Je hii ni hujuma kwa NHC?. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je hii ni hujuma kwa NHC?.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MIUNDOMBINU, Apr 16, 2010.

 1. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nilikuwa ninasikia kwa juu juu tu juu ya kuwepo kwa wapangaji wa Shirika la Taifa la nyumba ambao wanajihusisha na uuzaji au upangishaji wa Nyumba za Shirika hilo kwa njia za Panya.Lakini majuzi nikaamua kufanya kautafiti kadogo tu ili kujua ukweli wa mambo.Nilikaamua kwenda eneo la Upanga, nikatafuta madalari wanaojishughurisha na utafutaji wa nyumba za kupanga nikaweleza shida yangu wakaniambia Nyumba zipo.

  Mguu na njia mpaka kwenye nyumba husika nilipofika nikaonyeshwa sehemu yenye chumba kimoja na sebule,jiko na bafu.Nika uliza bei nikaambiwa NITAUZIWA KWA TSH 20 MILION.HUKU NA HUKU NIKAAMBIWA MWISHO NI 18 MILION.nikaondoka zangu kuelekea Ilala Boma.napo nikakuta eneo kama la awali bei nikaambiwa ni Tsh 17milion bila kupunguza.Yaani wewe ukinipatia pesa hii mie nakukabidhi card ya Luku, na wewe utakuwa mmliki, ambapo utatakiwa kulipia Tsh 48000 tu kila mwezi kwenye Shirika la nyumba.jamaa akanena.

  Duh siku amini nikaamua kwenda mtaa wa Uhuru ni kamkuta mdosi mmoja nae habari ikawa hiyo hiyo tu.Sasa je hii ni hujuma au ndo kawaida?.
   
 2. m

  mimi-soso Senior Member

  #2
  Apr 17, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mjini hapa mjomba
   
Loading...