Je, hizi ni mali halali za CCM?

Je, hizi ni mali halali za CCM?

Mr Bean.

Senior Member
Joined
Jan 25, 2015
Posts
185
Reaction score
133
Wadau,

Nimekuwa nikijiuliza mara kadhaa bila kupata majibu sahihi. Ni matumaini yangu humu jamvini wamo wataalam wa mambo mbalimbali.

Ninachotaka kujuzwa ni kuhusu haya maeneo na hasa viwanja vya mpira. Utasikia kiwanja kinaitwa kwa jina la CCM. Vipo viwanja kadhaa hapa nchini na Majumba kadhaa na Maeneo kadhaa ya wazi utasikia pia hata eneo fulani la wazi linaitwa kwa jina la ccm.

Swali langu, Je ni kweli CCM ndiyo walijenga hivyo viwanja vyote tunavyosikia ni mali ya CCM? Je, ni kweli CCM inamiliki kihalali maeneo ya wazi wanayochezea watoto? Je, ni kweli CCM inamiliki kihalali majumba na kumbi za starehe tunazozijua? nk.

Naomba nijibiwe lakini si kiushabiki wa chama tafadhali.
 
Tarehe 26
Vitakuwa Mali Ya Umma Baada Ya Kuingia Chadema
Maana Ccm Imedhurumu Hivyo Vilijengwa Na Wananchi Wote
 
Wakati wa kipindi cha chama komoja, chama ndicho kilikuwa kinashika hatamu za kuongoza Serikali 'party supremacy', kujiunga na CCM ilikuwa ni lazima na sio hiyari, na kuichangia CCM ilikuwa ni lazima sio hiyari!.

Wafanyakazi wrote walikatwa michango ya chama straight toka kwenye mishahara yao kama wanavyokatwa kodi, PAYE na michango ya pensions funds!.

Kipindi hicho CCM ndio ilikuwa kila kitu ikajitwalia kila ilichotaka vikiwemo viwanja, majengo, mashule, na maeneo ya wazi!.

Mwaka 1992 tulivyoanza vyama vingi, ilibidi CCM I surrender Mali zake zote ilizochuma wakati wa chama komoja, then vyama vyote vianze moja from the scratch!.

Hili halikufanyika hivyo CCM imeloot Mali ya Watanzania na Mali nyingine zote ikizoendelea kuchuma baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza, zimetokana na multiplied effect ya zile loot!.

Kazi ya kwanza kabisa baada ya Serikali ya Lowassa kuingia madarakani ni kuipurura CCM Mali zote ilizopora na kuzigeuza Mali za umma!.

Ila ili kuitebdea haki, Serikali Mpya itawajibika kumleta mtaalamu wa actuarial valuation kufanya tathmini ya Mali halali za TANU zilizotokana na michango ya halali ya hiyari vikiwemo lile jengo LA CCM Lumumba ni mali halali ya TANU!.

CCM ikiisha pururwa itakuwa reduced to nothing!.

Tulipobibafshisha sekta ya mabenki, tulishauriwa kuwa ili mabenki yaweze kuanzishwa, kwanza tulivunje lile li benki letu likubwa li NBC ili kujenga mazingira ya ushindani wa haki, NBC ikavunja!.

Hivyo tulipoanza vyama vingi ilibidi li CCM livunjwe kwanza ili kuleta ushindani wa haki!.

Pasco
 
Pasco nakubaliana nawewe kuhusu umiliki wa awali wa majengo viwanja NA miradi mingine ya ccm.Ni kweli wote tulikua huko wengine wakajiondoa huko wakaanzisha vyama vyao .kumbuka wengi waliondoka kwa utashi wao.Lakini kwa wema NA uzuri wa ccm rudini ili tuweze kumiliki mali hizo wote.KAMA pia hutaki nafikri ni vizuri WATU wakaenda mahakamani kuonyesha walichangia kiasi gani NA kwa makubaliano gani ili wapewe haki yao.MIMI NATAKA KUOWA NAOGOPA UKINICHANGIA TUKIKOSANA UNAWEZA KUDAI KISA ULINICHANGI HAHAAA!!!TUNAWAKARIBISHA WOTE WALIOCHANGIA NA WASIOCHANGIA TUNAWAPOKEENI WOTE
 
Last edited by a moderator:
hata chadema wakiacha kukodi jengo la ofisi na wakijenga litakuwa lao
 
Ata pale magogoni ni Mali ya CCM pia so kama kweli ukawa wanataka kwenda ikulu basi wajenge ikulu yao kwanza.
#Hapa kazi tu buana.
 
Itabidi wadaiwe na fidia, wakishindwa kulipa mali zao halali zipigwe MNADA ili liwe fundisho kali kwa kizazi cha sasa na kijacho. AMINA!
 
Wadau,

Nimekuwa nikijiuliza mara kadhaa bila kupata majibu sahihi. Ni matumaini yangu humu jamvini wamo wataalam wa mambo mbalimbali.

Ninachotaka kujuzwa ni kuhusu haya maeneo na hasa viwanja vya mpira. Utasikia kiwanja kinaitwa kwa jina la CCM. Vipo viwanja kadhaa hapa nchini na Majumba kadhaa na Maeneo kadhaa ya wazi utasikia pia hata eneo fulani la wazi linaitwa kwa jina la ccm.

Swali langu, Je ni kweli CCM ndiyo walijenga hivyo viwanja vyote tunavyosikia ni mali yan



Ni kweli,,,,,,swali jingine?
 
ni sawa na leo mtu aanze kuhoji kama kanisa catolic yale maeneo wanamiliki kweli kihalali ama walikatiwa tu...

ukweli ni kuwa ccm ama catolic waliona mbali na na kukamata maeneo kipindi kile yakiwa na bei cheap,kama shs 150 kwa heka na wakapata title zake.

sasa leo kibushuti tu kazaliwa miaka ya 90 eti anahoji uhalali wa mali za ccm
 
ni sawa na leo mtu aanze kuhoji kama kanisa catolic yale maeneo wanamiliki kweli kihalali ama walikatiwa tu...

ukweli ni kuwa ccm ama catolic waliona mbali na na kukamata maeneo kipindi kile yakiwa na bei cheap,kama shs 150 kwa heka na wakapata title zake.

sasa leo kibushuti tu kazaliwa miaka ya 90 eti anahoji uhalali wa mali za ccm

Hivi umeelewa kilichoandikwa kweli?
 
Mali yote wanayotamba nayo CCM vyote ni Mali ya watanzania wote. Ikitokea Chama pinzani kitwaa madaraka Mali zote zitakuwa maliya wote kwani zilipatikana kipindi cha mfumo wa Chama kimoja... Na huwezi compare na Mali za jumuiya za kidin
 
Sina hamu na CCM kwa mambo mengii ... ESCROW, EPA, UJANGILI, SEMBE, RICHMOND, MIKATABA YA KIFISADI, KUKWAPULIWA KWA MADINI YETU, GAS ... MAISHA MAGUMU, KODI KUBWA KWENYE MSHAHARA, MISHAHARA DUNI ISIYOKIDHI GHARAMA ZA MAISHA n so much more ...
 
Wapinzani watazisaidia Halmashauri kumiliki mali kama viwanja na mapato yataongezeka.
 
hata chadema wakiacha kukodi jengo la ofisi na wakijenga litakuwa lao
Yes litakuwa Lao kwasababu litakuwa limejengwa na chama. Kumbuka umeshaambiwa kwa sasa tupo kwenye vyama vingi. Hata kwa ccm miradi wanayofanya sasaivi lkn iwe kihalali zisiwe pesa za kuchukua kutoka serikalini kifisadi
 
mimi najiuliza swali moja tu,hivi ukifanyika uchunguzi wa kina ule ukumbi mpya kule dodoma hakuna hela ya serikali iliyoingia pale????
 
Ni vema kuzungumza ukweli hapa badala ya kudanganyana kama wajinga fulani....! Jambo la kutaifisha mali za chama si jambo rahisi kama wengine wanavyodhani....! Ila ni vema kabla ya yote, pengine ni vema tukaangalia mambo yafuatayo;
  1. Sheria ya vyama vingi vya siasa Tanzania, hasa iliyoruhusu mfumo huu rasmi mwaka 1992 kuwa imeelezaje kuhusu swala hili....!
  2. Kila aliyekuwa mwanachama wa CCM wakati huo arejee mkataba wake na chama wakati anajiunga...!
Kanuni hizi zitakueleza ni nini unaweza kufanya katika hilo...! Aidha, tunawahitaji watu kama Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila, mwenye ujasiri wa kwenda mahakamani mwenyewe kwa manufaa ya umma....! Labda kama CCM ingebadilisha jina mwaka 1992, basi tungesema CCM ilikufa na mrithi wake ni umma, vinginevyo bado iko hai....!
Ni vema tukafikiria na kujadili yanayowezekana, na kuachana na yasiyowezekana kabisa....! Ila siwakatishi tamaa, bali mie naona ndio hivyo...!
 
Back
Top Bottom