turbocharger
Member
- Dec 14, 2016
- 52
- 67
Habarini wanajukwaa siku si nyingi nimekutana na changamoto ya wafugaji kuvamia shambalangu na kuharibu mazao pamoja na bwawa langu la samaki. Nilifanikiwa kuripoti polisi na baada ya siku mbili niliwatia nguvuni kwa ushirikiano na polisi kesi ipo mahakamani na bado sijafunga ushahidi wangu lakini kwa uelekeo mtuhumiwa anaweza akafungwa.
Nia yangu ni kulipwa madhara yaliyotokana na uharibifu kabla mtuhumiwa hajafungwa Je ninaweza kufungua shauri la madai yaani civil huku kesi ya jinai ikiendelea? Kama jibu ni ndio je kifungu kipi kinanipa haki hiyo au precedent yoyote ya kitu kama hicho. Msaada tafadhali.
Sent using Jamii Forums mobile app