Je ingekuwa wewe ungefanyaje ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ingekuwa wewe ungefanyaje ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chamkoroma, Feb 21, 2011.

 1. C

  Chamkoroma Senior Member

  #1
  Feb 21, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukimwi umesababisha mke wangu aniache” Send to a friend Thursday, 17 February 2011 19:54 0diggsdigg

  Tumaini Msowoya

  “Sitaisahau siku niliporejea nyumbani kwangu nikitokea hospitali kupima Virusi Vya Ugonjwa wa Ukimwi. Hiyo ndiyo siku pekee niliyosikia uchungu baada ya mke wangu kunikataa kisa nimekutwa na maambukizi ya VVU, aliondoka na mpaka leo sijui yupo wapi!

  Ndivyo, Hery Chang’a mkazi wa kijiji cha Mazombe, Ilula Wilayani Kilolo ambaye alipima na kukutwa na maambukizi ya VVU mwaka 2007, alivyoanza kunieleza.

  Chang’a ambaye ni fundi seremala na mkulima wa nyanya katika kijiji hicho anasema haikuwa rahisi kwake kuikabili hali hiyo hasa pale mkewe alipoamua kumtoroka, kisa hawezi kuishi na mwanaume mwenye maambukizi.

  Chang’a anasema mkewe aliamini kwamba, kuishi na mtu mwenye VVU ni sawa na kujitafutia kifo na kwamba aliamua kufanya vile akiamini kwamba, itakuwa njia pekee ya kumfanya awe salama.

  Ilikuwaje akaamua kwenda kupima?

  Miaka yote ya maisha yao, Chang’a na mkewe walikuwa wakiishi maisha ya amani na furaha. Walijaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume mwenye afya njema.

  Chang’a anasema miaka michache baada ya kumpata mtoto huyo ndani ya ndoa yao, hali yake ya afya ilianza kubadilika kwa kuugua mara kwa mara, magonjwa tofauti.


  “Nilianza kuumwa kila siku, mara malaria, mara kifua na mengine mengi na kila nikitibiwa ugonjwa huu, mwingine unaibuka. Nilikwenda kwa waganga wa jadi lakini sikupata nafuu yoyote zaidi ya kutumia gharama kubwa bila manufaa yoyote,” anasema.

  Mwaka 2007, Changa alikuwa na hali mbaya zaidi kiasi cha kushindwa hata kuamka kitandani. Wanaomuuguza walimua kumpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu na akiwa huko, aliamua kupima VVU ili ajue ikiwa ana maambukizi au lah.

  “Nilipima na nikapewa majibu yangu, nilinyong’onyea sana, nilijua mwisho wa maisha yangu umefika lakini nilijipa moyo kwani niliamini mke wangu ananipenda na atanitia moyo pale atakapoijua afya yangu.”


  Anasema ilikuwa tofauti na hisia zake kwani, alipomueleza mkewe juu ya afya yake, hakumuelewa hata kidogo badala yake alikuwa mkali akiamini kwamba kuugua kwake kumetokea na tabia yake ya kutotulia jambo ambalo lilimfanya aondoke.

  “Nilimbembeleza sana nikimwambia asiniache, ila apime kwanza ili aijue afya yake ndipo afanye maamuzi anayotaka, alikataa, akaamua kuondoka bila kupima sijui kama amewahi kupima afya yake kwani tangua aniache, sijawahi kumuona tena ila nasikia yupo jijini Dar es Salaam,” anasema na kuongeza.

  “Niliumia kuondoka kwake, sikuwa na jinsi tena kwani kwa wakati huo hali yangu ilikuwa mbaya sana. Nilipiga moyo konde na nikaendelea na tiba, baadaye nilianza kutumia dawa za kurefusha maisha (ARVs) ambazo zilianza kunipa nafuu. Kilichokuwa kikiniuma ni ule unyanyapaa nilokuwa nikiupata toka kwa watu ambao wanaamini kwamba, mwenye ukimwi ni mtenda dhambi”.

  Anasema wakati wote toka mkewe aondoke alikuwa akiuguzwa na ndugu zake na kwamba kadri siku zilivyozidi kusogea ndivyo afya yake ilivyozidi kutengemaa kutokana na matumizi ya dawa.

  Anasema jambo lake la kwanza ilikuwa ni kuacha yale yote yaliyokatazwa na wataalamu wa afya, kubwa ikiwa unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na ngono zembe.

  “Sio kwamba nilikuwa muhuni sana ndio maana nikapata ukimwi kama mke wangu alivyofikiri, sijui niliupataje lakini ninachojua ni kwamba, nahitaji kuishi maisha mengine ya kumsahau kabisa ili afya yangu itengemae, nimeamua kuachana kabisa na pombe, sigara na ngono kwa sababu naamini vitu hivi vitakatisha ndoto zangu za kimaisha,” anasema.


  Shughuli zake…

  Imepita miaka mitatu tangu mke wa Chang’a aondoke. Jambo hilo limeitawanya familia yake kwani kutokana na afya aliyokuwa nayo kwa wakati huo hakuwa na uwezo wa kumlea mwanawe, hivyo kuamua kumpeleka kwa bibi yake.

  Alianza maisha mapya ya upweke, japo alipatiwa ushauri jinsi gani anaweza kuishi ili aweze kutimiza ndoto zake na kwamba kuwa na maambukizi ya VVU sio mwisho wa maisha.

  Mwaka 2009, Chang’a alijiunga na moja ya vikundi cha akiba na mikopo maarufu kwa jina la SILC, ambacho kilianzishwa kwa lengo la kuyasaidia makundi maalum, wakiwemo watu wanaoishi na VVU kupata njia za kujikwamua kiuchumi.

  Anasema alijiunga na kikundi hicho baada ya kubaini kuwa akiwa huko, ataweza kukutana na wenzake wenye hali kama yake, hivyo kuwa rahisi kwao kutiana moyo huku wakiendelea na kazi, ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

  “Vikundi hivi vimelenga kutuinua kiuchumi tuliokuwa tumekata tamaa kutokana na hali zetu, nilijiunga huku nikiamini nitafanikiwa kiuchumi na kiafya kwani, sitakuwa na mawazo tena,” anasema.

  Anasema wakati anajiunga na kikundi hicho tayari alikuwa na afya njema kutokana na kwamba alikuwa akitumia ARVs na kwamba, kwa mtu asiyemjua haikuwa rahisi kwake kuamini kwamba yeye ndiye yule ambaye aliwahi kukata tamaa baada ya kupata majibu kwamba anaishi na VVU.

  “Nilirejea tena kwenye kazi zangu za awali za kilimo cha nyanya na useremala. Ninafanya kazi kwa bidii kuliko hata hapo awali, kwani mahitaji yangu yamekuwa makubwa, nahitaji chakula kizuri, kulala mahali pazuri na hivi vitu nisingeweza kuvipata kama nisingefanya kazi kwa bidii,” anasema.

  Afisa mtendaji wa kata ya Mazombe, Joseph Nyoni anasema kuwa vikundi vya SILC katika kijiji chake, vimesaidia kuinua kipato cha wananchi wake ambao awali walikata tamaa kimaisha, wakiwemo wagonjwa wa ukimwi na watu wwenye maambukizi ya VVU.

  “Vikundi hivi vililenga makundi maalum ambayo yalikata tamaa kiuchumi kutokana na matatizo mengi yanayowakabili likiwemo janga hili la ukimwi. Hivi sasa wengi wamefanikiwa kwani kijiji kina vikundi vitano ambavyo vimekuwa na uhakika wa mtaji,” anasema

  Mwalimu wa SILC anasema kuwa eneo hilo linavikundi vitano, vyenye akiba ya Sh30 milioni na kwamba wanachama wake wamefanikiwa kujenga, kununua vyombo vya ndani kama magodoro, kuendeleza biashara na shughuli za kilimo.

  Miongoni mwa wanachama hao ni pamoja na Chang’a ambaye anasema kuwa aliweka akiba ya kutosha katika kikundi chake, na mwaka huu, amefanikiwa kupata fedha zaidi ya Sh1 milioni ambayo ameitumia kwa ajili ya kukarabati nyumba yake, kuongeza mtaji wa kilimo na kazi yake ya ufundi seremala.


  Anasema kuwa amekuwa akilima nyanya kila msimu huku akiendelea na kazi yake ya ufundi seremala kutokana na fedha anazopata toka kwenye kikundi hicho.

  Mahusiano
  “Naogopa sana, tangu mke wangu aondoke sijawahi kuwa na mwanamke yeyote yule na zaidi huwa najitahidi kutoa elimu juu ya Ukimwi kwani bado watu wengi hawafahamu vizuri na ndio maana hata mke wangu alininyanyapaa pale nilimpomweleza kwamba nina maambukizi,” anasema.

  Anasema ameamua kutulia ili aweze kufanya kazi kwa bidii na kuweza kumsomesha mwanawe, ambaye bado anaishi kwa bibi yake na kwamba, anaamini kuwa anaweza kuishi miaka mingi kuliko hata wale ambao hawana maambukizi
   
Loading...