Ndio mkuu cha muhimu tafuta desktop ambayo ina power supply ya kawaida na sio hizi dell na Hp zenye power supply ambazo ni ngumu ku upgrade.
Kwa around laki 5 unaweza tengeneza gaming machine kali, na around laki 3 na nusu mpaka 4 unaweza tengeneza gaming machine decent.
-Gaming machine kali,
1. Nenda aggrey ama machimbo ya pc yoyote katafute processor ya i7, unazipata around 30,000 mpaka 80,000 inategemea na generation, nilinunua i7 4790 kwa 80,000 na niliona pia i7 1st gen kwa hio 30k sema hazina maana.
2. Tafuta desktop ya celeron ama pentium ya gen husika, mfano umepata hio i7 4790k hio ni gen ya 4, tafuta desktop ya gen ya 4 pentium, unazipata chini ya 150k, kwangu nilinunua 130k bila HDD.
3. Toa pentium, weka i7, upgrade storage na ram, mimi nilitumia 80,000 kuweka ssd na around 60,000 kwa 8gb ram hivyo total inakuja kama 350,000 kwa machine ya i7 4790, 12gb ram na ssd 128/256gb.
4. Nunua GPU aliexpress ama popote unapoona rahisi, chini ya 150k unapata used.
-gaming machine ya kawaida
1. Nunua desktop ya i5 around 250k mpaka 400k kutegemea na gen
2. Upgrade gpu.
Ila suala la power supply kuwa makini sana mkuu, hizo zisizofaa zinakuwa na pin 8 na zile nzuri zinakuwa na pin around 20 hivi.
Unaweza kuziangalia zote hapa
All about the various PC power supply cables and connectors