2008
Messages
241
Likes
0
Points
0
M

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2008
241 0 0
Me nadhani wewe mzee kibiongo ndio umekasirika sijuwi ni umri au vipi anyway umesamehewa bure. Ulishindwa nini kujibu hoja au kukaa kimya badala ya kunishambulia na kutokwa na mate bila sababu? Nilichokiandika hapo ninadata zote sikusikia kwa mtu so unapaswa kunijibu kwa hoja kama wewe pia ni gret sinka or otherwise funga vidola vyako visiguse keyboard. Mimi si Mwanahalisi/Kubenea kama unavyolazimisha nina uhuru wa kutoa maoni kama ulio nao wewe huwezi kunipangia cha kucomment period.Sumu utakunywa ww si mimi.
Hahahahahahaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!! Si unaona sasa, tayari UMEKASIRIKA !!!!!!!! Naogopa usinywe sumu maana nakujua.
 
B

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2009
Messages
1,089
Likes
1,269
Points
280
B

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2009
1,089 1,269 280
Wazee na WaheshimiwaNaomba kutofautiana nanyi katika suala la Mwana Halisi kuandika habari za Lowasa na Rostam.Gazeti linaenda na sources hasa katika uandishi wa uchunguzi. Kubenea ana vyanzo vya kutosha kuandika anayoyaandika. Tuna serikali iliyogawanyika, ikiongozwa na chama kilichogawanyika. Chanzo cha mgawanyiko ni ufisadi.Kuebenea amefika kwenye chungu, tumwache apakue mpaka amalize. Waambie wengine akina Habarinews, IPP, na Habari Leo walete hizo mnazozihitaji.
 
Wacha1

Wacha1

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2009
Messages
12,765
Likes
1,031
Points
280
Wacha1

Wacha1

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2009
12,765 1,031 280
Ni kweli maana kama kashfa anazo nyingi huyu baba wa bagamoyo. Mojawapo ni hayo mahekalu 14 au ikulu kama wanakijiji wanavyoiita yalijyoengwa kijijini kwake hivi kuna mtu anafahamu yamejengwa kwa gharama ya nani? Maana 14 presidential houses sio kitu cha kubeza sasa amewezaje kusave kiasi hicho mpaka akaweza kujenga? By the way na hili gorofa jipya Msamvu Morogoro ambako kijana wake almost kila w'end anaenda kukagua ujenzi, huyu mkulu kapata wapi hizo pesa jamani?
Hakuna memba mwenye camera atuletee haya mahekalu whatever you call them? Tumeona nyumba ya Ndulu tunahitaji kuona fweza za walipa kodi zinakoishia huko Bwagamoyo.
 
B

Bobby

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2008
Messages
1,823
Likes
397
Points
180
B

Bobby

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2008
1,823 397 180
Hakuna memba mwenye camera atuletee haya mahekalu whatever you call them? Tumeona nyumba ya Ndulu tunahitaji kuona fweza za walipa kodi zinakoishia huko Bwagamoyo.
M.M.M sorry unaweza kutusaidia kainzi katurushie hizo picha za mahekalu ya Msoga? Nakumbuka ulishafanya hivyo kwenye cheche za fikra. Mimi nitaleta za ghorofa la Morogoro wakuu within 2 days.
 
Mama Mdogo

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2007
Messages
2,889
Likes
493
Points
180
Mama Mdogo

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2007
2,889 493 180
Mimi sioni ubaya wowote kwenye uandishi wa Mwanahalisi kwani hata magazeti ya IPP na ya Habari Coorporation naye huwa yanaweza shupalia mada moja kwa muda tu. Kinachohitajika ni takwimu za ukweli na si uzushi. Let the Newspapers write what they believe is true provided they have the evidence.
 
Forum statistics

Threads 1,238,894
Members 476,226
Posts 29,335,954