Je, Kichwa Hiki Cha Habari Ni Tata?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Kichwa Hiki Cha Habari Ni Tata?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Steve Dii, Oct 13, 2007.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Napenda niseme kabisaa hapa mwanzo kuwa miye siyo mwanataaluma wa uandishi, ila niliposoma tu kichwa cha habari cha ifuatayo nikajisikia vibaya kinamna fulani hivi. Naomba uisome kwanza:

  Source link: IppMedia.

  Najua ni kweli kuwa nchi yetu inategemea misaada, lakini katika kichwa hicho cha habari misaada inaonekana kuhalalishwa kama njia mojawapo ya kuendesha maisha, na pia kichwa cha habari nakiona kinapamba picha moja ya wananchi ambao hawana njia nyinginezo tena za kujikomboa ila misaada ndiyo ya kufurahia. Je ndiyo hivi?!

  Hilo neno 'kulamba' ndiyo linalonitatiza. Miye naona aliyeweka hicho kichwa cha habari anasahau kuwa Tanzania ina 'masikini jeuri' ndani yake. Nikimaanisha kuwa maneno kama hayo juu yanahalalisha misaada lakini pia kudharilisha kinamna fulani hapo hapo. Sijui kwa kweli, labda ndiyo maana rafiki zangu wananiita masikini jeuri...

  Nakubali hizo pesa ni za matumizi muhimu sana kama zitafanya kazi yake ipasavyo, ila ni hicho kichwa cha habari ndiyo nina utata nacho miye. Sasa Je, wenzangu JF mnaweza kuniweka sawa katika hili au ni hisia zangu tu hazijakaa vizuri katika hili.

  SteveD.
   
Loading...