Je, huu ni uungwana kweli?

nimekumbuka tukio la housegal aliyeua mtoto kwa kumuweka kwenye friji
Ila kwa sababu maovu yake
hayatangazwi siku mfanyakazi akishindwa kuvumilia akaamua kumtanguliza
bosi kwa sumu kila mtu atamuona mbaya!
 

kumbe familia iliyofanya hivyo ni ya kiarabu sishangai hata kidogo wana ubaguzi wa hali ya juu watu wa jamii hiyo
 
Huu ni unyanyasaji mkubwa/ ulipotiliza. Hawa mnaowaita beki tatu wanapitia kadhaa nyingi, manyanyaso mengi, kudharauliwa sana..!! Mkuu Ntuzu umezungumzia sehemu moja kati ya nyingi, na hayo uliyoona yanakupa majibu ya jinsi gani "the-so-called bosses" wanavyowafanyia wasaidizi wao majumbani.

..hawa wasaidizi wanalipwa kiasi kidogo sana, nyumba nyingi wanalipwa at most 50k per month. Itamsadia nini hiyo, akanunulie pedi na chupi tu au? Ni wakati wanaharakati na serikali iangalie Hilo tatizo. Kama huna uwezo wa kulipa kima kinachotajwa na serikali usiajiri mtu, manake HUNA UWEZO!

..unyanyasaji na kufanywa mke wa pili ndani ya nyumba, wababa wengi hawana soni hata chembe, utamvuliaje msaidizi wako wa ndani boxer aone utupu wako? Aibu sana na fedheha.

..Wasaidizi wengi "hula makombo" wakimaliza kula "mabosi" na wao hutenga chakula chao na kula, kama kimeisha wengine hupga desh kabisa.

boss my foot!!
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli sio kitu kizuri lakini nitakachoweza kusema wanasumbuliwa na choyo na ulimbukeni kiasi kwamba anaona binadamu mwenzake hastahili kula anachokula yeye kumbe mwisho wa yote thamani ya chakula mwisho kwenye ulimi kikashavuka ulimi hakina thamani.

Huwa nashindwa kuwaelewa watu wanaomaindi chakula na watu wa namna hiyo hata kama wangewanunulia chakula wasaidizi wao basi nina uhakika baadae wakiwa na wenzao matangazo tele.

Aghhh chakula nini bana!
 
kumbe familia iliyofanya hivyo ni ya kiarabu sishangai hata kidogo wana ubaguzi wa hali ya juu watu wa jamii hiyo


Dada Yangu miss neddy ni Kweli unachosema Lkn kuna familia za ngozi nyeusi km zetu zinanyanyasa wafanyakazi vibaya sn! Tena Yani kuna familia moja ninayoifahamu tena ni watu wenye uwezo mkubwa sn! Ni Ma billionea Lkn ni marufuku mfanyakazi kukaa sebuleni kuangia tv, kula chakula sawa Na anachokula boss wake au kunywa Maji yaliyopo kwenye fridge japo vyote hivyo wao ndio wanaoviandaa! Wao ni kula huko nje Na uwani!
 
Last edited by a moderator:


Mume mwenzangu Eli79 Umesema mambo ya msingi sn Na ninahisi unaweza Kua Na mengi ktk kadhia hii! Ebu endelea kutililika Mkuu ila kwa sharti moja tu, USIMTAJE Karucee wangu!
 
Last edited by a moderator:
Kunakuwa na mengi yaliyopelekea ila hayasemwi tu!!
Kuna mabint wa kazi wanaonyanyaswa sana!


Kweli kabisa Ennie Na kwasababu binti Wa kz basi anakandamizwa tu Na kukosa haki zake!

Jamani tubadilikeni Jamani!

Tuwapende Na kuwathamini Hawa ndugu zetu wanaotutizamia familia zetu Na miji yetu Na thamani zote zilizopo nyumbani Na hasa UHAI WA WATOTO WETU!
 
Last edited by a moderator:
Ni kukemea tu kadri unapoyashuhudia kwa ndugu,jamaa na marafiki.
Tukiwa wema kwao leo watoto wetu watajifunza kwetu nao watakuwa wema kwao kesho.



Ni Kweli kabisa Mkuu!

Mabadiriko ni Mimi kwanza!

Cc: Kaunga FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Mume mwenzangu Eli79 Umesema mambo ya msingi sn Na ninahisi unaweza Kua Na mengi ktk kadhia hii! Ebu endelea kutililika Mkuu ila kwa sharti moja tu, USIMTAJE Karucee wangu!

mhhhhh naomba kuunga undugu na eli kama ni mume mwenzio mi nimwiteje lol
 
Last edited by a moderator:
Huo sio uungwana hata kidogo mkuu

Mambo haya huwa yananiudhi sana na nahisi nikiongea sana naweza haribu mambo!
 
Huo sio uungwana hata kidogo mkuu

Mambo haya huwa yananiudhi sana na nahisi nikiongea sana naweza haribu mambo!



Mkuu Eiyer ongea tu Mkuu! Hapa lengo ni kuelimishana Mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Hizo ni hulka za kichoyo na roho ya kwanini,la hasha si uungwana hata kidogo,hizi tabia chimbuko lake ni majumbani,familia ni muunganiko wa undugu wa damu,jamaa na marafiki,wafanyakaz wa ndani lazima waheshimiwe na kuthaminiwa kama sehemu ya family,kula pamoja,kuvaa na hata kutoka,hujajipanga usitoke na mtu kisha kumnyanyapaa,mfanye mfanyakazi ajione sawa na mwanafamilia hata akiondoka atamani kurudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…