Je, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ilivunjika February 05, 1977 au ilivunjika siku rubani alipokataa kupark ndege, January 17, 1977?

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Kuna thread humu inaonyesha Rubani Kenan Tony Makinda aliirusha ndege kupinga amri ya kupaki na akaipeleka D'Salaam siku Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ilipovunjika.

Ukikiaangali cheti kile kinaonyesha hiyo ndege aliirusha January 17, 1977.

Sasa kumbukumbu zingine zinasema EAC ilivunjika February 05, 1977 na siku hiyo ndege zilizuiwa kule Nairobi.

Tena kuzuiwa huko kuliiathiri Tanzania maana pale Arusha kulikuwa na sherehe ya miaka 10 ya Azimio la Arusha na wageni wengi walikuwa pale Arusha.

Wageni hao walikuwa wanasubiri ndege ziwachukue pale Arusha ili jioni wawahi Zanzibar kwenye sherehe ya kuzaliwa chama kipya cha CCM kilichorithi TANU na ASP.

Kuzuiwa kwa ndege zile kukafanya wageni wengi wakachelewa kufika Zanzibar na hivyo sherehe za kuzaliwa CCM wakazikosa.

Sasa, sijui kimetokea nini kwenye cheti hiki kuhusu tarehe. Hebu tujadili ukweli wa tarehe.

Soma hapa:

Nishani ya Ndege: Magufuli kampa Mzee Mapunda, Kikwete alimtunuku Tony Makinda - JamiiForums
 
Back
Top Bottom