Je Hili ni sahihi au mie ndio sielewi

Je Hili ni sahihi au mie ndio sielewi

Joined
Jan 9, 2013
Posts
39
Reaction score
30
habari zenu wanajamvini
naomba kufahamu mambo mawili matatu hivi unapokuwa na rafiki wa kiume wote mnafanya kazi ila asilimia kubwa mnapotoka outing hata akikuona unalipia bili mlizotumia haoneshi kustuka anaona ni sawa tu , ndani ya mahusiano yasiozidi mwaka ameshaanza kukukopa hela akiomba mkopo mdogo milioni kabla hajarudisha ya kwanza anataka umkope na nyingine kwa ahadi atakurudishia zote ,na kama hiyo haitoshi most of the time anakuja nyumbani kwako kukusalimia ila atakula na kunywa ila hujawahi msikia akikuambia chukua hii hapa hela ununue mboga ila akivikuta anakula,gari anatumia yako mfano mafuta akiweka anahakikisha siku anakurudishia taa ya mafuta inawaka yaani kalijaze mwenyewe,mbaya zaidi hupafahamu anapokaa ila yye kazi yake kuja kwako na hata haoneshi msisitizo upajue nyumbani kwake ,
mbaya zaidi anakuambia anataka muoane hivi mtu akija kukuomba ushauri kwa hayo matatizo hapo juu ungemshaurije ??
 
ningemshauri yeye akajitambue kwanza halafu ndio aje nimshauri! tofautisha rafiki na kufahamiana, mm sioni km hapo kuna urafiki wa malengo, ila its just a bunch of a company!
 
si unaachana nae maana huyo is using you,na mkioana majukum yote
atakuachia wewe........,
the brain should lead you not the heart,cos as it is ryt now it will lead you to nowhere

hivi inakuaje from no where unamwazima mtu milion akikukana utafanyaje?
na wanaume wenye vitabia hivyo wamekuwa weng sana hapo mjini
 
habari zenu wanajamvini
naomba kufahamu mambo mawili matatu hivi unapokuwa na rafiki wa kiume wote mnafanya kazi ila asilimia kubwa mnapotoka outing hata akikuona unalipia bili mlizotumia haoneshi kustuka anaona ni sawa tu , ndani ya mahusiano yasiozidi mwaka ameshaanza kukukopa hela akiomba mkopo mdogo milioni kabla hajarudisha ya kwanza anataka umkope na nyingine kwa ahadi atakurudishia zote ,na kama hiyo haitoshi most of the time anakuja nyumbani kwako kukusalimia ila atakula na kunywa ila hujawahi msikia akikuambia chukua hii hapa hela ununue mboga ila akivikuta anakula,gari anatumia yako mfano mafuta akiweka anahakikisha siku anakurudishia taa ya mafuta inawaka yaani kalijaze mwenyewe,mbaya zaidi hupafahamu anapokaa ila yye kazi yake kuja kwako na hata haoneshi msisitizo upajue nyumbani kwake ,
mbaya zaidi anakuambia anataka muoane hivi mtu akija kukuomba ushauri kwa hayo matatizo hapo juu ungemshaurije ??
siku akitokomea usipopajua na hilo gari sijui utamtafutia kona ipi ya nchi
 
Kuwa makini kuna mmoja binti kama wewe juzi kawekewa dawa kwenye kinywaji watu wakaondoka na pete,mikufu, ATM Card, Kipochi, Simu nk Huyu aliyemuibia alijifanya anataka kuwa nae kimapenzi ---- tapeli.Usipoangalia kuna siku atarudi analia atakwambia kwamba gari imeibiwa. Kaa macho binti mji umeharibika sana.
 
Hivi ujue unatumalizia wino wa vibodi zetu wewe kwa kutufanya tujaze miushauri hapa wakati kwa uwazi kabisa unaona umelamba garasa...
Hivi kweli jamani huoni hapo kama umekutana na poyoyo ila umeamua tu kumuita mpenzi.
Mwanamke shtuka basi na uanze kufikiria kwa kutumia ubongo badala ya moyo...wewe kutwa kutoa tu sijui ukiombwa na kabang nayo utatoa!!!
 
Kweli umekutana na poyoyo sijui kwa nini siku hizi wamekuwa wengi mno jitu linajiachia kabisa mkitoka mfuko wako ndio unahusika yeye hata hashituki halafu kwa kukopa eti bby niazime laki, mara laki 2 na wala hatakaa akurudishie na kama ni gari yake basi ujue ukirudishwa kwako wewe ndio wa kuweka mafuta hovyo kabisa marioo tupa kule!
 
hili ni garasa ambalo umekula... mijamaa kama hii ipo kibao siku hizi ambayo inataka mitelemko... hawa wanaitwa "marioo" hebu jielewe mwanamke! nahili unataka sisi wanaume wenye akili zetu tukuweze? kama ni Hivyo subiri huyo kicheche akuwezeshe ipasavyo!
 
Hivi mtu hata kwake hupajui unamuamini hadi kumpa gari yako atembelee! Lol
 
Kila mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake! mjini hapa ohoooo
 
Mmmh.... Hebu fumbua macho dada!

Huyo jamaa anataka kuchuma kupitia jasho lako, na hayo mamilioni uliyokopwa sijui utayadai vipi..!
 
Tena kibaya zaidi mijanaume kama hiyo huwa ni wahuni wa kutupwa leo yuko na wewe, kesho mie, kesho kutwa sijui nani kotekote anapiga miziga kwa mtaji wa kifanyio chake ..... wahusika hebu mjielewe na kijitambua basi khaa!
 
Hawa vijana wa design hii sasa wapo wengi sana.
Utakuta kijana anakupigia sim, wewe unakuwa humjui. ukimuuliza number katoa wapi, anasema wewe mwenyewe ndio ulimpa. most of the time atakutajia maeneo kama mlimani city ndio mlikutana ukampa number(huku akijua kwamba wakazi wengi wa DSM ufika maeneo hayo) Anakung'ang'ania kuwa number ulimpa mwenyewe. Sasa kwa wadada ambao wanajijua hawana tabia ya kutoa number kwa strangers hapo imekula kwa kijana)
ukimuuliza kijana shida yako nini, utasikia ooh tufahamiane etc etc, au mbona una haraka dada. yaani ujinga mtupu. so basically huyo kijana anakuwa amekufuatilia nyendo zako for sometime na kupata contacts zako kwa njia anazofahamu yeye, na most of the time anakuwa amejua kwamba wewe ni dada mwenye pesa zako.
 
dalili ya mvua ni mawingu, unaweza ukamsomeshea hata kijiji chake chote!!! chezea vidume wewe...
 
Naomba nikueleze ukweli, hizo hela unazomkopesha anaenda kumpa demu wake mwingine, hata hilo gari huwa antumia kujirusha naye. Pole sana, uamuzi ni wako kuendelea kuhudumia watu wawili au...
 
kwani lazima kuwa na mwanaume?
usipokuwa nae utakufa au? aya sasa wakiitwa wenye wapenzi na wewe unatoka?
 
shusha hasira ndugu...post zingine mods waweke alert aisee ili tujue jinsi ya kuzisoma

Back
Top Bottom