Je, huyu mwanaume ana malengo?

Je, huyu mwanaume ana malengo?

Jamani habari zenu,
Naomba ushauri kwa niaba ya rafiki yangu mmoja amejikuta yupo dilema juu ya haya mahusiano yake.

Amekua kwenye mahusiano na mwanaume kwa miaka miwili sasa. Mwanaume huyo hajawahi kumsaidia kwa chochote wa kumpa chochote huyo mwanamke , hata chokoleti zawadi hajawahi.

Mwanaume huyo anachojua ni kwenda nyumbani kwa mdada kula na kulala na sometimes mdada akisafiri , mwanaume huyo anamuangalizia nyumba na vinginevyo.

Jamaa huyo amekua akimdanganya mdada kwa nyamati tofauti tofauti juu ya suala la ndoa ama kutambulishwa kwao, alimdanganya huyo mdada kwamba mwezi wa nne 2022, atamtambulisha na muda ulivofika jamaa akabaki kimyaaaa, baadae akamwambia mwezi wa nane anaona jamaa haongelei lolote kuhusu hilo jambo.

Mdada wa watu amechoka sasa, haelewi kma jamaa anampenda au anamtumia tu. Jamaa hataki story za ndoa akigusiwa ni kama ana panic. Jamaa bado anaishi kwao anavyosema so akija kwa huyu mdada ni kama anajificha ficha. Anawadanganya kwao yupo kazini shifti ya usiku.

Inshort huyo dada haelewi position yake na hajui anamuulizaje zaidi huyo mkaka.

Na mkaka huyo amekua hodari ku hack simu ya mdada na kufatilia msgs na maongezi yote. Incase mdada akichati na mwanaume hata kidogo jamaa anagundua nakuja kumwambia kila kitu.

Anaomba ushaurikwa umri wake umeenda na yeye anataka ndoa na jamaa hamuelewi kabisa. Je hapo kuna mapenzi? Au jamaa anapitisha muda tu?
Jamaa amependa vya dezo akimaliza hapo atatafuta chaguo la moyo wake na rafiki ako atabaki doro, usiache kuleta mrejesho yakitimia.
 
Amuacheje wakati yeye halipi, si kitumbua kitamuozea 😂😂😂 demu mbaya akiwa na bwana HB hawezi kumuacha kizembe, atalalamika tu which is a common thing na hata akiachwa ataanza kulia lia allover the internet. Cc rubi the artist!
Yap! Nafikiri shida ipo hapo.
 
Sisi wataalamu wa lugha akrama ya kiswahili au wa lumbi wa lugha tumeshajua huyo mdada unaemsema ni wewe mwenyewe umeamua kumlea marioo baada ya kuona age inaenda alafu unamlazimisha akuoe inabidi umtafutie na mahari sasa
Baada ya kusema hayo naomba nikuage naruka nikiyeyuka huku nikiweweseka kiuwazim
 
MBONA MWANAUME AANAWEZA KAA NA MWANAMKE MIAKA 10 BILA MCHANGO NA IKAWA FRESH TU, ILA WEWE KUKAA NAYE 2 YEARS HUYO JAMAA Unasema hana malengo kivipi?
Vumilianeni kuna baraka mbele!
Huenda jamaa hana maisha! Hana mchongo!

Unaweza sema kwann hajikujitambulisha hata kama hana hela?
JIBU mwanaume asipokuwa na kipato, hata kama anakupenda huwa HANA AMAN MOYONI ingawa usoni anatabasam kiume!
Nguvu ya mwanaume ili amiliki imefichwa kwenye mamlaka! Sasa huyo hata kama anakupenda kwasababu hana mchongo anakosa nguvu ya kimamlaka ili kuanza huo mchakato wa ndoa!

Ukimuacha huyo ndipo utakutana na boya zaidi ya hilo!
Boya linaweza kuwa jizi, tapeli, au lenye ugonjwa was ukimwi litakuambukiza likuhonge na mihela mfe!
Kukaa na MTU miaka miwili bila kuachana siyo jambo dogo huenda anafaa ila tatizo umeanza kumlinganisha na wrngine ndo shida!
Ushauri wangu mvumilie halafu fuatilie jamaa ujue kipato chake na umwambie hikohiko kidogo umelidhika nacho! Utamuongezea nguvu ya kupambana
 
Jamaa anakupenda wewe muandika thread. Wala hakuchezei. Sio fara aadanganye kwao aje kwako.
Sio fara usafiri aje kwako.
Sio fara akufatilie msg zako.
Ana nia na wewe... shida ni kwamba hana mchongo. Na ana hofu anakupeleka vipi kwa wazazi wake na hana kitu cha maana. Wakimuuliza utakaa nae wapi? Na usifikiri anafikiria akutambulishe alafu yeye aendelea kukaa kwao. Mambo ni Mengi.. hyo kupanic ni ana msongo wa mawazo na hilo jambo ukimwambia linampasua kichwa..Na vijana wengi wa sasa wakiume. They don’t talk their mind wanataka wafanikishe wao wenyewe..
utampa hela ila hawezi kukwambia inatosha au laah..
ili muda usipotee na una hela fungua biashara muweke.
Kama hamjaoana in a year ahead.
 
Ofcourse kama mmependana wee endelea kumpa tuuu kibubu , PUNYETO NI MBAYA SANA KWA MWANAUME .
 
Unawezaa kukaa na mwanamkeee mia 10 asiwee na kazi na kilaa ktu anakutegemeaa ww ndugu jamaa zake na wazaz wakee unawasaidiaa n km ulimkuta ana mtt ukamsomeshea mwanaee na kumpaa mwayee mahitaji yt ,lkn mwanamkeee akikusaidiaa mwanaumee cku mbilii atatangazaa dunian nzimaa hapo haijalishi mwanaumee unapitiaa kipnd gan ktk uchumi wako,ilaa ndio hvyo tulishaambiwa tuishii nao kwa akili
 
Achaane na huyo jamaa, afanye mambo mengine... sababu jamaa anapenda kitonga hana malengo...
 
Mwambie akae mbali na hujamaa ni mume wa mtu huyo, narudia tena ni mume wa mtu ndio maana anajifanya anakaa home na anakuja kwa mdada kwa kujificha na kujifanya yupo shift ya usiku. Hiyo shift ya usiku ni kumzuga mkewe, mwambie achunguze atapata jibu
 
Ayaaa huyo demu kaingia mikononi Kwa marioo..anategemea ndoa Kwa marioo..ebu nipe namba yake nimshauri,Fanya upesi kabla hajabugi zaidi
 
Wavulana Wana shida Sana....unajua unaweza kuwa na umri mkubwa lkn bado ni mvulana...

Kuna viashiria ambavyo sio vizur kutoka Kwa huyo mvulana.....amekuwa muongo mara kadhaa....na kibaya Zaidi akiambiwa kuhusu ndoa ana panic....kwanini apanic?

Halafu anajisahaulisha kana kwamba hakuna Jambo linaloendelea....sikia hata kama hajajipanga bado Kwa Mda ambao mmekuwa pamoja angekuwa muwazi kuwa mwenzangu usione kimya najipanga Kwanza kuna moja mbili tatu...wanaume ndio wanafanya hivyo...at least anakuweka ktk mazingira Fulani ambayo yanakupa moyo.

Na kama angekuwa seriou walau hata angekutambulisha Tu Kwanza kwao walau ujue unajulikana kwao..

Sikia sitafuni maneno hapo hakuna ndoa kabisa utakuja kusema....nipo pale nasuburia matokeo ya Sensa tujue tupo milioni ngapi now!
 
Back
Top Bottom