Je, kifo ni uzembe,bahati mbaya au mapenzi ya Mungu?

1. Hapana, hapangi kifo wala siye aliyesababisha watu waanze kufa - ndiyo sababu anaahidi kuwapatia watu uzima wa nnmilele.
2. Watu wakifa hawaendi mahali popote panapoitwa peponi bali wanaenda kaburini - ndiyo maana kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini
3. Shetani ndiye aliyesababisha watu waanze kufa na kuvuruga makusudi ya Mungu (kwa muda tu) - ndiyo maana Mungu anaahidi kumfutilia mbali shetani na wote wanaomfuata hivi karibuni
4. Kifo cha binadamu si mapenzi ya Mungu - kazi ya Mungu haina makosa, yenye makosa si kazi yake.
Swali jingine.

(A)Mwanzo 2:19
kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

(B)Ayubu 1:12
Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana.

Hoja yako ya kwanza haiko sahihi kabisa. Kifo kimepangwa na mungu na yeye ndie mwenye mamlaka juu ya kifo

A hapo juu, mungu aliweka kifo, B hapo chini shetani hakuruhusiwa kugusa nafsi ya ayubu.
 
1. Hapana, hapangi kifo wala siye aliyesababisha watu waanze kufa - ndiyo sababu anaahidi kuwapatia watu uzima wa nnmilele.
2. Watu wakifa hawaendi mahali popote panapoitwa peponi bali wanaenda kaburini - ndiyo maana kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini
3. Shetani ndiye aliyesababisha watu waanze kufa na kuvuruga makusudi ya Mungu (kwa muda tu) - ndiyo maana Mungu anaahidi kumfutilia mbali shetani na wote wanaomfuata hivi karibuni
4. Kifo cha binadamu si mapenzi ya Mungu - kazi ya Mungu haina makosa, yenye makosa si kazi yake.
Swali jingine.

Hii point no 2 ichapishie Biblia yake, Hii tunayoisoma sasahivi inakukataa 100%.

(A)Watu wakifa hawaendi mahali popote:
Unapozungumzia mtu unazungumzia mwili na roho, tufundishe baada ya mwili na roho kutengana roho inaenda wapi?

(B) kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini :Umesoma wapi? hakuna maelezo hayo kwenye Biblia! ila ninachojua mimi kwa muujibu wa maandiko tunaambiwa tutapewa mwili mpya, wewe hayo mafundisho umeyatoa wapi?

Zingatia sana Kuwa Mungu haokoi miili, bali anaokoa Roho..... Hata huwazi kuwa mwili ukikaa kaburini wiki tu funza tupu, baada ya miezi 6 mifupa, Makaburi yalifufuliwa kwenye ujenzi wa barabara mbuyuni, ilikuwa mifupa mitupu. Huyo mungu unayemzungumzia kuwa atafufua watu kutoka makaburini atakuta mifupa tu, labda useme atafufua skeleton. Lakini mungu wa biblia hii ninayoisoma mimi hana kazi na miili hii. kwasababu ameandaa miili mipya. "Mwili ni mavumbi utarudi mavumbini" shughuli yake imeisha. na "Roho itamrudia yeye alieitoa".
 
Hakuna uwezo wala nguvu juu yake yeye. Mungu asipotaka jambo litokee halitokei. Yeye ndiye mwenye mamlaka. Angetaka tusife tusingekufa. Kila nafsi itaonja umauti.....hili ni neno lake. Na neno la Mungu halianguki hata siku moja.
Ni mpango tu wa maisha aliouweka kwamba kukutana nae tutakufa kisha kwa uweza wake atatufufua.
Mungu ndiye mwenye mamlaka yote duniani na mbinguni na sayari zote. Asipotaka jambo halifanyiki.

Mungu kakataza dhambi,na amesema mshahara wa dhambi ni mauti kumpa option binadamu afanye dhambi au asifanye!! Unataka kutuambia Mungu ndio anawafanya binadamu wafanye dhambi wafe?? Umeiba umekamatwa umepigwa umekufa,utasema Mungu kataka ufe awali kakemea wizi?? Vifo vingine ni vya shetani.
 
Mkuu hapo kwenye red huoni kuwa unamfanya shetani kuwa na uwezo kuliko Mungu? Kama Mungu ana uwezo kuliko shetani kwa nini aruhusu shetani asababishe vifo?

Heshima kwako mkuu,napenda ujue kuwa uweza wa Mungu hauna mipaka,haulinganishwi na kitu chochote kile chenye uhai na kisicho na uhai,kilicho mbinguni juu ama duniani chini.

Sasa kwanini anaweza kuruhusu:
1. Ni kwajili ya upendo wake mkuu kwetu.Kuna wakati anaona bora aruhusu kifo,ili roho ikapumzike kwake kuliko kumuponya mtu ile hali akijua anawezakutenda dhambi baadaye na kukapotea milele.

2. Sijui kama unaisoma biblia,kama ndio unaiamini?Kwa kuwa ki-biblia nguvu za Mungu zinatenda kazi ndani ya mtu,na zinaachiliwa kwa njia ya kutamka(maombi). Efeso 3:20
n.k

Hivyo kwa kadiri tunavyomkaribia Mungu kwa maombi,ndivyo nguvu zake za ki-ulinzi juu yetu zinavyoongezeka, and vice versa.
Hata hivyo yapo mambo mengi ya kujifunza juu ya Mungu wetu,hatutayajua yote,tutamfahamu kwa sehemu tu,na kwa jinsi atakavyoendelea kujifunua kwetu kwa njia ya Yesu.

Asante mkuu.
 
Heshima kwako pia Mkuu. Naona bado sijauelewa huu uwezo alionao Mungu unaomfanya aweze kila kitu lakini anashindwa kumthibiti shetani ambaye ni kumbe wake mwenyewe. Kwenye pointi yako namba 1 inaonyesha kwa mara nyingine kuwa shetani anampa tabu Mungu kiasi kwamba badala ya kumsaidia kiumbe wake asitende dhambi anaamua kuwa heri kiumbe afe ili aokoe roho yake.
 
Vipi kuhusu ghosts/mizuka au roho ambazo huwatokea watu kwa madhumuni mbalimbali? Mi nahisi
ukifa ndio utaenda kujua huko mbele ya safari kukoje. Na ndio maana kila mtu anajibu kwa kutumia kitabu
chake kitakatifu ilhali kila kitabu kitakatifu kina imani tofauti. Kwa mfano wahindu wanaamini ukifa unazaliwa
upya kama mtu/mnyama/ n.k. Maisha baada ya kifo ni swala ambalo liko kiimani zaidi. Sijui wasioamini uwepo
wa Mungu nao wanamajibu gani kuhusu maisha baada ya kifo na kutoka kwenye rejea ipi:):).

Ukiangalia takwimu za hapo chini huwezi kuhitimisha kwamba ukweli wenyewe ni upi. Kwa hiyo
waweza endelea kuamini unachoamini au usubiri ufe ndio ukajue habari kamili.

Size of Major Religious Groups, 2012
ReligionPercent
Christianity  
31.5% (2 Billion)
Muslim  
23.2%(1.6 Billion)
Unaffiliated  
16.3%(1.1 Billion)
Hindu  
15.0%(376 Million)
Buddhist *  
7.1%
Folk  
5.9%
Other  
0.8%
Jewish  
0.2%
 
point no.2 kwamba watu wakifa wanaenda kaburini...je hiyo roho inakwenda wapi??? kwani hiyo roho ikitoka kwenye mwili ndo tunasema mtu kafa na hana budu kuzikwa..je hyo roho inazikwa nayo???huwa najiuliza pia bila majibu ya uhakika.
roho zote humrudia yeye aliyezitoa.
 
Kama ni kweli kwanini anampangia kifo mtoto mdogo ambae hata hajaanza kutenda dhambi na kuacha wenye dhambi.

Mkuu, hivi karibuni nilipewa somo kali sana juu ya hili suala na jamaa alikuwa anakuja kunitembea nyumbani kwa ajili ya mafundisho nilishangaa hadi nikaandika notes. Hebu ngoja nikupe na wewe uchambue mwenyewe logiki kali ya huyu jamaa. Ila inabidi usome maandiko yaliyoorodheshwa kwenye Biblia yako.

Mungu hapangi kifo cha mtu. Maandiko yanasema hata mtu mwovu sana Mungu hafurahii kuona anakufa (Ezekiel 18:23). Na pia Mungu hapendi kuona watu wakihuzunika (Maombolezo 3:33). Hivyo basi, kama Mungu hafurahii hata kifo cha mtu mwovu, wala hapendi kuona watu wakihuzunika, iweje basi awe ndie msababishi wa kifo ambacho kinahuzunisha sana watu, wanapopoteza baba, mama, kaka, dada, mume, mke au mtoto?

Kumbuka kwamba wakati ule Lazaro alipokufa, Yesu alihuzunika sana na hata kutoa machozi. Je, ni akili kufikiri kwamba Yesu angehuzunika hadi kutoa machozi kwa kitu ambacho ni baba yake amependa kufanya au mapenzi ya baba yake? Hiyo ingemaanisha kwamba Yesu hakubaliani na kile alichofanya baba yake, au kwamba Baba wa Yesu si mkweli kwamba hapendi kuhuzunisha watu, maana amemhuzunisha hata mwanae mpendwa wa pekee.

Sasa, nani anasababisha kifo? Kuna vitu viwili; chanzo cha kifo chochote kile, cha ugonjwa au uzee ni Shetani Ibilisi (Yohana 8:44). Shetani ndiye chanzo cha kifo kwa kuwa yeye ndie aliwadanganya Adamu na Hawa na matokeo yake watu tunakufa leo kutokana na dhambi ya urithi (Waroma 5:12). Na pia shetani anasababisha vifo kwa kuchochea migongano ya jamii, hasira nk., kama kule Rwanda.

Lakini pia, pamoja na kwamba chanzo cha kifo ni Ibilisi, kuna vifo vingine ni suala la wakati na mahali, kama alivyoeleza Yesu juu ya wale watu walioangukiwa na ukuta pale Yerusalem (Luka 13:4). Lakini pia kuna vifo vya uzembe vya kujitakia, ambavyo wala sio vya asili na wala sio vya Ibilisi. Kwa mfano, ukiendesha gari huku umelewa ukapiga mzinga ukafa, kwa kweli huo ni uzembe wako wala huwezi kumlaumu shetani, japo ni kweli shetani ndiye aliyeleta kifo. Mtu akiweka sumu mezani na kwa hiari yako ukainywa ukijua ile ni sumu, huwezi kumlaumu kwa kunywa sumu kwa kuwa ulijua ile ni sumu, japo ni kweli kuna lawama kiasi zitamwendea yule aliyeileta sumu.

Hivyo basi kwa kifupi, kifo ni adui mkubwa wa Mungu ndio maana anasema lazima akiondolee mbali wakati muafaka utakapofika (1Wakorintho15:26). Lakini ni dhambi kubwa kusema Mungu, ambaye ni mtakatifu sana asiyeweza kufanya au hata kuwaza ovu lolote, ndiye msababishi wa vifo (Yakobo 1:13 na Jobu 34:10).

Kwa mantiki hii basi, wale wote wanaosema kifo ni mapenzi ya Mungu (Bwana ametoa, Bwana ametwaa) Mungu anawaona wanaropoka mambo wasiyoyajua kwa kumsingizia vitu ambavyo chanzo chake ni shetani Ibilisi, na Mungu anasema wanaongea ujinga na atakuja kuwahukumu kwa kumsingizia vitu vya uongo, pamoja na kwamba utumbo wanaoongea wanafundishwa na viongozi wao na wanaishia kuongea ujinga mtupu (Isaya 9:16-17).

Ila sasa, usisahau kwamba Mungu anahukumu watu waovu kwa kutumia kifo. Ila katika hizo hukumu zake wanaokufa ni waovu tu kama adhabu yao, na baada ya kuwa amewapa nafasi na maonyo ya kutosha kujirekebisha. Vifo vinavyohusu hukumu za Mungu havichanganyi waovu na wema. Na huwa anafanya hivyo sio kwa matukio ya kila siku, bali katika siku maalumu anayoichagua. Katika historia ya wanadamu, ameshafanya hivyo kwa Wa-Misri ili kuwakomboa Waisraeli, Sodoma na Gomora, Gharika ya Nuhu, Angamizo la Yerusalemu baada ya kifo cha Yesu na matukio mengine mbali mbali kama wakati ule jamaa walimezwa na ardhi kwa kosa la kupinga uongozi wa Musa (Hesabu 16:31-32).
 
Shetani anaua watu na Mungu huruhusu na hata ugonjwa Mungu anaruhusu lakini mhusika mkuu shetani...soma Ayubu katika Biblia. Pia Mungu hamjaribu mtu bali tamaa ya mtu ndiyo tatizo....
Mungu anapenda wote watubu ili waokolewe
Mungu ni Pendo
 
Wana JF,

Jana nilikutana na mchungaji mmoja nikamuuliza swali kuwa ajali yoyote duniani inatokea kwa mapenzi ya Mungu au ni laana , hakunipa jibu zuri ila ilionekana naye hajui vizuri kwa kuwa alinijibu ni mapenzi ya Mungu, ni kamuuliza kama ni mapenzi ya Mungu iweje watu wapangiwe kifo cha pamoja, iweje mtoto mdogo ambaye ana hata zambi moja afe?

Mbona sasa waliosababisha wanatiwa nguvuni na kufungwa? Hata vifo vya Albino watu wanatafutia utajiri , kweli albino amepangiwa hivyo?

Tukafika mbali kuwa mbona nchi nyingi tajiri duniani kama Norway, Sweden Uswis watu hawafi kiasi hiki hao Mungu hawapendi? kwa kweli mjadala ulivunjika bila kupata majibu.

Nakaribisha maoni , ya kuridhisha na majibu yenye ukweli. Ila tuzingatie kuwa katika biblia Adam alipewa onyo asile tunda la katikati ya bustanini lenye mvuto sana kwani akila atakufa.

Sio kila kifo hupangwa na Mungu na ndo maana kupitia maandiko yake matakatifu akaahidi adhabu kali kwa wenye kudhurumu nafsi zao na za wenzao...mfano kwa wale wanaojinyonga, kunywa sumu na vifo vingine vinavyofanana na hvyo pia wale wanaua wenzao mfano mauaji ya albino.

Kwa hayo niliyoyatolea mfano wala sio mipango ya Mungu bali ni binadamu wenye ukatili na roho ya unyama huyafanya.

Pia vipo vyakizembe kama baadhi ya vifo vya magari na ndege ambavyo hutokea sehemu tofauti duniani. Uzembe huo aidha huletwa na waongozaji wa vyombo, wakaguzi wa vyombo hvyo na kuwepo kwa miundombinu mibovu.

Mfano ile ajali iliyotokea Iringa baada ya Kontena kudondokea basi la abiria na kuua wasio na batia ni miundombinu mibaya ndiyo ilikuwa chanzo.
 
Subiri ufe ndio utajua kama ni uzembe au ni mpango wa MUNGU
 
1. Hapana, hapangi kifo wala siye aliyesababisha watu waanze kufa - ndiyo sababu anaahidi kuwapatia watu uzima wa nnmilele.
2. Watu wakifa hawaendi mahali popote panapoitwa peponi bali wanaenda kaburini - ndiyo maana kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini
3. Shetani ndiye aliyesababisha watu waanze kufa na kuvuruga makusudi ya Mungu (kwa muda tu) - ndiyo maana Mungu anaahidi kumfutilia mbali shetani na wote wanaomfuata hivi karibuni
4. Kifo cha binadamu si mapenzi ya Mungu - kazi ya Mungu haina makosa, yenye makosa si kazi yake.
Swali jingine.

namfuata mchungaji sasa hivi kwa sababu tumebishana sana kuusu kifo kuwa mapenzi ya Mungu.
 
Ulieandika hii thread hebu kesho kapande jengo lenye gorofa Km kumi kisha jiachie kinachofata ni kifo sasa hapo umekufa kwa mapenzi ya Mungu au vp wale wanaokunywa Sumu kwa kujitakia Mungu anapanga hvo na kibaya anaejisababishia kifo km kujiua Mungu anamsubiri kumpa hukumu kali.

Kwanza kufa wakati mwengine ni uzembe na la pili mtu hufa kwa Mapenzi yake mwenyewe Mungu kutokana na alivopanga ila anaezungua kujiwahisha kuzimu anakwambia njoo.
 
Kuna vifo vingi Tanznia, Ajari yamoto (Umeme)(Itilafu) , mjamzito kufa na mtoto, Kudondokewa na magorofa, kuangukiwa na migodi.
Most of what you mentioned if not all, is self murder. God is not involved in that. In fact, God created you to live forever.
 
Back
Top Bottom