Je, Karume amzunguuka Kikwete?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Na Waandishi Wetu

HOFU imetanda. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kumeguka – Zanzibar huku na Tanganyika kule – hivyo kuweka Muungano mashakani.

Taarifa mjini hapa zinasema Rais Amani Abeid Karume amejiandaa “kuasi kauli zake mwenyewe” na hata za chama chake katika kufanikisha serikali ya umoja wa kitaifa Visiwani, hatua ambayo inaweza kukimega chama.


Kwa zaidi ya wiki mbili sasa, kumekuwa na tetesi kwamba kundi la wana-CCM na viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), wanashawishi Karume aongezewe muda wa miaka miwili au mitatu ili asimamie kile kinachoitwa “azma yake.”


Tayari umezuka upinzani ndani ya CCM pande zote mbili za Muungano kwamba Karume hawezi kuongezewa muda zaidi ya kipindi kinachoruhusiwa kikatiba. Hata hivyo, wachunguzi wa siasa mjini Zanzibar wanasema ili kuleta kile ambacho Karume na CUF wanadaiwa kutaka, siyo lazima iwe kwa njia ya kuongeza muda wa urais. “Rais akiiva katika hoja hii, aweza kuanzisha serikali ya mseto hata kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu,” ameeleza mmoja wa wachambuzi.

Wachunguzi wanasema Rais Karume, iwapo ataamua, aweza kuvunja baraza lake la mawaziri na kuunda jipya ambalo linaweza kuwa na wawakilishi kutoka upinzani.

Hiyo haitakuwa mara ya kwanza kufanya mambo chapuchapu. Iliwahi kutokea wakati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume walipokuwa wanajadili jinsi ya kuunganisha Tanganyika na Zanzibar.


“Mara baada ya Nyerere kujenga hoja ya muungano, Karume alinukuliwa akisema, “Hilo naafiki. Wewe utakuwa rais wa muungano, mimi nitakuwa makamu. Basi, wakaishia hapo,” ameeleza mzee mmoja mjini hapa muumini wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Iwapo baadhi ya viongozi Zanzibar watasimama na Rais Karume, ambaye imeelezwa anaungwa amkono ba baadhi ya viongozi katika vikao vya juu vya CCM bara, kuna uwezekano wa chama kumeguka.

Ingawa CCM ilizaliwa miaka 13 baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964), chama kimekuwa mhimili mkubwa wa muungano. Kutenguka kwake kutaathiri, kwa vyovyote vile, uimara wa muungano.


Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa alipoulizwa kuhusu jambo hilo alisema haraka, “Siyajui hayo. Sijayasikia. Tusubiri tuone. Lakini siyo lazima sisi tufahamu; hayo ni mambo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.”


Msekwa alisema hata hivyo, kwamba “mambo haya hayaingii akilini na mimi sijayasikia popote pale. Msiandike uwongo. Kwa nini unakimbilia kupiga ramli?” Wakati Msekwa anazuia MwanaHALISI kuandika taarifa hizi, alizungumza na magazeti ya serikali yaliyomnukuu akisema CCM haiwezi kuruhusu kipindi kingine cha utawala wa Rais Karume na kwamba hiyo itakuwa kuvunja katiba.

Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa CCM Zanzibar, mkakati wa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa, ni sehemu ya makubaliano kati ya Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.

Kumekuwa na mazungumzo kati ya Rais Karume na Maalim Seif. Mazungumzo yao ya pili nay a mwisho kufahamika yalifanyika ikulu ya Zanzibar mapema Desemba.


Wafuatiliaji wa masuala ya siasa Zanzibar wanasema kumekuwa na mashauriano kati ya viongozi hao wawili kwa takribani miezi mitano, lakini wamewahi kukutana mara mbili. Bali akizungumza na MwanaHALISI, juzi Jumatatu, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa, alisema kwa jinsi anavyofahamu, hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa kati ya Seif na Karume kuhusu kuongeza kipindi cha urais.

Alisema ingawa msemaji rasmi wa CUF kuhusu mazungumzo hayo ni Katibu Mkuu, Maalim Seif, kwa taarifa alizopewa yeye na kiongozi wake huyo, hakuna mahali alikoeleza kuhusu kuongeza kipindi cha urais.

“Hayo ni mawazo ya watu wengine na si ya Maalim Seif wala CUF. Siwezi kusemea watu wa CCM lakini kwa upande wetu hakuna kitu kama hicho,” alisema.


Jussa, hata hivyo, amenukuliwa na vyombo vingine vya habari juzi akisema ipo haja kufikiria kumwongezea muda Karume ili aongoze “mabadiliko.”

Alisema kama kungekuwa na kitu kama hicho, CUF isingesita kukisema hadharani kama ilivyofanya baada ya mazungumzo kati ya Seif na Karume.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya CUF zinasema kwamba kuna mpango wa kuandaa hoja binafsi itakayowasilishwa katika mkutano ujao wa Baraza la Wawakilishi na mjumbe mmoja wa CUF.

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi ameliambia gazeti hili alipoulizwa uwezekano wa muda zaidi kwa rais, kuwa hakuna uwezekano wa kumwongezea muda Karume kwa sababu katiba inakataza.

Alisema katiba zote – ya Muungano na Zanzibar – zinataja rais kushika madaraka kwa vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja. Akimaliza anastaafu na kwamba hili la kuongezewa muda halikubaliki.

Dk. Mvungi amesema anachoweza kufanya Rais Karume ni kuweka mchakato bora wa kufikia kile ambacho anataka na kwamba muda wake ukiisha aache wengine wakiendeleze hicho.

Habari za ndani zinasema mpango wa kuwezesha Karume kusimamia “mabadiliko” unaungwa mkono na baadhi ya nchi wahisani. Haikufahamika ni nchi gani. Lakini Jussa alipoulizwa iwapo anaunga mkono Karume kuongezewa muda wa uongozi baada ya kumalizika kipindi chake kwa mujibu wa Katiba, alisema “wakati ndio utakaoamua kuhusu hilo.”

“Kwa sasa kuna mambo mengi ya msingi kabla ya kujadili kuongeza muda wa uongozi. Kuna kuweka mfumo wa kulinda tulichokubaliana kwa sasa na mambo mengine ya haki za kidemokrasia na kiraia. Baada ya hapo, wakati utaamua kuhusu hilo,” alisema. Kauli ya Jussa yaweza kumaanisha kuwa mpango huo upo lakini siyo jambo la hivi sasa; ni mpaka mipango mingine itekelezwe na huenda kadri ya makubaliano kati ya Karume na Maalim Seif.
 
Karume hamzunguki Kikwete, bali ni kuwa Karume is genuine kwenye kuumaliza mpasuko wa Zanzibar, amegundua Kikwete ni weak na ni hypocrite kwa kulitangazia Bunge kwenye ule mkutano wake wa kwanza mara baada ya kuchaguliwa, kumbe alitoa ahadi ambayo its only lip service.

Ili Karume afanikiwe. his only way is doing it the Zanzibar Style, revstyle, kwa kumside line JK na CCM bara.

Karume ameongea kitu na Seif, kitendo cha Seif kujitokeza hadharani na kutangaza kumtambua Karume, its not for nothing, sio kwa ile glasi ya maji pale Ikulu Zanzibar, there was something more to it than what was given out.

Kwavile Wanzanzibar wameshawastukia Wabara hawako genuine when it comes to Zanzibar interests, sasa wameamua kwa dhati kumaliza tofauti zao bila Kikwete, bila CCM.
 
Hivyo ndivyo inavyotakiwa. Matatizo ya Zanzibar yatatuliwe na Wanzanzibari wenyewe kwani ndiyo wanayajua vyema matatizo yao.
Kama Karume na Seif wameelewana na wanaona njia pekee ya kuyamaliza matatizo yao ni kumtema JK mimi naona sawa kabisa. JK na CCM yake atawaletea porojo na hadithi za Abunuwasi.
 
Hivyo ndivyo inavyotakiwa. Matatizo ya Zanzibar yatatuliwe na Wanzanzibari wenyewe kwani ndiyo wanayajua vyema matatizo yao.
Kama Karume na Seif wameelewana na wanaona njia pekee ya kuyamaliza matatizo yao ni kumtema JK mimi naona sawa kabisa. JK na CCM yake atawaletea porojo na hadithi za Abunuwasi.

Kwani JK ndiye aliyekuwa anawaletea Wazanzibari matatizo? Acha kutema upupu ndugu!
 
Kwani JK ndiye aliyekuwa anawaletea Wazanzibari matatizo? Acha kutema upupu ndugu!

Buchanan, Jakaya siye aliyewaletea wazenj matatizo lakini ndiye
aliyewapa matumaini kuwa wakati wa utawala wake angetatua matatizo yao ya kisiasa yaliyokuwa yanawasibu kwa muda mrefu!!Huu ni mwaka wa mwisho wa muhula wa kwanza wa Jakaya kutawala na muhula wa pili na wa mwisho wa Karume kutawala kufuatana na katiba; mpaka sasa hakuna lolote la maana la kuwapa matumaini wazenj kuwa matatizo yao ya kisiasa walioahidiwa yatapatiwa ufumbuzi. Kama kawaida yake Jakaya ameendelea kutoa ahadi tu hata huko ughaibuni anakokwenda kutalii kuwa angeyapatia ufumbuzi matatizo ya zenj; Karume na Seij wamegundua kua wao peke yao ndio wanaoweza kuyapatia ufumbuzi matatizo ya visiwa vyao. Kikwete kwa hulka yake sio mtatua matatizo yanayoikabili nchi yake na mara nyingi ndio maana huenda nje ya nchi kuyakimbia matatizo na kudhania yatajipatia ufumbuzi yenyewe, including haya ya zenj!!Ni kwamisingi hiyo Karume na Seif wameamua kuwaweka wabara kando katika kutafuta suluhu ya matatizo yao; hawa wabara mara nyingi ndio chanzo cha kukwamisha matakwa halisi ya wazenj!!
 
Kwa vyovyote vile, Karume hajamzunguka Rais wa JMT kwa kuingia makubaliano na CUF (Seif S. Hamad). Kitendo kilichofanyika ZNZ, kinaungwa mkono na wote wanaoitakia ZNZ hali bora ya kisiasa na pia ni kitu kinachowezekana tu, kwa makubaliano ya wahusika hao wawili.

Mimi sioni sababu ya kuongeza muda wa Rais wa Zanzibar ili kuweza kutekeleza makubaliano ambayo wamefikia miezi michache iliyopita. Kama kuna nia ya kutekeleza makubaliano hayo, wanaweza kuanza sasa. Ila ninachoamini kuwa ni cha msingi, ni kuweka usawa katika usimamizi wa siasa za Zanzibar, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila chama kina haki sawa ya kushinda uchaguzi.

Naamini S. S. Hamad anajua kuwa hilo ndilo jambo muhimu kabisa kwa Zanzibar, na hawezi kutaka tofauti na hilo. Labda kama kuna jingine tusilolijua.
 
Ili Karume afanikiwe. his only way is doing it the Zanzibar Style, revstyle, kwa kumside line JK na CCM bara.

Kwavile Wanzanzibar wameshawastukia Wabara hawako genuine when it comes to Zanzibar interests, sasa wameamua kwa dhati kumaliza tofauti zao bila Kikwete, bila CCM.

It can be done Zanzibar style. Be optimistic -bro.
 
hawa wabara mara nyingi ndio chanzo cha kukwamisha matakwa halisi ya wazenj!!

Matatizo ya Wazanzibari yaliletwa na Wazanzibari wenyewe na wameamua kuyamaliza wenyewe! Hizo lugha za vitisho zilizokuwa zinatolewa na akina Seif kwamba damu itamwagika, ngangari, nk na Wapemba kuanza kutafuta kujitenga ina maana walichukulia tuition Tanzania Bara? Na Seif alipokuwa anazunguka nchi mbali mbali kutaka Zanzibar inyimwe misaada alitumwa na Wabara? Kutokumtambua Karume na Wawakilishi wa CUF kugoma kuingia kwenye Vikao vya Baraza la Wawakilishi, tuition walichukulia bara?
Tafuteni njia ya amani ya kutatua matatizo kama walivyofanya Karume na Seif na kuancha visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu!
 
Ni wazi kwamba Karume kamzunguka mungwana, ameushitukia usanii wake. Kosa la kwanza alilolifanya JK ni kubadilisha kamati ya muafaka ilokuwepo wakati wa Mkapa kwa kuwaweka wasanii kina Makamba wakati anaelewa wazi kuwa uwezo wake ni mdogo, kisha akawajaza wabara badala ya wazanzibari wenyewe.

Kamati ya kina Mangula ilitatua mambo mengi ya msingi ikiwemo kuanzishwa kwa daftari la kudumu la wapigakura, tume huru ya uchaguzi na Seif kurudishiwa hadhi yake ya Waziri Kiongozi Mstaafu akilipwa stahili zake.

Ni wazi, kwa mtazamo wangu, Seif na Karume wametambua hitilafu hiyo hivyo kwa maslahi ya Wazanzibari na wao wenyewe hawakuwa na jingine zaidi ya kuketi pamoja na kuondoa tofauti zao.

Nawapongeza kwa hilo kwani usanii wa JK na CCM yake unawaumiza zaidi Wazanzibari, visiwa vinapewa taswira ya ukorofi wakati ni tatizo la watu wachache wanasiasa, katika mitafaruku yote hiyo ya kisiasa visiwani humo wanaoathirika ni Wakazi wake huku wenzao wa Bara waliendelea kufaidi pepo ya amani kama vile ni nchi mbili tofauti.

Mungwana ataongea kidiplomasia kuwapongeza lakini ndani ya nafsi yake atabaini kaumbuliwa.

Bravo Karume na Seif, tunahitaji amani ya kweli visiwani hivyo nanyi isije ikawa usanii wa kupisha uchaguzi.
 
Back
Top Bottom