GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Nakumbuka wakati Babu wa Loliondo alipoibuka Viongozi wetu wengi sana hasa wa Kisiasa walikuwa wakifunga safari zao kwenda kupata Kikombe cha Babu ambacho inasemekana kuwa kilikuwa kinatibu magonjwa mengi sana ambayo yalikuwa ni magumu kutibika katika Hospitali zetu hapa nchini.
Sasa leo naomba kuuliza hivi hatuwezi tukamuuliza Babu wa Loliondo kuwa wale Viongozi wengi wa Taasisi na Vyama mbalimbali vya Siasa ambao alikuwa akiwapa Vikombe wanywe walikuwa wanaugua nini hasa? Je hakuna labda mmoja wapo ambaye alimzidishia dozi na pengine leo imeanza kumuathiri na hata ameanza kuwa Kero kwa wanaomzunguka?
Mwenye mawasiliano na Babu wa Loliondo atusaidie kwa hili tafadhali ili pengine tuweze kuchukua tahadhari mapema tusije tukadhurika hatimaye kupelekea kushindwa kujenga Tanzania yetu hii nzuri ya Viwanda tunayoitaka na kuitarajia pia.