Je, hizi ndio tabia za wanawake?

Je, hizi ndio tabia za wanawake?

oa mwanamke upweke mbaya sana hao watoto ni wakubwa. utaepuka magonjwa coz najua mpaka sasa kuna sehemu unapeleka genye zako. uongo?
 
Pole ndugu kwa yaliyokufika. Usiache kumuomba Mungu azidi kukusaidia kwenye malezi ya hao watoto.
Ni kweli wanawake wanapenda sana maneno ya kuambiwa.
Ningependa wanawake mmbadilike katika hili. Mnaharibu familia na males I kwa maneno ya kipuuzi.
 
Watu hawafanani! Tafuta mke uoe, mweleze ukweli kuhusu familia yako, naamini utapata mke mwema . Hao watoto uwe nao karibu ili hata ikitokea shida wakueleze.
 
Mkuu Moja Ya Sababu Za Ndoa Kuvunjika Chini Ya Kifungu 107(2) Ya Sheria Ya Ndoa Ya Mwaka 1971 Ni Kutelekeza (Wilful Neglect Au Desertion).
She Deserted You.Miaka Miwili Imepita Since Amekukimbia. Apo Nenda Conciliation Board Ataitwa Akiitwa Mkishindwana Bodi Wanakupa Certificate Kua Ndoa Imeshindikana Na Wameshindwa Kutatua Mgogoro. Baada Ya Hapo Tunaapply For Divorce Very Easily. I Wish I Was A Real Advocate. But Am On My Way.

All The Best Mkuu.
 
Miaka 8 bado unamfikiria tu? Yani huyu hata akirudi hatokuwa kama alivyokuwa mwanzo.
 
Wakuu

Leo ni miaka nane imetimia toka niachwe na mke wangu, nasema ni mke wangu kwa sababu hakuna talaka yoyote tuliyopeana kisheria kuivunja ndoa yetu na kwa muda wote huo nimekuwa nikimbembeleza sana ili arudi tulee familia imeshindikana.

Sababu za kuniacha hazikuwa na msingi wowote, kwani alidai kuwa aliambiwa na rafiki zake kuwa nina uhusiano na dada mmoja, hivyo akaamua kuchukua uamuzi huo. Ukweli ni kuwa huyo ambaye nilituhumiwa kuwa na mahusiano naye wala nilikuwa simfahamu, nikamwambia alete ushahidi, ilishindikana zaidi ya maneno tu kuwa aliambiwa.

Nilijaribu kuwaomba wazee wamsihi na vikao vya ukoo vilifanyika lakini ilishindikana, juhudi zangu zote ziligonga ukuta, na hivyo kuwalazimu ndugu waniambie kama naweza kupata mwanamke mwingine, nioe.

Kwa muda wote huo nimeishi peke yangu nikiwa na wanangu, namshukuru Mungu kwa sasa wameshakua. Mmoja alimuacha akiwa na miaka 6 na sasa ana miaka 14 na mwingine alimuacha akiwa na miaka 3 na sasa ana miaka 11.

Huyo mke wangu, sasa yapata miaka sita imepita sijamtia machoni pangu, ila nasikia tu yupo mkoa fulani.

Wanajamii, nimeshindwa kuoa mwanamke mwingine kila nikifikiria mateso ambayo wanaweza kupata wanangu kutoka kwa mwanamke mwingine. Kila nikifikiria tu manyanyaso ambayo wanapata watoto wengine ambao wanalelewa na mama tofauti akili yangu inapoteza network kiasi kwamba hata sitamani kuoa tena.

Najiuliza, pengine hizo ndo tabia za wanawake wote au ni baadhi tu ambao kwao upendo umewapita mbali.

Naombeni ushauri waungwana!
sio tabia za wanawake wte. pole sna ndugu ila ungejaribu tena kumsihi arudi mlee familia. huenda this time atakuelewa.
 
Pole ndugu kwa yaliyokufika. Usiache kumuomba Mungu azidi kukusaidia kwenye malezi ya hao watoto.
Ni kweli wanawake wanapenda sana maneno ya kuambiwa.
Ningependa wanawake mmbadilike katika hili. Mnaharibu familia na males I kwa maneno ya kipuuzi.
Nashukuru mkuu kwa ushauri mzuri
 
sio tabia za wanawake wte. pole sna ndugu ila ungejaribu tena kumsihi arudi mlee familia. huenda this time atakuelewa.
Nimejaribu kila mbinu ya kumfanya arudi, imeshindikana na ndo maana nimeamua kuleta huu uzi humu jukwaani ili nipate msaada wa ushauri
 
Miaka 8 bado unamfikiria tu? Yani huyu hata akirudi hatokuwa kama alivyokuwa mwanzo.
Nimemsubiria muda wote huo nikijua kwamba pengine anaweza badilika, na isitoshe kama ningeoa, basi kile ambacho alikuwa anaambiwa angeamini
 
Mkuu Moja Ya Sababu Za Ndoa Kuvunjika Chini Ya Kifungu 107(2) Ya Sheria Ya Ndoa Ya Mwaka 1971 Ni Kutelekeza (Wilful Neglect Au Desertion).
She Deserted You.Miaka Miwili Imepita Since Amekukimbia. Apo Nenda Conciliation Board Ataitwa Akiitwa Mkishindwana Bodi Wanakupa Certificate Kua Ndoa Imeshindikana Na Wameshindwa Kutatua Mgogoro. Baada Ya Hapo Tunaapply For Divorce Very Easily. I Wish I Was A Real Advocate. But Am On My Way.

All The Best Mkuu.
Thanks mkuu kwa ushauri mzuri
 
Watu hawafanani! Tafuta mke uoe, mweleze ukweli kuhusu familia yako, naamini utapata mke mwema . Hao watoto uwe nao karibu ili hata ikitokea shida wakueleze.
Lakini mkuu, nitajuaje kama huyo ambaye nitaoa ataweza kuwacare vizuri wanangu? Isije ikawa naoa, matatizo ndo akashindwa kuwacare kabisa hao wana,
 
Mi sikushauri uoe kama umeweza kuwalea toka wadogo haina haja ya kuwatafutia mama mwingine. Wanawake sie bana huwa ni kama tunakumbwa na mapepo katika malezi ya watoto wakambo.
 
*WOGA ukiwa mwingi hata BAHATI zako utaziogopa.
*MAWAZO ukiyapa nafasi hata pasipo TATIZO wewe utaona TATIZO TU
*Inabidi uoe tu mkuu mateso hakuna kitakachotokea watoto ni wa kubwa tayari miaka 14 ameshabaleghe na 11 ufahamu ni mkubwa (mateso mengi ni chini ya miaka10)
 
Kingine cha kujifunza sasa hivi mwanamke akisema NO basi hata uje ukoo mzima, familia na viongozi wa dini ataendelea na msimamo wake.
*wabishi sana
*hawaelewi kitu zaidi ya msimamo
*hawarudii matapishi
*endapo atakusamehe/ kusulihishwa na wazee basi atakuja kukulipizia kisasi.
 
Kaka me cjaoa ila kutokana na hali kama hyo haina haja ya kurisk kutafut mwanamk mwingin aje akulelee wanao, Sawa sikatai kwamb sio wanawak wote ndo wenatabia hizo ila tatizo linakuja Nani ndiye Nani siye sasa huon kwamb hyo ni risk. Nimewaza sana umemkuza mtoto toka miak 3 had 11, bila mama aje akushinde 11 kuendelea mtu ameshakua kabic, sikushaur bro lea wanao haina haja ya kucheza Kamar kutafut limwanamke lingine. Bora wangekua na alama kwamb huyu n mzur huyu ni mbaya. Komaa lea wanao wala hutobadilika chocht kile na mungu akutie nguvu na ujacri katika hilo. One day utajivunia juu ya hilo
Duuu! Nashukuru mkuu!
 
Kingine cha kujifunza sasa hivi mwanamke akisema NO basi hata uje ukoo mzima, familia na viongozi wa dini ataendelea na msimamo wake.
*wabishi sana
*hawaelewi kitu zaidi ya msimamo
*hawarudii matapishi
*endapo atakusamehe/ kusulihishwa na wazee basi atakuja kukulipizia kisasi.
Ok, thanks
 
Back
Top Bottom