Je, kifo ni uzembe,bahati mbaya au mapenzi ya Mungu?

Hii point no 2 ichapishie Biblia yake, Hii tunayoisoma sasahivi inakukataa 100%.

(A)Watu wakifa hawaendi mahali popote:
Unapozungumzia mtu unazungumzia mwili na roho, tufundishe baada ya mwili na roho kutengana roho inaenda wapi?

(B) kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini :Umesoma wapi? hakuna maelezo hayo kwenye Biblia! ila ninachojua mimi kwa muujibu wa maandiko tunaambiwa tutapewa mwili mpya, wewe hayo mafundisho umeyatoa wapi?

Zingatia sana Kuwa Mungu haokoi miili, bali anaokoa Roho..... Hata huwazi kuwa mwili ukikaa kaburini wiki tu funza tupu, baada ya miezi 6 mifupa, Makaburi yalifufuliwa kwenye ujenzi wa barabara mbuyuni, ilikuwa mifupa mitupu. Huyo mungu unayemzungumzia kuwa atafufua watu kutoka makaburini atakuta mifupa tu, labda useme atafufua skeleton. Lakini mungu wa biblia hii ninayoisoma mimi hana kazi na miili hii. kwasababu ameandaa miili mipya. "Mwili ni mavumbi utarudi mavumbini" shughuli yake imeisha. na "Roho itamrudia yeye alieitoa".
Sasa kama tunaenda kupewa miili brand new , inakuwaje tupewe adhabu ya kuchomwa moto wakati miili hii haikutumika fufanya dhambi?
 
Thread yoyote ya Mungu ikitokea mtu wa kwanza kunijia akilini ni wewe! Honestly ukifikiria sanaaaa ni ngumu kuamini Mungu.
A chemical animal can not comprehend non chemical living things. Is like searching water by using metal detectors. It is unintelligent dumb as tongue-tied taurine.
 
Kuna natual death na possible death. Possible cause unatokana na vitu kama magari, ndege, sumu, nk
 
Mkuu, hivi karibuni nilipewa somo kali sana juu ya hili suala na jamaa alikuwa anakuja kunitembea nyumbani kwa ajili ya mafundisho nilishangaa hadi nikaandika notes. Hebu ngoja nikupe na wewe uchambue mwenyewe logiki kali ya huyu jamaa. Ila inabidi usome maandiko yaliyoorodheshwa kwenye Biblia yako.

Mungu hapangi kifo cha mtu. Maandiko yanasema hata mtu mwovu sana Mungu hafurahii kuona anakufa (Ezekiel 18:23). Na pia Mungu hapendi kuona watu wakihuzunika (Maombolezo 3:33). Hivyo basi, kama Mungu hafurahii hata kifo cha mtu mwovu, wala hapendi kuona watu wakihuzunika, iweje basi awe ndie msababishi wa kifo ambacho kinahuzunisha sana watu, wanapopoteza baba, mama, kaka, dada, mume, mke au mtoto?

Kumbuka kwamba wakati ule Lazaro alipokufa, Yesu alihuzunika sana na hata kutoa machozi. Je, ni akili kufikiri kwamba Yesu angehuzunika hadi kutoa machozi kwa kitu ambacho ni baba yake amependa kufanya au mapenzi ya baba yake? Hiyo ingemaanisha kwamba Yesu hakubaliani na kile alichofanya baba yake, au kwamba Baba wa Yesu si mkweli kwamba hapendi kuhuzunisha watu, maana amemhuzunisha hata mwanae mpendwa wa pekee.

Sasa, nani anasababisha kifo? Kuna vitu viwili; chanzo cha kifo chochote kile, cha ugonjwa au uzee ni Shetani Ibilisi (Yohana 8:44). Shetani ndiye chanzo cha kifo kwa kuwa yeye ndie aliwadanganya Adamu na Hawa na matokeo yake watu tunakufa leo kutokana na dhambi ya urithi (Waroma 5:12). Na pia shetani anasababisha vifo kwa kuchochea migongano ya jamii, hasira nk., kama kule Rwanda.

Lakini pia, pamoja na kwamba chanzo cha kifo ni Ibilisi, kuna vifo vingine ni suala la wakati na mahali, kama alivyoeleza Yesu juu ya wale watu walioangukiwa na ukuta pale Yerusalem (Luka 13:4). Lakini pia kuna vifo vya uzembe vya kujitakia, ambavyo wala sio vya asili na wala sio vya Ibilisi. Kwa mfano, ukiendesha gari huku umelewa ukapiga mzinga ukafa, kwa kweli huo ni uzembe wako wala huwezi kumlaumu shetani, japo ni kweli shetani ndiye aliyeleta kifo. Mtu akiweka sumu mezani na kwa hiari yako ukainywa ukijua ile ni sumu, huwezi kumlaumu kwa kunywa sumu kwa kuwa ulijua ile ni sumu, japo ni kweli kuna lawama kiasi zitamwendea yule aliyeileta sumu.

Hivyo basi kwa kifupi, kifo ni adui mkubwa wa Mungu ndio maana anasema lazima akiondolee mbali wakati muafaka utakapofika (1Wakorintho15:26). Lakini ni dhambi kubwa kusema Mungu, ambaye ni mtakatifu sana asiyeweza kufanya au hata kuwaza ovu lolote, ndiye msababishi wa vifo (Yakobo 1:13 na Jobu 34:10).

Kwa mantiki hii basi, wale wote wanaosema kifo ni mapenzi ya Mungu (Bwana ametoa, Bwana ametwaa) Mungu anawaona wanaropoka mambo wasiyoyajua kwa kumsingizia vitu ambavyo chanzo chake ni shetani Ibilisi, na Mungu anasema wanaongea ujinga na atakuja kuwahukumu kwa kumsingizia vitu vya uongo, pamoja na kwamba utumbo wanaoongea wanafundishwa na viongozi wao na wanaishia kuongea ujinga mtupu (Isaya 9:16-17).

Ila sasa, usisahau kwamba Mungu anahukumu watu waovu kwa kutumia kifo. Ila katika hizo hukumu zake wanaokufa ni waovu tu kama adhabu yao, na baada ya kuwa amewapa nafasi na maonyo ya kutosha kujirekebisha. Vifo vinavyohusu hukumu za Mungu havichanganyi waovu na wema. Na huwa anafanya hivyo sio kwa matukio ya kila siku, bali katika siku maalumu anayoichagua. Katika historia ya wanadamu, ameshafanya hivyo kwa Wa-Misri ili kuwakomboa Waisraeli, Sodoma na Gomora, Gharika ya Nuhu, Angamizo la Yerusalemu baada ya kifo cha Yesu na matukio mengine mbali mbali kama wakati ule jamaa walimezwa na ardhi kwa kosa la kupinga uongozi wa Musa (Hesabu 16:31-32).


Kwa kweli ulikuwa umetiririka vizuri sana nilikuwa upande wako nikakuamini sana lakini misitari ya mwisho umenichanganya, ulishasema Mungu hasababishi kifo, hapendi tuuzunike ila ukasema Mungu anaweza kukuangamiza ukiwa maovu yamezidi kama alivyofanya sodoma na gomora, na kwa misri zidi ya Islael, hapo msimamo wako uko wapi?
 
Samahani wana jamvi kama nitakuwa nimeingiza thread hii mahala ambapo siyo mahala pake, ila leo nilikuwa nimepanda daladala kukatokea mabishano yaliyo nishawisha mimi kwashirikisha ninyi tupate maoni.

Kuna mtu alisema kuna binadamu wanakufa kwa kujitakia, au kupenda wao, akitumia mfano m2 unajua kuna magonjwa na unafanya ngono zembe.

Mwingine akaulioza kwani wote walioathirika wanakufa kabla au baada ya kujua wameathirika,? Mwingine akasema mbona wanakufa kwa ajali na tunasema freemason.

Kwamuda huo nikawa nimefika kituo changu cha kushuka nikaacha mjadala unanaendelea, wadau nini maoni yenu mkizingatia kuwa, kama ni ajali wapo waliopata ajali za kutisha na bado wapo hai, wapo waliougua na kuteseka sana bado wapo, na tulio wafahamu wazima au wenye uwezo walmekufa.

Nawakilisha


Lazma! Yaani lazima kwa kila chenye uhai.
Na hayo ndo mapenzi ya mungu.
 
Mungu hajawahi kufanya lolote bali binadamu. Hajawahi umba wala kupanga bali binadamu. Kifo kipo kabla ya chochote hakijaandikwa. Walioandika walifanya hivyo kwa kuona hali halisi. Vipi tembo na wanyama wengine walifanya kosa gani hadi nao wafe? TEMBO akiwa na malisho mazuri huishi hadi maika 70 ndio anakufa na kama si meno kuisha na kushindwa kula angeishi zaidi. Sisi tunakufa kwa sababu tumejipangia hivyo. Kama unabisha kula kwa utaratibu mwili utakavyo kama hujaishi miaka mingi pia na kupumzika.

....utaishi miaka mingi lakini mwisho......
Mapenzi ya mungu kwetu yatatimia
 
1. Hapana, hapangi kifo wala siye aliyesababisha watu waanze kufa - ndiyo sababu anaahidi kuwapatia watu uzima wa nnmilele.
2. Watu wakifa hawaendi mahali popote panapoitwa peponi bali wanaenda kaburini - ndiyo maana kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini
3. Shetani ndiye aliyesababisha watu waanze kufa na kuvuruga makusudi ya Mungu (kwa muda tu) - ndiyo maana Mungu anaahidi kumfutilia mbali shetani na wote wanaomfuata hivi karibuni
4. Kifo cha binadamu si mapenzi ya Mungu - kazi ya Mungu haina makosa, yenye makosa si kazi yake.
Swali jingine.

Hata uwe mwema VP, Uzima wa milele huupati hadi ufe kwanza duniani.

Tujiandae na sisi
 
Wafu wako wapi?
“Wewe ni mavumbi nawe utarudi mavumbini.”—Mwanzo 3:19.
WATU HUSEMA NINI? Watu fulani hufikiri kwamba, baada ya kifo, watu huenda mbinguni, motoni, toharani, au kwingineko. Wengine wanaamini mtu huzaliwa upya akiwa kiumbe kingine. Kwa upande mwingine, wale wanaokataa mawazo ya kidini wanaamini kwamba kifo ndio mwisho wa mambo yote.
BIBLIA INASEMA NINI? Andiko la
Mhubiri 9:10 linasema hivi: “Hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima katika Kaburi, mahali unapokwenda.” Biblia hueleza pia kinachowapata wanadamu na wanyama wanapokufa. Inasema: “Wote wanaenda mahali pamoja. Wote wametoka katika mavumbi, nao wote wanarudi mavumbini.”—Mhubiri 3:20.
Wafu wako katika hali gani?
“Roho yake hutoka, naye hurudi kwenye udongo wake; siku hiyo mawazo yake hupotea.”—Zaburi 146:4.
WATU HUSEMA NINI? Wengi wamefundishwa kwamba mahali atakapoenda mtu baada ya kufa panategemea mambo aliyofanya alipokuwa hai duniani. Ikiwa alifanya mambo mazuri, thawabu yake itakuwa furaha ya milele; ikiwa alifanya mabaya, atateseka milele. Inasemekana kwamba lazima wanadamu wasafishwe dhambi kabla ya kukubaliwa kumwona Mungu baada ya kufa. Inadaiwa wale ambao hawajasafishwa hawawezi kupata shangwe hiyo milele.
BIBLIA INASEMA NINI? Wafu hawafurahii wala kuteseka. Kwa kweli, kwa kuwa hawajui lolote, hawawezi kuhisi chochote, kuwasaidia au kuwaumiza walio hai. Andiko la Mhubiri 9:5, 6 linasema: “Kwa maana walio hai wanajua kwamba watakufa; lakini wafu, hawajui lolote kamwe, . . . Pia, upendo wao na chuki yao na wivu wao tayari zimepotea, na mpaka wakati usio na kipimo hawana fungu lolote tena katika chochote ambacho kitafanywa chini ya jua.”
Je, wafu wana tumaini lolote?
“Mtu akifa, je, anaweza kuishi tena? Mimi nitangojea siku zote za kazi yangu ya kulazimishwa, mpaka kitulizo changu kije.”—Ayubu 14:14.
WATU HUSEMA NINI? Inaaminiwa kwamba mtu anapohukumiwa kwenda motoni, hana tumaini tena. Mateso ya motoni yanasemekana ni ya milele. Kwa upande mwingine, inasemekana kwamba wale walio toharani wanaweza tu kwenda mbinguni baada ya kuondolewa kabisa dhambi zao.
BIBLIA INASEMA NINI? Mwana wa Mungu atawafufua wale waliolala katika kifo, au kuwarudisha hai hapa duniani. Biblia inasema: “Msistaajabie jambo hili, kwa sababu saa inakuja ambayo wale wote waliomo ndani ya makaburi ya ukumbusho wataisikia sauti yake na kutoka.” (Yohana 5:26, 28, 29) Baada ya hapo, vitendo vya mtu ndivyo vitakavyoamua kama Mungu atampa uzima wa milele.*
MACHAGUO YA UPAKUAJI
PODIKASTI
Makala Nyinginezo
Biblia Inasema Nini Kuhusu Uzinzi
Inachosema Biblia Kuhusu Jeuri
Biblia Inasema Nini Kuhusu Wanyama?
Biblia Inasema Nini Kuhusu Kucheza Kamari?
SOMA KATIKA
AMKENI! JUNI 2014
Kuutazama Ulimwengu
Unawezaje Kuwa Rafiki Mzuri?
Kifo
Joseph Priestley
Je, Unakabili Hatari ya Kupata—Ugonjwa wa Fizi?
Jinsi ya Kudhibiti Matumizi
Ustadi wa Kusafiri wa Mbawakawa
 
A chemical animal can not comprehend non chemical living things. Is like searching water by using metal detectors. It is unintelligent dumb as tongue-tied taurine.

Hebu niandikie kiswahili,sijaelewa.
 
Hii hoja hakuna mtu yeyote ataeweza kuijibu zaidi ya anayejua kitabu kituku quran na hadithi za bwana mtume muhammad s.a.w ambaye hatamko neno hata moja kutoka mdomoni isipokuwa ni maono ana wahyi kutoka kwa M.Mungu humo.ndimo muimozungumzwa habari za kifo na maisha baada ya kufa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom