Tunguja
JF-Expert Member
- Feb 15, 2018
- 450
- 327
Dada yangu katimuliwa na mumewe,dada yangu ameolewa kwenye ndoa ya wake wawili na yeye ni mke mdogo,bahati mbaya sana mke mkubwa hajajaaliwa kupata uzazi,Ila dada yangu ana watoto wanne.
Sababu ya yeye kutimuliwa kwa mujibu wa maelezo ya shemeji ni kwamba ada yangu amekuwa akimwambia mwanaye mkubwa (15yrs) kwamba yeye ndio mrithi wa mali zote za baba yake kwasababu mke mkubwa hana watoto, kwa maelezo yake shemeji ni kwamba alishawahi kumuonya mkewe mara kadhaa kwamba anachokifanya sio sahihi kabisa, kwasababu
1: Watoto watabweteka wakitegemea mali za baba yao.
2: Hajui bibi mkubwa anawaza nini anaposikia hizo kauli, Inawezekana anaweza akafanya vitu ambavyo vinaweza kuwaletea madhara watoto ili wakose wote
3: Anahisi mkewe anamwombea kifo ili yeye na wanawe warithi mali zake
Anadai kwamba baada ya kuona hiyo tabia haikomi kaamua amtimue kabla madhara makubwa ambayo yeye anahisi yanaweza kutokea hayajatokea,kamwachia nyumba pia kampa mtaji milioni thelathini ili ,kamwambia alichopewa ndio urithi wa watoto yeye asimamie ikitokea akifa vitakavyokuwepo vyote ni vya mke mkubwa, najua ,je nani mwenye kosa kati yao?