Je, hili la TANESCO siyo "utapeli"?

Je, hili la TANESCO siyo "utapeli"?

Watanzania tunapenda sana miteremko,utakuta mtaani umeme haupo nguzi ziko mbali unaongea na jirani zako kwamba mchangie gharama za kununua nguzo ila kila unayemgusa jibu lake atakwambia 'MIMI BADO' lkn ukishaamua kulipia nguzo zote unaanza kuwaona mmoja baada ya mwingine wanaunganishiwa umeme kupitia nguzo ulizozilipia wewe, hiyo si haki kabisa
 
Siyo kweli unapotosha! miundo mbinu hiyo tiyari imeshakuwa mali ya SHIRIKA, alichokosa yeye ni subra ya kuwasubiria TANESCO wafanye Installations ya miundo mbinu yao wenyewe kwa kuwa PESA alikuwa nayo na sasa analazimisha FIDIA kitu ambacho hakiwezekani. Labda kama utaratibu umebadilika
Mkuu insu sio utaratibu\sheria kuwepo au kutokuwepo, mleta mada anaona utaratibu huu ni aina ya utapeli, wewe unaona ni sawa kugharamia miundombinu ya mtu mwingine na wengine waje watumie kwa gharama zako? Mi binafsi sipingi tanesco kutaifisha miundombinu ya umeme iliogharamiwa na mtu, (kwa maslai ya nchi) lakini kwa nn wasimfidie kwenye units za umeme mpaka deni lake litapoisha? Mi naona sio utapeli tu, huu ni wizi kabisa!
 
TANESCO hawana makosa ila sisi ndio hatuelewagi
 
Mkuu insu sio utaratibu\sheria kuwepo au kutokuwepo, mleta mada anaona utaratibu huu ni aina ya utapeli, wewe unaona ni sawa kugharamia miundombinu ya mtu mwingine na wengine waje watumie kwa gharama zako? Mi binafsi sipingi tanesco kutaifisha miundombinu ya umeme iliogharamiwa na mtu, (kwa maslai ya nchi) lakini kwa nn wasimfidie kwenye units za umeme mpaka deni lake litapoisha? Mi naona sio utapeli tu, huu ni wizi kabisa!
Hakulazimishwa lakini, na angeweza kuuliza kama atafaidikaje kutoka kwa jirani watakaokuja kunganishiwa kupitia miundo mbinu aliyoilipia kuliko kuja kulalamika baadae wakati ameshafikishiwa umeme tiyari.
 
Ndugu wadau,

Kuna jambo linanitatiza katika mpangilio wa ufanyaji biashara wa hili shirika la umeme TANESCO. Mimi nahitaji kuunganishiwa umeme katika nyumba yangu umeme ambao nitakuwa naulipia kwa kadiri ya matumizi yangu. Lakini ninakerwa na huu utaratibu wa malipo ya vifaa vya kuunganishiwa umeme.

Kwa mfano natakiwa nilipie nguzo kadhaa, waya mita kadhaa, Transformer, na kadhalika jumla ya ngarama naambia ni Tshs Mil. 15, eti kwa ajili ya kuweka miundombinu ya kufikisha umeme ndani ya nyumba yangu. Lakini cha kushangaza baada ya kulipia vifaa hivi kwa Mil 15, vifaa husika vinageuzwa kuwa mali ya TANESCO Bila mimi muhusika kufahamishwa au kuombwa na Shirika hili.

Kupitia miundo mbinu hii niliyo nunua kwa pesa zangu za kudunduliza na mikopo, utaona TANESCO wakianza kuunganishia umeme watu wengine jirani yangu kwa bei nafuu bila kuulizwa au kuombwa na wahusika. Je hii ni haki? Shirika kujinufaisha kupitia mpango huu! Au kwa kuwa ni Shirika la Serikali linafanya litakavyo?

Je kujenga miundombinu ya umeme ni kazi ya mlaji au ni kazi ya msambazaji?
Hapa unayohaki ya kufungua kesi mahakamani, huu ni zadi ya utapeli na ulaghai.
 
Hoja hii ni ya msingi kabisa. Kwa hili la Tanesco kubinafsisha miundombinu iliyogharamiwa na wananchi utaratibu huu ni vyema ulaangaliwa kwaupya. Sio haki kabisa. Pia ni vizuri tukaangalia kwa jicho la upamde wa accouting, hizi assets zinarecordiwaje kwenye vitabu vya Tanesco? Je hii haitoi mwanya kwa Tanesco kuonyesha kuwa wamenunua equipment wakati funds za manunuzi hayo hazikutoka kwako na je ile allocation ya funds za kununua equipment hizo inakwenda wapi au inatumikaje? Nani anayefuatilia hili?
 
Hakulazimishwa lakini, na angeweza kuuliza kama atafaidikaje kutoka kwa jirani watakaokuja kunganishiwa kupitia miundo mbinu aliyoilipia kuliko kuja kulalamika baadae wakati ameshafikishiwa umeme tiyari.
Kibaya hakiwi kizuri eti kwa sababu watu hawajalalamika! Ina maana ni sawa tu serekali iwafanyie mabaya raia wake kwa vile hawalalamiki au hawaoni!? Mbona unatetea dhuluma kupitia shida za wananchi!? Nyie ndo watu wakilalamika na kusema ukweli mnawaita wachochozi na kwamba hawakutakiwa kusema! (Fisimaji)
 
Hopeless!
 
Hakulazimishwa lakini, na angeweza kuuliza kama atafaidikaje kutoka kwa jirani watakaokuja kunganishiwa kupitia miundo mbinu aliyoilipia kuliko kuja kulalamika baadae wakati ameshafikishiwa umeme tiyari.
Silalamiki baadae bali huu ndiyo utaratibu wa Tanesco wanao utumia katika kuunganisha umeme, na ndiyo nauliza je hii ni HAKI !!
 
Silalamiki baadae bali huu ndiyo utaratibu wa Tanesco wanao utumia katika kuunganisha umeme, na ndiyo nauliza je hii ni HAKI !!
Haya mambo yapo kimaandishi mkuu,kama una document ziweke hapa ili tuweze kupata validation ya suala lako
 
Tanesco ni miongoni mwa taasisi zinazoingeza ucheleweshaji wa maendeleo na azma ya serikali ya viwanda hasa vidogo. Mfano mtaani kwetu wameweka Nguzo za HT na nyaya toka mwaka jana na transforma imewekwa kny nyumba ya mtu binafsi kwa kipindi chote hiki je ikiibiwa pale na ni mali ya umma nani mtamlaumu? Mnakera sio kidogo
 
Sheria zilitungwa na zinaweza badilishwa, bora hizo gharama mtu afidiwe kwenye units za umeme, hii itachochoa watu kuchangia huo usambazaji wa umeme.
 
[HASHTAG]#Mda[/HASHTAG] Mwingine Unapotaka Huduma Flani za Kijamii Unatakiwa Upunguze Kiherehere sawa Unashida ya Umeme Kwani Ukisubiri Rea Wapite Unaumia Wapi Kwa Jinsi Ulivyo Utaenda Dawasco Ulipie Maji Kwa Mil10 Mambo mengine Unajitakia Mwenyewe Na Utakuwa Wa Mwisho kabisa Alafu watakwambia Tunakuunga Single Phase2
 
Hukusoma vizuri ile form ya mkataba? fomu imeeleza wazi kuwa mali zote ni za TANESCO.
 
Gharama kubwa kabisa ya kulipia ili kupata umeme was TANESCO ni 1,500,000TZS Iweje utoe pesa kubwa hiyo milioni 15?
 
Back
Top Bottom