Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,217
- 3,125
Wengi wanafiki tu.Wewe leo hii mfano uteuliwe ubunge,halafu upewe wizara utachomoa?Wengi wapiga kelele JF kwavile wako nje ya system,lakini wakikatiwa ulaji ndiyo hao watakuwa wakwanza kuifisadi nchi.
Kasema wazi kabisa labda wewe ndio hukumsoma vizuri..wengi wetu tumekimbilia kujibu hii post bola tafakari mzuri, mtoa mada hajaiweka vizuri, wadhifa upi? maana hata ubunge ni wadhifa na CUF wameukubali.
mimi sioni tatizo ni nini hasa hapa
mkuu nyadhifa ni dhana pana sana haiishii ktk uwaziri na mkuu wa mashirika.Kasema wazi kabisa labda wewe ndio hukumsoma vizuri..
Ukiwa kama mwana JF ambaye unataka mabadiliko ya kweli kwa watanzania, leo hii JK anakuteua kushika wadhifa fulani serikalini au katika shirika la umma; je utakubali? Kama ndio au hapana, tupe sababu za msingi! Ulimwengu alikwisha wahi mkatalia Mkapa!!
Duh mkuu wangu swali kaliuliza jamaa kinachotakiwa ni sisi kujibu na kutoa sababu..muhimu alosema mtoa mada ni ajira seriklaini au ktk mashirika ya Umma!mkuu nyadhifa ni dhana pana sana haiishii ktk uwaziri na mkuu wa mashirika.
anyway kwanini ukatae?
Gembeif i will be a supervisor..
1.Nitakuwa mkali kwa wezi wote na sitawaonea haya hata kama ni wakongwe wa chama
2.Nitahakikisah mabadiliko makubwa ya sheria yanafanyika ili yaendana na kasi ya kuleta mabadiliko
3.Watu wote ambao hawana uwezo wa kuleta mabadiliko nitawang'oa,itakuwa siyo serikali ya kulipana fadhila..
Kuchukua kazi ya kuteuliwa ni aina nyingine tu UFISADI as simple as that.Kuna haja ya kutumia akili pana. Mimi ni mwananchi. Raisi kanipa kazi ya kutumikia wananchi. Nitaikubali bila hata remorse. Nitaifanya kwa uadilifu hata kama zipo forces without zinataka nipindishe. Nikiona sivyo nitamrudishia kazi yake. Simple and straight forward. Hii ishu kuwa watumishi wote serkalini ni mafisadi siyo sahihi. Wapo wachapa kazi wazuri tu.
Wengi wanafiki tu.Wewe leo hii mfano uteuliwe ubunge,halafu upewe wizara utachomoa?Wengi wapiga kelele JF kwavile wako nje ya system,lakini wakikatiwa ulaji ndiyo hao watakuwa wakwanza kuifisadi nchi.
Mkuu ya kweli haya?... Je akikuteuwa kuwa mshauri wake vipi bado utakataa na kwa nini?...P53 lingekuwa jambo la maana sana kama ungeongelea nafsi yako kwanza ingawa jibu lako tu laonyesha kuwa wewe ni mojawao. Ni vizuri ujue kuwa kuna watanzania wengi tu ambao wamekataa toka siku nyingi tu kuhusishwa kwa namna yoyote na huu utawala dhalimu. Kwangu mimi kwa mfano uteuzi wowote ule wa JK nitauona kama tusi na sitachukua hata dakika moja kuufikiria. Najua mtaguna, nyie mlio tayari hata kulala makaburini kulilia hizo nafasi lakini kaa ukijua kuwa wapo wenye msimamo tofauti na mimi ni mojawapo.
Mtu yeyote akiteuliwa na rais kushika madaraka bila shaka atayakubali isipokuwa rais mwenyewe hawezi kumteua mtu yeyote asiyekuwa mwanachama wa CCM kushika madaraka ya uongozi ngazi ya juu ya uongozi wa serikali kutokana na mfumo wa Kijamaa tulokuwa nao..
Toka enzi ya Mwalimu kiongozi yeyote alilazimika kujiunga na chama kwanza ili kupewa wadhifa wa juu serikalini au mashika ya Umma..Hivyo ni swala la kuuliza - Je, rais anaweza kumteua mtu kushika wadhifa serikalini au shirika la Umma hali mtu huyo ni Mpinzani wa siasa za chama CCM?