kwetumasoko
JF-Expert Member
- Aug 24, 2016
- 866
- 517
Wakuu
Leo ni miaka nane imetimia toka niachwe na mke wangu, nasema ni mke wangu kwa sababu hakuna talaka yoyote tuliyopeana kisheria kuivunja ndoa yetu na kwa muda wote huo nimekuwa nikimbembeleza sana ili arudi tulee familia imeshindikana.
Sababu za kuniacha hazikuwa na msingi wowote, kwani alidai kuwa aliambiwa na rafiki zake kuwa nina uhusiano na dada mmoja, hivyo akaamua kuchukua uamuzi huo. Ukweli ni kuwa huyo ambaye nilituhumiwa kuwa na mahusiano naye wala nilikuwa simfahamu, nikamwambia alete ushahidi, ilishindikana zaidi ya maneno tu kuwa aliambiwa.
Nilijaribu kuwaomba wazee wamsihi na vikao vya ukoo vilifanyika lakini ilishindikana, juhudi zangu zote ziligonga ukuta, na hivyo kuwalazimu ndugu waniambie kama naweza kupata mwanamke mwingine, nioe.
Kwa muda wote huo nimeishi peke yangu nikiwa na wanangu, namshukuru Mungu kwa sasa wameshakua. Mmoja alimuacha akiwa na miaka 6 na sasa ana miaka 14 na mwingine alimuacha akiwa na miaka 3 na sasa ana miaka 11.
Huyo mke wangu, sasa yapata miaka sita imepita sijamtia machoni pangu, ila nasikia tu yupo mkoa fulani.
Wanajamii, nimeshindwa kuoa mwanamke mwingine kila nikifikiria mateso ambayo wanaweza kupata wanangu kutoka kwa mwanamke mwingine. Kila nikifikiria tu manyanyaso ambayo wanapata watoto wengine ambao wanalelewa na mama tofauti akili yangu inapoteza network kiasi kwamba hata sitamani kuoa tena.
Najiuliza, pengine hizo ndo tabia za wanawake wote au ni baadhi tu ambao kwao upendo umewapita mbali.
Naombeni ushauri waungwana!