Je, inawezekana kuomba uhamisho kabla ya kuthibitishwa kazini?

mamyd

Member
Mar 28, 2023
22
49
Habari zenu,

Naomba wenye uelewa wa haya mambo ya Serikali mtoe ideas kuhusu swala zima la mtu kutaka kuhama kabla ya kuthibitishwa kazini, hii imekaaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka uthibitishwe kazini ndo unaweza kuomba uhamisho.Sababu ukipata nafasi unapotaka kuhamia lazima utaambatanisha barua ulojibiwa kuna nafasi,vyeti pamoja na barua ya kuthibitishwa kazini ulipo sasa kwenda kwa katibu mkuu utumishi.

Bila hivyo ni vigumu labda kama una mtu mkubwa na connection utumishi akusaidie kukuhamisha. Ushauri kwako malizia tu kwanza probabation period ulipo ndo uhangaike na uhamisho.

Lasivyo boss wako atakuona mguu nje mguu ndan na utanyimwa fursa zitakazojitokeza hapo kazini ulipo kwa kutaka kuondoka mapema hivyo
 
Labda uwe na tatizo la kiafya lililothibishwa na hospital kubwa kwamba huwezi huishi kwenye kituo cha kazi hivyo unahitaji uhamisho
 
Hahahaha inawezekana sana saaana SEMA Huwa jamaa wanadanganya tu watu. Confirmation Haina connection yoyote na kituo Cha KAZI, system ni Ile ile tu
 
Back
Top Bottom