Je huyu ni mtoto wangu au?

Mwanaweja

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
3,575
521
Pole wana Jf na shughuli za ujenzi wa taifa. Naomba msaada wenu wa kimawazo kwa kujaribu kunijibu kwa umakini zaidi. Miaka ya nyuma nilikuwa na girl friend kwa muda wazaidi ya miaka 2 lakini kulingana na majukumu ya shule nilikuwa naonana naye wakati wa likizo tu ikatokea likizo moja niliporudi nikapata taarifa alikuwa anatembea na jamaa mwingine nikaamua kufanya uchunguzi ili nijue nini kinaendelea lakini kwa kuwa nilikuwa ndiyo nimerudi likizo nikaamua kukaa kama mwezi bila kuwa naye karibu mpaka nilipopata ukweli wanilichosikia. Kweli binti alikuwa anatembea na mvulana mmoja hapo kijijini akaja nilimuuliza akakubali na akaomba msamaha lakini kwa kuwa mimi nilikuwa nampenda nikamsamehe. Cha ajabu ndani ya wiki 2 binti baada ya kukutana alisema anaujauzito wangu mimi sikukataa sana ila nilimuuliza maswali mengi sana hata kutaka kwenda kumpima laikini kwa kuwa likizo ilikuwa inaelekea mwishoni niliamua kurudi shule. Wakati nikiwa shule binti aliendelea kulea mimba wazazi wake walipojua yuko mimba wakamuuliza ni ya nani akasema ni yangu kukawepo na ubishani kati ya wazazi wangu na wazazi wake. Kwa hiyo binti kaendela kulea mimba hadi ilipofikisha miezi 8 ikapelekwa kwa jamaa aliyekuwa anatembea naye nikiwa shuleni.
Niliporudi likizo nikuta alishajifungua mtoto wa kiume,ndipo yule binti alipo amua kuanza kunifanyia mambo ya kimazingara kwa kunitamkia atahakikisha ameniua na kweli mwaka huo nilipata zaidi ya ajali 3 na ajali moja ilikuwa mbaya sana iliua watu 15 maeneo ya Nyanguge Magu. Lakini Mungu aliniepushia mbali na ajali hiyo. Nilipo maliza O'level nilichanguliwa kwenda Mbeya technical collage niliondoka 2000 kuelekea mbeya sikurudi hadi nilipomaliza shule na kupata kazi huko huko Mbeya. Mwaka 2005 nilirudi nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya kwenda kusoma first degree. Sikuweza kurudi nyumbani tena lakini baada ya kumaliza masomo niliamua kurudi nyumbani ndipo nilipokutana na huyu mwanamke (girl friend) aliye olewa na huyo jamaa aliyekuwa anatembea naye nikiwa shule na wana watoto 5 akiwemo na huyo mwenye utata.
Huyu mama aliposikia nimekuja mwaka 2009 alifunga safari kuja mpaka nyumbani kwa wazazi wangu natukaa tukaongea alisema huyo mtoto ni wa kwangu kwa hiyo natakiwa ni muhudumie. Nilipomuliza inakuwaje ni hudumie mtoto aliye na baba yake yeye akasema ni mtoto wangu na wazazi wake ndio walimlazimisha kuolewa na jamaa.
msaada kwenu wa JF
1. Nilianza kutembea naye tena 1/1/1997 baada ya kurudi likizo na alijifungua tarehe 17/8/1997 na mtoto alikuwa amekamilika je, huyo ni mtoto wangu?
2. Mtoto mpaka ninavyoandika anatumia jina la jamaa je, itakuwaje hapo?
3.Je, mama huyu aliyetaka kuniua na alishanisababishia matatizo ndani ya mwili wangu itakuwaje? japo hata aliomba msamaha kwa yote aliyoyatenda juu yangu lakini roho bado inauma sana hasa ninapokumbuka aliyoyatenda kwangu.
nawasilisha nahitaji msaada wenu wamawazo maana mtoto ndio amemaliza darasa la saba mwaka huu anahitaji kwenda shule je ni muhudumie na kwenda kupima DNA naona kama nikupoteza hela afadhali nikumpatia hiyo hela aende shule
 

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,195
1,336
Mkuu kwa kutoa utata wa huyo mama kukusumbua na kukuletea shida pimeni DNA
Kwa kutoa msaada hata kama mtoto sio wako unaweza kuchangia masomo yake...

[h=2]Serenity Prayer...[/h]"Lord grant me the serenity to accept the things I cannot change, the courage to change the things I can, and the wisdom to know the difference.
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,773
23,063
ulianza kutembea nae tena tat 1/1, kajifungua tar 17/8 = miezi 7.5.
Swali je alijifungua mtoto njiti?

Full utata
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,802
94,311
mimi niko curious na hiyo ya kutaka kukua na kusababisha ajali iliyoua watu 15

duhh so hizi ajali zina siri nyingi???????
 

Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,323
9,965
Mkuu siku hizi DNA nasikia mpaka uwe na court order maana watu washataka kuuana pale ocean road.Kama uko sirias na DNA tafuta mwanasheria akusaidie kupata hiyo amri ya mahakama,lakini ujue itabidi na consent ya mama ipatikane maana yeye ndo mwenye custody.Lakini by the way we nae kwanini ulianza kuchovya,tena bila condom wakati ungali mtoto mdogo maana kama ulimaliza o level 2000 ina maana 1997 you were hardly 14 or 15(form 2),du vijana nyie!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom