Je, hili la TANESCO siyo "utapeli"?

Je, hili la TANESCO siyo "utapeli"?

Gharama kubwa kabisa ya kulipia ili kupata umeme was TANESCO ni 1,500,000TZS Iweje utoe pesa kubwa hiyo milioni 15?
Na Transformer pia? kuna added cost hapo kwenye kesi ya huyu ndugu
 
Jamani hivi huyu mtumbua majipu hajui maovu ya TANESCO?Mi nafikiri angeanzia hapo kwenye nguzo,maana kusimikiwa nguzo moja tu ni MSALA!
 
[HASHTAG]#Mda[/HASHTAG] Mwingine Unapotaka Huduma Flani za Kijamii Unatakiwa Upunguze Kiherehere sawa Unashida ya Umeme Kwani Ukisubiri Rea Wapite Unaumia Wapi Kwa Jinsi Ulivyo Utaenda Dawasco Ulipie Maji Kwa Mil10 Mambo mengine Unajitakia Mwenyewe Na Utakuwa Wa Mwisho kabisa Alafu watakwambia Tunakuunga Single Phase2
Wewe wa wapi mkuu, Hiyo Rea haiko kila mahali. Suala la kusubiri ndio yaleyale kwamba hili shirika ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. unadhani kila mtu angesema asubiri ingekuwaje? Jukumu la kusambaza miundo mbinu ni la shirika husika.
 
Ndugu wadau,

Kuna jambo linanitatiza katika mpangilio wa ufanyaji biashara wa hili shirika la umeme TANESCO. Mimi nahitaji kuunganishiwa umeme katika nyumba yangu umeme ambao nitakuwa naulipia kwa kadiri ya matumizi yangu. Lakini ninakerwa na huu utaratibu wa malipo ya vifaa vya kuunganishiwa umeme.

Kwa mfano natakiwa nilipie nguzo kadhaa, waya mita kadhaa, Transformer, na kadhalika jumla ya ngarama naambia ni Tshs Mil. 15, eti kwa ajili ya kuweka miundombinu ya kufikisha umeme ndani ya nyumba yangu. Lakini cha kushangaza baada ya kulipia vifaa hivi kwa Mil 15, vifaa husika vinageuzwa kuwa mali ya TANESCO Bila mimi muhusika kufahamishwa au kuombwa na Shirika hili.

Kupitia miundo mbinu hii niliyo nunua kwa pesa zangu za kudunduliza na mikopo, utaona TANESCO wakianza kuunganishia umeme watu wengine jirani yangu kwa bei nafuu bila kuulizwa au kuombwa na wahusika. Je hii ni haki? Shirika kujinufaisha kupitia mpango huu! Au kwa kuwa ni Shirika la Serikali linafanya litakavyo?

Je kujenga miundombinu ya umeme ni kazi ya mlaji au ni kazi ya msambazaji?
Sasa mkuu,umeme utakaondelea kuja kwako kupitia hivyo vifaa ulivyolipia unabakia kuwa wa Tanesco,sasa hivyo vifaa kama nguzo,waya,mita na hilo transformer hata wakiamua kukuachia ulitaka ufanye navyo nini??
 
Ndugu wadau,

Kuna jambo linanitatiza katika mpangilio wa ufanyaji biashara wa hili shirika la umeme TANESCO. Mimi nahitaji kuunganishiwa umeme katika nyumba yangu umeme ambao nitakuwa naulipia kwa kadiri ya matumizi yangu. Lakini ninakerwa na huu utaratibu wa malipo ya vifaa vya kuunganishiwa umeme.

Kwa mfano natakiwa nilipie nguzo kadhaa, waya mita kadhaa, Transformer, na kadhalika jumla ya ngarama naambia ni Tshs Mil. 15, eti kwa ajili ya kuweka miundombinu ya kufikisha umeme ndani ya nyumba yangu. Lakini cha kushangaza baada ya kulipia vifaa hivi kwa Mil 15, vifaa husika vinageuzwa kuwa mali ya TANESCO Bila mimi muhusika kufahamishwa au kuombwa na Shirika hili.

Kupitia miundo mbinu hii niliyo nunua kwa pesa zangu za kudunduliza na mikopo, utaona TANESCO wakianza kuunganishia umeme watu wengine jirani yangu kwa bei nafuu bila kuulizwa au kuombwa na wahusika. Je hii ni haki? Shirika kujinufaisha kupitia mpango huu! Au kwa kuwa ni Shirika la Serikali linafanya litakavyo?

Je kujenga miundombinu ya umeme ni kazi ya mlaji au ni kazi ya msambazaji?
Ila kwa gharama iyo mkuu utakuwa unakiwanda ama
 
Mkuu insu sio utaratibu\sheria kuwepo au kutokuwepo, mleta mada anaona utaratibu huu ni aina ya utapeli, wewe unaona ni sawa kugharamia miundombinu ya mtu mwingine na wengine waje watumie kwa gharama zako? Mi binafsi sipingi tanesco kutaifisha miundombinu ya umeme iliogharamiwa na mtu, (kwa maslai ya nchi) lakini kwa nn wasimfidie kwenye units za umeme mpaka deni lake litapoisha? Mi naona sio utapeli tu, huu ni wizi kabisa!
Subiri nguzo zote zioze ni huyo huyo atakaenda kuomba zibadilishwe na atabadilishiwa bila hata kulipa 100.
 
Ndugu wadau,

Kuna jambo linanitatiza katika mpangilio wa ufanyaji biashara wa hili shirika la umeme TANESCO. Mimi nahitaji kuunganishiwa umeme katika nyumba yangu umeme ambao nitakuwa naulipia kwa kadiri ya matumizi yangu. Lakini ninakerwa na huu utaratibu wa malipo ya vifaa vya kuunganishiwa umeme.

Kwa mfano natakiwa nilipie nguzo kadhaa, waya mita kadhaa, Transformer, na kadhalika jumla ya ngarama naambia ni Tshs Mil. 15, eti kwa ajili ya kuweka miundombinu ya kufikisha umeme ndani ya nyumba yangu. Lakini cha kushangaza baada ya kulipia vifaa hivi kwa Mil 15, vifaa husika vinageuzwa kuwa mali ya TANESCO Bila mimi muhusika kufahamishwa au kuombwa na Shirika hili.

Kupitia miundo mbinu hii niliyo nunua kwa pesa zangu za kudunduliza na mikopo, utaona TANESCO wakianza kuunganishia umeme watu wengine jirani yangu kwa bei nafuu bila kuulizwa au kuombwa na wahusika. Je hii ni haki? Shirika kujinufaisha kupitia mpango huu! Au kwa kuwa ni Shirika la Serikali linafanya litakavyo?

Je kujenga miundombinu ya umeme ni kazi ya mlaji au ni kazi ya msambazaji?
Ndugu Hashm! Tanzania yetu hii ni nchi kubwa yenye takribani kilomita za mraba laki 9 na nusu ambazo ni ngumu kwa tanesco kusambaza miundombinu ya umeme katika eneo lote hili kwa wakati mmoja na pia kama inavyoeleweka hili ni shirika la kibiashara hivyo moja kwa moja lilianza kusambaza umeme katika maeneo yenye makazi/wateja wengi tayari na kufuatia na makazi mapya yenye uwezekano wa kuwa na wateja wengi zaidi katika kupindi kifupi baada ya huduma kupelekwa ama maeneo yanayopigiwa chapuo na serikali ama kikundi fulani cha watu kwa sababu za kimkakati kama vile Maeneo ya viwanda, EPZ, makazi maalumu n.k hivyo shirika kupanga bajeti zake na plan zake za mwaka mzima kwa kuangalia vipaumbele hivyo lakini kwa kuwa Tanesco ni shirika la kibiashara linaloongozwa serikali kwa maana ya kuhudumia wananchi wote bila kujali umbali wa maeneo yao kutoka ilipoishia mifumo ya usambazaji umeme, basi kwa watu walioko mbali zilipoishia line hawakatazwi kuungalisha umeme na hupewa machaguo kadhaa ikiwemo kusubiri eneo husika lipangiwe bajeti kama limekidhi vigezo kwa maana ya idadi ya wateja bajeti ikipita umeme utafika eneo husika pia kama mteja atakuwa na haraka sana ama eneo lake limejitenga na makazi mengine ambapo uwezekano wa kupelekewa huduma na shirika kutokana na garama zisizoakisi faida itakayopatikana kutokana na matumizi madogo ya mteja husika, mteja huyo huruhusiwa kulipia garama za uvutaji umeme mpaka ilipo nyumba yake kwa mchangano unaowekwa katika maandishi na document halali za shirika(quatation/invoice) na mteja akiridhia na akalipia shirika litanunua vifaa hvyo na kumfikishia umeme mara moja.
HOJA YA KWANINI NGUZO NA NYAYA VIBAKI KUWA MALI YA TANESCO?
Vifaa hivi vinabaki kuwa mali ya tanesco kutokana na mkataba wa huduma kwa mteja unavyoeleza ambao wateka hupewa na kuusain kabla ya huduma lakini lengo kuu la tanesco kuendelea kumiliki line hyo ni kwamba kama likitokea tatizo katika line au nguzo imeoza au kuanguka, tanesco wanakuja kurekebisha kwa garama zao na syo wewe mteja utakayenunua ama kulipa hela ya nguzo au waya ama mafundi na usafiri walioutumia vivyo hivyo wana uwezo wa kuongeza wateja wengine kwenye line hiyo kufidia garama zao za matengenezo.
Maoni yangu ni hayo mdau
 
ukifunga hiyo solar system ya hata millioni kumi itakuwa inauwezo mkubwa sana
 
Ndugu John ! Umejieleza kwa vizuri sana na ndipo suali langu hapa nataka kujuwa , kama mimi mwananchi wa kawaida nagharamia kufikisha miundombinu kwa walaji bila Tanesco kutoa senti 1 , kwanini hizi gharama hawa Tanesco wasi rejeshe kwangu baada ya kupata wateja wengine kupitia miundombinu niliyo gharamia mimi.

Kwani wangekuwa wakirejesha hizi ngarama ingevutia watu wengi kujitolea na kugharamia hili zoezi na Tanesco wangepata wateja wengi kwa muda mfupi sana na faida ingekuwa kubwa kwao.

Lakini kwa ujanja huu mafaniko yatakuwa ni machache sana Kwani huu ni utapeli wa wazi.
 
Mkuu wala hujatapeliwa, watu wengi wavivu kusoma terms and conditions,

Miundo mbinu yote ya TANESCO ambayo umelipia haijalishi thamani yake bado vitabaki kuwa vyao. Hilo limeainishwa wazi kabisa bila kificho.

Wakati mwingine tunalalamika wakati utaratibu upo wazi kabisa
Kwani terms and conditions haziwezi kubadilishwa ,wabadilishe maana zinaumiza
 
[HASHTAG]#Mda[/HASHTAG] Mwingine Unapotaka Huduma Flani za Kijamii Unatakiwa Upunguze Kiherehere sawa Unashida ya Umeme Kwani Ukisubiri Rea Wapite Unaumia Wapi Kwa Jinsi Ulivyo Utaenda Dawasco Ulipie Maji Kwa Mil10 Mambo mengine Unajitakia Mwenyewe Na Utakuwa Wa Mwisho kabisa Alafu watakwambia Tunakuunga Single Phase2
Tunahitaji maendeleo Leo siyo ya kusubiri. Lakini lazima haki itendeke unapo changia gharama za miundombinu ni muhimu mchangiaji urejeshewe gharama zake kwani wewe ni mlaji kama walaji wengine na umesaidia kusambaza kwa walaji wengine ambayo ilikuwa kazi ya msambazaji Tanesco.
 
Tatizo kwanini wasisambaze kwa ela yao kama vifaa vya kwao mbona kampuni za simu hazichangishi minara?
Ndio maana watu wanatamani makampuni binafsi yaingie kwenye biashara ya kutoa huduma za umeme ili.kuleta ushindani. TANESCO ni shirika la umma ndio maana mkurugenzi anateuliwa na rais. Lakini makampuni ya simu ni binafsi sio ya umma ndio maana hakuna upuuzi wa namns hiyo.
 
Hili shirika letu kuna wachache wamelifisidi sasa dhambi yake ndiyo inayotumaliza watanzania waliyo wengi. Nilidhani upatikanaji wa gesi asilia ungeleta unafuu katika suala zima la umeme lakini naona mambo si mambo. Na si vyema mtu ukagharamia kiasi kikubwa cha mil. 15 halafu bado ununue umeme kutoka kwa muuzaji. Bora mkubaliyane utoe hizo gharama halafu wakupe umeme wenye thamani ambayo itatosha kufidia gharama za ziada, ili na watu wengine wafaidike na nguzo hizo, na hiyo itawatia moyo watu wenye uwezo kutoa kiasi kikubwa cha pesa kwa manufaa ya wengi wasiyokuwa na uwezo ili wapate umeme.
 
Ndugu wadau,

Kuna jambo linanitatiza katika mpangilio wa ufanyaji biashara wa hili shirika la umeme TANESCO. Mimi nahitaji kuunganishiwa umeme katika nyumba yangu umeme ambao nitakuwa naulipia kwa kadiri ya matumizi yangu. Lakini ninakerwa na huu utaratibu wa malipo ya vifaa vya kuunganishiwa umeme.

Kwa mfano natakiwa nilipie nguzo kadhaa, waya mita kadhaa, Transformer, na kadhalika jumla ya ngarama naambia ni Tshs Mil. 15, eti kwa ajili ya kuweka miundombinu ya kufikisha umeme ndani ya nyumba yangu. Lakini cha kushangaza baada ya kulipia vifaa hivi kwa Mil 15, vifaa husika vinageuzwa kuwa mali ya TANESCO Bila mimi muhusika kufahamishwa au kuombwa na Shirika hili.

Kupitia miundo mbinu hii niliyo nunua kwa pesa zangu za kudunduliza na mikopo, utaona TANESCO wakianza kuunganishia umeme watu wengine jirani yangu kwa bei nafuu bila kuulizwa au kuombwa na wahusika. Je hii ni haki? Shirika kujinufaisha kupitia mpango huu! Au kwa kuwa ni Shirika la Serikali linafanya litakavyo?

Je kujenga miundombinu ya umeme ni kazi ya mlaji au ni kazi ya msambazaji?
Je ukiimiliki wewe, line ikaharibika aidha nguzo zimezolewa na maji ama upepo au transfoma kuungua utaingia garama za matengenezo mwenyewe?? Ndio maana Tanesco wanamiliki line ili yakitokea hayo yote wao wanagaramia
 
Mkuu wala hujatapeliwa, watu wengi wavivu kusoma terms and conditions,

Miundo mbinu yote ya TANESCO ambayo umelipia haijalishi thamani yake bado vitabaki kuwa vyao. Hilo limeainishwa wazi kabisa bila kificho.

Wakati mwingine tunalalamika wakati utaratibu upo wazi kabisa
Watanzania tu wavivu wa kusoma, na form yenye izo term na condition aliisaini vizuri tuu
 
MONOPOLY ndio inawapa kichwa hawa Tanesco..

Bora hata kwangu nimeweka Solar Panels sina shida kabisaa
 
Je ukiimiliki wewe, line ikaharibika aidha nguzo zimezolewa na maji ama upepo au transfoma kuungua utaingia garama za matengenezo mwenyewe?? Ndio maana Tanesco wanamiliki line ili yakitokea hayo yote wao wanagaramia
Sina tatizo na Tanesco kumiliki line tatizo langu pale gharama za kuweka hizo line naambiwa nitoe mimi mlaji.
 
Gharama kubwa kabisa ya kulipia ili kupata umeme was TANESCO ni 1,500,000TZS Iweje utoe pesa kubwa hiyo milioni 15?
Tena anasema kalipia na transformer kabisa,umeomba service line ya kiwanda au
 
Back
Top Bottom