Je, kifo ni uzembe,bahati mbaya au mapenzi ya Mungu?

Sasa kama tunaenda kupewa miili brand new , inakuwaje tupewe adhabu ya kuchomwa moto wakati miili hii haikutumika fufanya dhambi?
 
Thread yoyote ya Mungu ikitokea mtu wa kwanza kunijia akilini ni wewe! Honestly ukifikiria sanaaaa ni ngumu kuamini Mungu.
A chemical animal can not comprehend non chemical living things. Is like searching water by using metal detectors. It is unintelligent dumb as tongue-tied taurine.
 
Kuna natual death na possible death. Possible cause unatokana na vitu kama magari, ndege, sumu, nk
 


Kwa kweli ulikuwa umetiririka vizuri sana nilikuwa upande wako nikakuamini sana lakini misitari ya mwisho umenichanganya, ulishasema Mungu hasababishi kifo, hapendi tuuzunike ila ukasema Mungu anaweza kukuangamiza ukiwa maovu yamezidi kama alivyofanya sodoma na gomora, na kwa misri zidi ya Islael, hapo msimamo wako uko wapi?
 

Lazma! Yaani lazima kwa kila chenye uhai.
Na hayo ndo mapenzi ya mungu.
 

....utaishi miaka mingi lakini mwisho......
Mapenzi ya mungu kwetu yatatimia
 

Hata uwe mwema VP, Uzima wa milele huupati hadi ufe kwanza duniani.

Tujiandae na sisi
 
Wafu wako wapi?
“Wewe ni mavumbi nawe utarudi mavumbini.”—Mwanzo 3:19.
WATU HUSEMA NINI? Watu fulani hufikiri kwamba, baada ya kifo, watu huenda mbinguni, motoni, toharani, au kwingineko. Wengine wanaamini mtu huzaliwa upya akiwa kiumbe kingine. Kwa upande mwingine, wale wanaokataa mawazo ya kidini wanaamini kwamba kifo ndio mwisho wa mambo yote.
BIBLIA INASEMA NINI? Andiko la
Mhubiri 9:10 linasema hivi: “Hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima katika Kaburi, mahali unapokwenda.” Biblia hueleza pia kinachowapata wanadamu na wanyama wanapokufa. Inasema: “Wote wanaenda mahali pamoja. Wote wametoka katika mavumbi, nao wote wanarudi mavumbini.”—Mhubiri 3:20.
Wafu wako katika hali gani?
“Roho yake hutoka, naye hurudi kwenye udongo wake; siku hiyo mawazo yake hupotea.”—Zaburi 146:4.
WATU HUSEMA NINI? Wengi wamefundishwa kwamba mahali atakapoenda mtu baada ya kufa panategemea mambo aliyofanya alipokuwa hai duniani. Ikiwa alifanya mambo mazuri, thawabu yake itakuwa furaha ya milele; ikiwa alifanya mabaya, atateseka milele. Inasemekana kwamba lazima wanadamu wasafishwe dhambi kabla ya kukubaliwa kumwona Mungu baada ya kufa. Inadaiwa wale ambao hawajasafishwa hawawezi kupata shangwe hiyo milele.
BIBLIA INASEMA NINI? Wafu hawafurahii wala kuteseka. Kwa kweli, kwa kuwa hawajui lolote, hawawezi kuhisi chochote, kuwasaidia au kuwaumiza walio hai. Andiko la Mhubiri 9:5, 6 linasema: “Kwa maana walio hai wanajua kwamba watakufa; lakini wafu, hawajui lolote kamwe, . . . Pia, upendo wao na chuki yao na wivu wao tayari zimepotea, na mpaka wakati usio na kipimo hawana fungu lolote tena katika chochote ambacho kitafanywa chini ya jua.”
Je, wafu wana tumaini lolote?
“Mtu akifa, je, anaweza kuishi tena? Mimi nitangojea siku zote za kazi yangu ya kulazimishwa, mpaka kitulizo changu kije.”—Ayubu 14:14.
WATU HUSEMA NINI? Inaaminiwa kwamba mtu anapohukumiwa kwenda motoni, hana tumaini tena. Mateso ya motoni yanasemekana ni ya milele. Kwa upande mwingine, inasemekana kwamba wale walio toharani wanaweza tu kwenda mbinguni baada ya kuondolewa kabisa dhambi zao.
BIBLIA INASEMA NINI? Mwana wa Mungu atawafufua wale waliolala katika kifo, au kuwarudisha hai hapa duniani. Biblia inasema: “Msistaajabie jambo hili, kwa sababu saa inakuja ambayo wale wote waliomo ndani ya makaburi ya ukumbusho wataisikia sauti yake na kutoka.” (Yohana 5:26, 28, 29) Baada ya hapo, vitendo vya mtu ndivyo vitakavyoamua kama Mungu atampa uzima wa milele.*
MACHAGUO YA UPAKUAJI
PODIKASTI
Makala Nyinginezo
Biblia Inasema Nini Kuhusu Uzinzi
Inachosema Biblia Kuhusu Jeuri
Biblia Inasema Nini Kuhusu Wanyama?
Biblia Inasema Nini Kuhusu Kucheza Kamari?
SOMA KATIKA
AMKENI! JUNI 2014
Kuutazama Ulimwengu
Unawezaje Kuwa Rafiki Mzuri?
Kifo
Joseph Priestley
Je, Unakabili Hatari ya Kupata—Ugonjwa wa Fizi?
Jinsi ya Kudhibiti Matumizi
Ustadi wa Kusafiri wa Mbawakawa
 
A chemical animal can not comprehend non chemical living things. Is like searching water by using metal detectors. It is unintelligent dumb as tongue-tied taurine.

Hebu niandikie kiswahili,sijaelewa.
 
Hii hoja hakuna mtu yeyote ataeweza kuijibu zaidi ya anayejua kitabu kituku quran na hadithi za bwana mtume muhammad s.a.w ambaye hatamko neno hata moja kutoka mdomoni isipokuwa ni maono ana wahyi kutoka kwa M.Mungu humo.ndimo muimozungumzwa habari za kifo na maisha baada ya kufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…