Je, hii ni smear campaign, au kuna ukweli ndani yake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, hii ni smear campaign, au kuna ukweli ndani yake?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanaHaki, Sep 11, 2008.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Sep 11, 2008
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Waungwana,

  Wahenga walinena, Lisemwalo lipo, kama halipo, laja!

  Jana jioni, takriban saa 14:01:07 GMT +300 (yaani saa 8:01:07 za Afrika Mashariki), nilipokea ujumbe mfupi wa maaandishi kwenye simu yangu ya mkononi, kama ifuatavyo - ninanukuu:

  "Je? Wewe ni mmojawapo wa waliofaidi bingo ya Mboe ili kuzima habari zake zisiandikwe au kutangazwa? Mhariri Rai Mr Balile kavuta mamilioni kadhaa ili kuzima ha" (mwisho wa kunukuu).

  Ujumbe huo mfupi wa maandishi ulitoka kwenye simu yenye namba +255716398703.

  Kwa kweli, (a) nilishangazwa na ujumbe huo na (b) punde nilipoupata, kwani inaonekana ulichelewa kunifikia... ulinifikia majira ya saa 12 za jioni, namba iliyotumika iliita bila kupokelewa, na hivi sasa haipatikani kabisa. Sikujaribu kumwuliza aliyeutuma yeye ni nani au kwa sababu gani alikuwa ananitumia habari hizo, kama zina ukweli.

  Nimeongea kwa simu na mmojawapo wa wanahabari makini hapa Tanzania, ambaye aliniambia hivi (nanukuu, ila sitamtaja jina):

  Yeye: Kama kuna kesi, kinachopaswa kutokea ni Jeshi la Polisi kutuita sisi waandishi na kutuelezea kwamba kuna uchunguzi uliofanyika, na kwamba tuhuma zilizopo, kama ni kesi ya jinai, ni kwamba kuna kusudio la kumpeleka mahakamani Mbowe na kumshtaki ili sheria ichukue mkondo wake.

  Mimi: Kwani mmeitwa na Polisi?

  Yeye: Hapana. Hatujaitwa.

  Mimi: Na wewe una habari kuhusu SMS hiyo ambayo mimi nimetumiwa?

  Yeye: Hapana. Nadhani huko ni kupotezeana muda tu.


  Mimi ninajiuliza, hapa ni mpango tu wa kuchafuliana majina kwa kashfa zisizo na mpango, au kuna ukweli ndani yake? Huyu ambaye amedai Balile (Deodatus, zamani alikuwa mhariri kwenye gazeti la Tanzania Daima, kama sikosei) amepokea mamilioni ya shilingi ili asiandike habari hizo, ana ushahidi gani? Ameshuhudia au amesikia? Alikuwepo wakati Balile akipokea mamilioni hayo? Amepokea kiasi gani?

  Kama mnavyojua, rushwa ni jambo la siri kati ya mtoaji na mpokeaji, si jambo la wazi hata kidogo. Usitarajie mtu akakuambia amepokea kiasi gani, pasi na wewe kuwapo na kushuhudia, au ametoa kiasi gani, hali kadhalika.

  Je, ni kweli kwamba ndugu yetu Freeman Mbowe anaweza kudiriki kutoa rushwa ili wanahabari wasiandike habari zinazomhusu yeye? Je, ni kweli kwamba Balile ni mwanahabari anayekiuka miiko ya kazi yake, kiasi cha kupokea ngawira/fulusi ili asiandike habari hizo, huku akijua wazi kwamba (a) hilo ni kosa, la jinai na la kikazi, na (b) anawanyima Watanzania haki yao ya msingi ya kutafuta, kupokea na kusambaza habari kwa mujibu wa Katiba?

  Nawaachieni wenye habari zaidi kuhusu suala hili tata (ingawa pengine hoja hii ni ya kisiasa zaidi, kuliko kuwekwa hapa... Moderators wanaweza kutambua hili...) nanyi pia mtoe mchango wenu.

  Swali la mwisho: Huyo aliyenitumia mimi huo ujumbe mfupi wa maandishi, ananifahamu mimi kwa namna gani na aliipataje namba yangu, kwani, namba iliyotumika, awali ya jana, sijawahi kuitumia hata kwa siku moja!

  Wabillah Tawfiq, Wa Rahmatullah Taala Wa Barakatuh!

  ./Mwana wa Haki
   
Loading...