je hii ni halali?

una kubali mmiliki gari mbili alafu hata kiwanya hamna? uyo mwana mke amekuona mzembe mpaka akaamuwa kukopa ili anunuwe kiwanja. akilini akijuwa mawazo hayo wewe huna...
 
jibu ni kwamba usijenge na usimfiche mwambie wazi hofu yako
 
Nimeiona kwa Kaka yangu. Lakini kwa namna tofauti, mke alikuwa na kiwanja kabla hawajaoana, walipofikia hatua ya kuanza ujenzi Kaka yangu akamrudishia gharama nusu mke wake na akawa na umiliki wa 50%.

Na hiyo nusu aliyoipata Mke wake akaiingiza kwenye gharama za ujenzi kama mchango wake.
Kaka yangu alifanya hivyo kwa kuamini kwamba hatakuwa 'comfortable' kuishi kwenye nyumba ambayo Mke ni mmiliki
wa kiwanja kwa 100%. Na kwa sasa wameshahamia kwenye makazi mapya kiroho safi.

Hiyo ni scenario yao, sijui kama kwako inaweza kufanya kazi.
Ila kawaida katika maisha yetu ya Kiafrika...........Cha mume cha familia, cha mke ni chake. Hapa haitakiwi kuanzisha ugomvi kwa sababu amenunua kwa pesa yake. Tumia diplomasia kumaliza hii ishu.

Good luck.
 
Arrangements za maisha ya ndoa zinatofautiana, but generally mke majukumu yake ni short term, chakula, afya za watoto, mahala mnapoishi pako sawa etc. Wewe mwanaume, long term projects kama ujenzi na miradi ya kuongeza uhakika wa kipato.

Sasa kaka after 5 years, hata mipango ya kiwanja ulikuwa huna? Maana yake kama ungekuwa nayo, basi at least mngekuwa wote kwenye process nzima. Hapo katumia principles za aliyelala usimwamshe
 
Mkuu, jumlisha yooote changanya na ya kwako! Kama vp aandike majina ya watoto otherwise! toa sadaka tu
 

nakubaliana na wewe mia kwa mia mipango ya kiwanja ilikuwepo ila mambo yalikuwa hayajakaa vizuri na tulijadiliana kuwa yeye ndio achukue mkopo kwa dhamana ya kazi mimi hadi ramani nilishachorewa ipo tatizo hati kuandikwa jina lake
 

asante kwa ushauri jamini its not a joke kulala kwenye nyumba yenye jina la mwanamke inataka ujasiri hata kama umechangia mchango nakubaliana na usemi cha mke cha mke cha mume cha wote
 
huyo dada mroho sana mwanaume ndo kichwa atakama kanunua yeye lazima aandikwe mme,mtoto,au wote,iyo cyo dalili nzuri kabisa na ninjia yakumpashetan loophole yakumletea uyuda!kaa nae mpaka hati uwepo au watoto unless its dangerbut 2mia busara sana,xor

mwanamke nae ana haki ya kumiliki na ku access mali si lazima awe mwanaume huo sasa mfumo dume unaouongelea
 
una kubali mmiliki gari mbili alafu hata kiwanya hamna? uyo mwana mke amekuona mzembe mpaka akaamuwa kukopa ili anunuwe kiwanja. akilini akijuwa mawazo hayo wewe huna...

kaka gari ni bei rahisi zote mbili hazifiki milioni 15,kuna watu wana magari ya thamani hata kiwanja hawana japo kwa wengine inaonekana kituko ila inategemea na mazingira na mipano yenushida z usafiri wa dar si unazijua na tumekuwa nazo kwa miaka mingi hata tukiuza zote hazitoshi kujenga after all kila kitu tulikuwa tumepanga kama familia tatizo ni hati kuandikwa jina lake
 

izo ndo inferiority complex sasa! Kwanini mwanaume akiwa titled kwenye mali mwanamke awe huru kukitumia na mwanamke akiwa titled wanaume mnahisi mwanamke ana tamaa?? Vitu tumepewa tumiliki wote sio jinsia moja bana
 
hii ni post yangu ya kwanza nawashukuru wana jf nimepata solution toka kwenu otherwise uamuzi ambao ningechukua ungeleta nyufa kwenye ndoa yangu, nawaomba wote tukubaliane cha mke cha mke cha mume cha wote ,na biblia inasema tuishi nao kwa akili na wenye mapenzi hakuna mjuzi 100% kuna anayenishangaa kwa hili kumbe yeye anamatatizo makubwa ila hajui anaona sawa kwa mtazamo wake,kweli JF ni chuo kikuu.
 
Me sioni ubaya wa mkeo kuandika jina lake pengine aliona haina shida na ndio maana alikushirikisha suala la kununua pia, na isitoshe na yeye ana haki ya kumiliki acheni mambo ya ukandamizaji wa kijinsia. Kwani imeandikwa wapi mwanaume tu ndo mwenye haki ya kumiliki resorces?
 

Ha ha ha,yu made my day,ina maanisha wanaume mnatuogopa wanawake wa kichaga??kyambaa kiyuumuu ndedee
 
nema13 usiongee kishabiki,imagine mimi ni kaka yako then nyumba inaisha natimuliwa kwenye nyumba
pili angalia sheria ya ndoa inasemaje,mali yote iliyochumwa kwenye ndoa ni mali ya wote,pili anagalia utamaduni wa kiafrika mwanamume kulala kwenye nyumba yenye jina la mke inataka roho ngumu
ingeandikwa jina la wote au mtoto mi nisingekuja kuomba ushauri hapa
 
Ha ha ha,yu made my day,ina maanisha wanaume mnatuogopa wanawake wa kichaga??kyambaa kiyuumuu ndedee

shemejiii we chezea wanawake wa kichaga wana macho matatu
 
shemejiii we chezea wanawake wa kichaga wana macho matatu

Being honest alichofanya hyu mwanamke kiasi flani nna msupport maana magari mawili ni aina moja wapo ya anasa kama bado hamna hata kiwanja na kama mume haushauriki amewaza kuna leo na kesho umezima yeye na wanawe watakua wageni wa nani??at times the way a man behaves and act ndivyo jinc mke nae atakua
 
nimekaa kimya sijaongea kitu na mkataba tayari umeandikwa na malipo yote yameshafanyika ,nahofia kwenda kwa wanasheria atatake it serious inaweza kuharibu mahusiano na akaanza kufanya mambo yake kisirisiri
Wewe tatizo lako nini mkifa hiyo ni mali ya watoto au watoto sio wa kwako? hapo future ni watoto sio nyinyi tena hata mkifia kwenye hiyo ya kupanga ni poa tu. Nyumba ikiisha mwambie mpangishe mlipie watoto ada na kama vipi na wewe chukua mkopo mjenge kwenye kiwanja chenye jina lako muwe nazo mbili si faida hiyo? akitaka kukufunga bao wewe sawazisha atasuzika na roho yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…