Je, hili ni kweli na linawezekana?

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Je, mahakama inao uwezo wa kubadilisha sheria bila kupitia tena bungeni? Kutokana na maelezo ya Mh Marmo, naomba wataalamu wa sheria watusaidie.


*************************************

Serikali yaitupia mahakama mgombea binafsi

na Sauli Giliard na Mariam Maregesi


SERIKALI imesema hatima ya mgombea binafsi kushiriki katika chaguzi mbalimbali nchini iko mikononi mwa Mahakama ya Rufaa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo alisema hayo jana wakati wa kukusanya maoni ya wadau juu ya sheria za uchaguzi katika zoezi linalosimamiwa na Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge.
Akijibu hoja zilizotolewa na mwakilishi wa Chama cha Wananchi (CUF), Joram Bashange juu ya kuruhusiwa kwa mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu, kiongozi huyo alisema suala hilo liko kimchakato zaidi.
Marmo akitoa ufafanuzi wake kwa wanahabari nje ya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, alisema tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amekwishaagiza mahakama iangalie kama ina uwezo wa kuibadilisha sheria inayotaka wabunge kuwa ndani ya chama.
“Tatizo hatuwezi kuiga wengine. India na Ujerumani kwao hawataki kabisa suala hili, inategemea na mazingitra ya kwao yako vipi, lakini mwanasheria mkuu amekwishaiambia mahakama kama ina uwezo wa kubadilisha sheria hiyo,” alisema Marmo.
Katika hatua nyingine, mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Laetitia Petro alisema katika marekebisho ya sheria hizo, suala la mgombea wa chama fulani kupita bila kupingwa ni kuwakosesha wananchi haki zao.
Mwanasheria huyo alisema ni bora uchaguzi ukahairishwa hata kama serikali itaingia gharama ili kuepuka kumpata mgombea ambaye watu hawamtaki.

Source: Tanzania Daima (http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=12326)
 
Back
Top Bottom