Je, kifo ni uzembe,bahati mbaya au mapenzi ya Mungu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, kifo ni uzembe,bahati mbaya au mapenzi ya Mungu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Emmanuel_mtui, Aug 19, 2012.

 1. E

  Emmanuel_mtui Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Samahani wana jamvi kama nitakuwa nimeingiza thread hii mahala ambapo siyo mahala pake, ila leo nilikuwa nimepanda daladala kukatokea mabishano yaliyo nishawisha mimi kwashirikisha ninyi tupate maoni.

  Kuna mtu alisema kuna binadamu wanakufa kwa kujitakia, au kupenda wao, akitumia mfano m2 unajua kuna magonjwa na unafanya ngono zembe.

  Mwingine akaulioza kwani wote walioathirika wanakufa kabla au baada ya kujua wameathirika,? Mwingine akasema mbona wanakufa kwa ajali na tunasema freemason.

  Kwamuda huo nikawa nimefika kituo changu cha kushuka nikaacha mjadala unanaendelea, wadau nini maoni yenu mkizingatia kuwa, kama ni ajali wapo waliopata ajali za kutisha na bado wapo hai, wapo waliougua na kuteseka sana bado wapo, na tulio wafahamu wazima au wenye uwezo walmekufa.

  Nawakilisha

   
 2. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Rejea vitabu vitakatifu utapata jibu.
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Kama ulivyo anza tumekusamehe, tambua sasa kuwa,

  KIFO NDIO ZAWADI KUBWA KULIKO ZOTE MUNGU AMEPATA KUMPA KIUMBE HAI YOYOTE.
   
 4. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  kufa ni sifa ya kiumbe hai chochote . as long as ni kiumbe hai basi ni lazima kife . KAMA NI MAPENZI YA MUNGU KIUM BE GANI AMBACHO MUNGU HAKUPENDA KIFE NA KIKO HAI HADI LEO????
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya ni uzembe
  Mapenzi ya mungu ni kama wale wanaoenda kulala wakiwa wameagana na jamaa wakiwa wazima, hawakuonesha dalili yoyote ya kuumwa na asubuhi jamaa zake wanamsubiri aamke lakini kimya. Wanagonga mlango kimya, wakiingia ndani jamaa amenyooka kama mtu wa jana au juzi. Chukulia, Mandela kwa umri alionao akiondoka ni mapenzi ya Mungu.(Mandela anapatiwa matibabu lakini kuna siku viungo vitakataa dawa)

  Lakin hawa katika hii link https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo/310381-abiria-wamgomea-dereva-wa-al-saedy-high-class-t322-ddp-kisa-mlevi-kutoka-kilombero-dar.html wangekubali dereva aliyelewa aendeshe na basi kupata ajali na vikatokea vifo basi huo ni uzembe au ndio bahati mbaya yenyewe.....bahati mbaya maana yake uzembe. Au ajali ni uzembe. Ukichunguza ajali yoyote utagundua kuna uzembe ulifanyika.
   
 6. M

  Molembe JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2014
  Joined: Dec 25, 2012
  Messages: 7,746
  Likes Received: 4,234
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli kwanini anampangia kifo mtoto mdogo ambae hata hajaanza kutenda dhambi na kuacha wenye dhambi.
   
 7. chaUkucha

  chaUkucha JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2014
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 3,223
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  duh! aisee umefikiria nini kusema ivyo?!
   
 8. J

  James Kasonda Member

  #8
  Jun 2, 2014
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  1. Hapana, hapangi kifo wala siye aliyesababisha watu waanze kufa - ndiyo sababu anaahidi kuwapatia watu uzima wa nnmilele.
  2. Watu wakifa hawaendi mahali popote panapoitwa peponi bali wanaenda kaburini - ndiyo maana kuna siku ya kuwafufua watu toka makaburini
  3. Shetani ndiye aliyesababisha watu waanze kufa na kuvuruga makusudi ya Mungu (kwa muda tu) - ndiyo maana Mungu anaahidi kumfutilia mbali shetani na wote wanaomfuata hivi karibuni
  4. Kifo cha binadamu si mapenzi ya Mungu - kazi ya Mungu haina makosa, yenye makosa si kazi yake.
  Swali jingine.
   
 9. michosho

  michosho JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2014
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 454
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  point no.2 kwamba watu wakifa wanaenda kaburini...je hiyo roho inakwenda wapi??? kwani hiyo roho ikitoka kwenye mwili ndo tunasema mtu kafa na hana budu kuzikwa..je hyo roho inazikwa nayo???huwa najiuliza pia bila majibu ya uhakika.

   
 10. Makamee

  Makamee JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2014
  Joined: Nov 29, 2013
  Messages: 2,005
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mwenyenzimungu hakika yeye ni mwingi wa Hekma,Mwenye nguvu,
  basi na atusamehe sisi wakosefu tunaohoji uwezo na mipango yake muumba wetu.
  Hakika amesema kamwe mwanadamu hatojua
  1.hatojua lini atakufa
  2.wapi itafia
  3.nini itachuma kesho.
   
 11. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2014
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Baada ya mwanadamu kukaidi maagizo ya mungu mungu alisema kika nafsi itaonja mauti hivyo mungu ndio anayepsnga vifo vyetu
   
 12. aloycious

  aloycious JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2014
  Joined: Dec 17, 2012
  Messages: 5,522
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  wewe umekufa kwa ngoma Mungu kapanga kivipi?? Mungu tunamsingizia tuu mambo mengine!!
   
 13. c

  chief72 JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2014
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 567
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  tunachanganya nadhalia mbili hapa kifo, na sababu ya kifo, swala la kufa halina mjadala tareh ikifika mtu hufa, iwe kwa ukimwi malaria kagongwa na gar nk
   
 14. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2014
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  kwanini ukiwa mzee meno yanapukutika wakati ulikuwa na meno kama magurudumu ya trekta???
   
 15. Ishmael

  Ishmael JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2014
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Allah says: "He it is who created death and life so He may try you as to which of you is best in deeds." [Sûrah al-Mulk: 2]
   
 16. Ishmael

  Ishmael JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2014
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  [​IMG][​IMG]
   
 17. M

  Muhusika Member

  #17
  Jun 3, 2014
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Mungu hajawahi kufanya lolote bali binadamu. Hajawahi umba wala kupanga bali binadamu. Kifo kipo kabla ya chochote hakijaandikwa. Walioandika walifanya hivyo kwa kuona hali halisi. Vipi tembo na wanyama wengine walifanya kosa gani hadi nao wafe? TEMBO akiwa na malisho mazuri huishi hadi maika 70 ndio anakufa na kama si meno kuisha na kushindwa kula angeishi zaidi. Sisi tunakufa kwa sababu tumejipangia hivyo. Kama unabisha kula kwa utaratibu mwili utakavyo kama hujaishi miaka mingi pia na kupumzika.
   
 18. s

  st44273 JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2014
  Joined: Nov 3, 2013
  Messages: 329
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana nawe hapo namba 1,lakini no. 2. hakika mtu akifa kinachoenda kaburini ni mwili lakini roho huchukuliwa na kuwekwa sehemu ya mangojeo,yaani paradiso (peponi) kwa watakatifu na jehanumu ya mangojeo kwa wenye dhambi.

  Yesu akamwambia,Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi. (sio makaburini) Luka 23:43
  Zaidi angalia Ufunuo 20:4.

  Hapo no. 3 nakubaliana na wewe.

  Ni sahihi si mapenzi ya Mungu watu wafe,lakini kwa kadri dhambi zilivyozidi na miaka ya mwanadamu ilipungua hata kufikia 70.(Vinginevyo shetani anahusika kwa vifo visivyotarajiwa).

  Asante mkuu
   
 19. s

  st44273 JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2014
  Joined: Nov 3, 2013
  Messages: 329
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Ni kweli tunapozeeka lazima tufe(natural death),lakini vijana na watoto wanaweza kufa.(Ni shetani anayesababisha vifo visivyotarajiwa,sio Mungu,ingawa anaweza ruhusu.
   
 20. Excel

  Excel JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2014
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 18,888
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  huduma mbovu tu za afya ndiyo zinasababisha watoto kufa, wala sio Mungu...

  angalia nchi zilizoendelea, hakuna vifo vya ajabu ajabu, sasa huko tuseme Mungu anawapendelea ama vipi?

  Waafrika tuko rough katika field nyingi sana za maisha, ndiyo maana hatuishiwi shida!

  Kufa nako kunatengenezwa wakati mwingine.

  mtoto anakufa kwa malaria, twasingizia Mungu badala ya kutafuta chanzo na suluhu ya tatizo..
   
Loading...