SI KWELI Je, Kalonzo atafanya kazi na Ruto

SI KWELI Je, Kalonzo atafanya kazi na Ruto

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu ni ukweli kuwa Kalonzo alisema heri kufanya kazi na Rais Ruto kuliko kufanya kazi na Gachagua
1793725246315.jpg
 
Tunachokijua
Tunachokijua

Kalonzo Musyoka ni mmoja wa wanasiasa wakuu na wenye uzoefu mkubwa katika mrengo wa upinzani nchini Kenya. Katika siasa za sasa za upinzani, anachukuliwa kama mmoja wa viongozi wakuu wanaompinga Rais William Ruto na serikali ya Kenya Kwanza.

Madai

Kutipia mtandao wa facebook picha hii imekuwa ikisambaa ikiwa na madai kuwa Kalonzo alisema heri ashirikiane kisiasa na Rais Ruto badala na kufanya kazi na Rigathi Gachagua wa upizani.

Uhalisia wa madai haya

Kulingana na ufuatiliaji ulioufanya inabainika kuwa Kiongozi wa chama cha wiper hawajahi kutoa kauli hii. Mnamo Jumapili tarehe 1 Novemba 2026 Kalonzo Musyoka alikataa waziwazi mialiko ya kujiunga na Serikali ya Rais William Ruto akidai kuwa serikali ni ya walagai na kusisitiza kuwa watakutana kwenye debe katika uchaguzi mkuubwa 2027

Kalonzo amekuwa akifanya kazi kwa karibu na aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua na viongozi wa upizani ili kuunda upizani thabiti. Picha na nukuu hii zimesambazwa kwenye mtandao kama propaganda tu ya kisiasa na si kauli ya Kiongozi wa wiper Kalonzo Musyoka
Back
Top Bottom