Haa haa haaa hii ni kali
Nakubaliana na wewe kabisa huu ni udini wa uwazi, na siyo hili tu watanzania tuna tabia ya udini kila tunachokifanya. Ukipita kwenye maofisi ya public utakuta wafanyakazi wameweka nyimbo za dini kwenye makompyuta yao, wengine wamevaa rozari, wengine wanasalimiana bwana yesu asifiwe, wengine wameweka miti ya krismass wengine wamevaa mabarakashia.
Na kosa kubwa sana ni pale serikali iliporuhusu dini kutoa huduma za elimu na afya kwa wananchi wake baada ya Uhuru. Kwa ufahamu wangu huduma hizi ni haki ya msingi ya binadamu na pia ni majukumu ya msingi ya serikali. Hivyo nilizani havikutakiwa vimilikiwe kidini au kikabila kama kweli Tanzania tulikusudia iwe secular state.
Nasikitika kuona ni too late, kusawazisha sasa hivi maana wengi wamelelewa huko, Udini, dini, udini, dini. Viongozi waliokuwepo wakati wa uhuru wamepoteza fursa ya kututengenezea taifa safi la Tanzania. Kwa ufupi hawakuweka misingi yoyote ya kuzuia udini. maana huwezi kuzuia kitu kwa kutumia mdomo tu ukifa jee watakaozaliwa baada ya wewe kufa nani atawazuia. tafakari.