BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Na Waandishi Wetu
HOFU imetanda. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kumeguka Zanzibar huku na Tanganyika kule hivyo kuweka Muungano mashakani.
Taarifa mjini hapa zinasema Rais Amani Abeid Karume amejiandaa kuasi kauli zake mwenyewe na hata za chama chake katika kufanikisha serikali ya umoja wa kitaifa Visiwani, hatua ambayo inaweza kukimega chama.
Kwa zaidi ya wiki mbili sasa, kumekuwa na tetesi kwamba kundi la wana-CCM na viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), wanashawishi Karume aongezewe muda wa miaka miwili au mitatu ili asimamie kile kinachoitwa azma yake.
Tayari umezuka upinzani ndani ya CCM pande zote mbili za Muungano kwamba Karume hawezi kuongezewa muda zaidi ya kipindi kinachoruhusiwa kikatiba. Hata hivyo, wachunguzi wa siasa mjini Zanzibar wanasema ili kuleta kile ambacho Karume na CUF wanadaiwa kutaka, siyo lazima iwe kwa njia ya kuongeza muda wa urais. Rais akiiva katika hoja hii, aweza kuanzisha serikali ya mseto hata kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, ameeleza mmoja wa wachambuzi.
Wachunguzi wanasema Rais Karume, iwapo ataamua, aweza kuvunja baraza lake la mawaziri na kuunda jipya ambalo linaweza kuwa na wawakilishi kutoka upinzani.
Hiyo haitakuwa mara ya kwanza kufanya mambo chapuchapu. Iliwahi kutokea wakati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume walipokuwa wanajadili jinsi ya kuunganisha Tanganyika na Zanzibar.
Mara baada ya Nyerere kujenga hoja ya muungano, Karume alinukuliwa akisema, Hilo naafiki. Wewe utakuwa rais wa muungano, mimi nitakuwa makamu. Basi, wakaishia hapo, ameeleza mzee mmoja mjini hapa muumini wa serikali ya umoja wa kitaifa.
Iwapo baadhi ya viongozi Zanzibar watasimama na Rais Karume, ambaye imeelezwa anaungwa amkono ba baadhi ya viongozi katika vikao vya juu vya CCM bara, kuna uwezekano wa chama kumeguka.
Ingawa CCM ilizaliwa miaka 13 baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964), chama kimekuwa mhimili mkubwa wa muungano. Kutenguka kwake kutaathiri, kwa vyovyote vile, uimara wa muungano.
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa alipoulizwa kuhusu jambo hilo alisema haraka, Siyajui hayo. Sijayasikia. Tusubiri tuone. Lakini siyo lazima sisi tufahamu; hayo ni mambo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Msekwa alisema hata hivyo, kwamba mambo haya hayaingii akilini na mimi sijayasikia popote pale. Msiandike uwongo. Kwa nini unakimbilia kupiga ramli? Wakati Msekwa anazuia MwanaHALISI kuandika taarifa hizi, alizungumza na magazeti ya serikali yaliyomnukuu akisema CCM haiwezi kuruhusu kipindi kingine cha utawala wa Rais Karume na kwamba hiyo itakuwa kuvunja katiba.
Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa CCM Zanzibar, mkakati wa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa, ni sehemu ya makubaliano kati ya Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.
Kumekuwa na mazungumzo kati ya Rais Karume na Maalim Seif. Mazungumzo yao ya pili nay a mwisho kufahamika yalifanyika ikulu ya Zanzibar mapema Desemba.
Wafuatiliaji wa masuala ya siasa Zanzibar wanasema kumekuwa na mashauriano kati ya viongozi hao wawili kwa takribani miezi mitano, lakini wamewahi kukutana mara mbili. Bali akizungumza na MwanaHALISI, juzi Jumatatu, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa, alisema kwa jinsi anavyofahamu, hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa kati ya Seif na Karume kuhusu kuongeza kipindi cha urais.
Alisema ingawa msemaji rasmi wa CUF kuhusu mazungumzo hayo ni Katibu Mkuu, Maalim Seif, kwa taarifa alizopewa yeye na kiongozi wake huyo, hakuna mahali alikoeleza kuhusu kuongeza kipindi cha urais.
Hayo ni mawazo ya watu wengine na si ya Maalim Seif wala CUF. Siwezi kusemea watu wa CCM lakini kwa upande wetu hakuna kitu kama hicho, alisema.
Jussa, hata hivyo, amenukuliwa na vyombo vingine vya habari juzi akisema ipo haja kufikiria kumwongezea muda Karume ili aongoze mabadiliko.
Alisema kama kungekuwa na kitu kama hicho, CUF isingesita kukisema hadharani kama ilivyofanya baada ya mazungumzo kati ya Seif na Karume.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya CUF zinasema kwamba kuna mpango wa kuandaa hoja binafsi itakayowasilishwa katika mkutano ujao wa Baraza la Wawakilishi na mjumbe mmoja wa CUF.
Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi ameliambia gazeti hili alipoulizwa uwezekano wa muda zaidi kwa rais, kuwa hakuna uwezekano wa kumwongezea muda Karume kwa sababu katiba inakataza.
Alisema katiba zote ya Muungano na Zanzibar zinataja rais kushika madaraka kwa vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja. Akimaliza anastaafu na kwamba hili la kuongezewa muda halikubaliki.
Dk. Mvungi amesema anachoweza kufanya Rais Karume ni kuweka mchakato bora wa kufikia kile ambacho anataka na kwamba muda wake ukiisha aache wengine wakiendeleze hicho.
Habari za ndani zinasema mpango wa kuwezesha Karume kusimamia mabadiliko unaungwa mkono na baadhi ya nchi wahisani. Haikufahamika ni nchi gani. Lakini Jussa alipoulizwa iwapo anaunga mkono Karume kuongezewa muda wa uongozi baada ya kumalizika kipindi chake kwa mujibu wa Katiba, alisema wakati ndio utakaoamua kuhusu hilo.
Kwa sasa kuna mambo mengi ya msingi kabla ya kujadili kuongeza muda wa uongozi. Kuna kuweka mfumo wa kulinda tulichokubaliana kwa sasa na mambo mengine ya haki za kidemokrasia na kiraia. Baada ya hapo, wakati utaamua kuhusu hilo, alisema. Kauli ya Jussa yaweza kumaanisha kuwa mpango huo upo lakini siyo jambo la hivi sasa; ni mpaka mipango mingine itekelezwe na huenda kadri ya makubaliano kati ya Karume na Maalim Seif.