je hii ni halali?

Ww mbona mkeo mstaarabu sana,mke wa kaka angu alinunua kiwanja kwa hela ya bro akaandika ni chake mama ake,bro alipojua huo mchezo,nusu amuufosaro.ila pole sana bro,wanawake wengne n pasua kichwa

wakati mwingine mnawaonea wanawake. mwanamke kachukua mkopo bank (hajamuomba pesa), kanunua kiwanja, kaandika jina lake, sasa upasua kichwa wake unatokea wapi?
tukiwaomba pesa mnalalamika, tunachukua mikopo wenyewe bado ni lawama pia, mbona hamna jema jamani. mleta mada ashukuru mkewe kawa na akili ya kuanza ujenzi, maana inaonekana yeye alikuwa bado anakula raha za mjini
 
Ebu simama kiume bana,au labda kakuona hauko serious na majukumu yako ndani ya nyumba! Zungumza nae akupe sababu ya yeye kufanya hivo kisha mridhiane. Ukikaa kimya hataelewa.
 
mbona mimi na mchumba wangu japo sijamuoa ila tuna account ya akiba yenye jina langu na yeye akiba zake anaweka humo,haya ndo mapenz nasiwez msalit na mpango wa Mungu tatzo cku iz ata mke na mume cyo ki2kimoja kama Mungu anavotaka.hii ya bidada cyo!
 
je kama wewe ndio ungekuwa umechukua mkopo na kununua kiwanja, ungeandika jina la nani?
 
wakati tunaoana kila mtu alikuwa na gari yake ni gari yake ni vijigari vya bei rahisi na ni kawaida kwa dar es salaam si kila mtu mwenye gari ana nyumba labda kama unaishi mkoa tofauti na dar

Mkuu kitendo cha mwanamke/mke kuamua kuchukua mkopo benki, ningelikuwa ni mimi hilo unaloliita kijigari ningekiuza haraka mno ili kuongezea vijisenti kwenye hela ya kiwanja.

Kwa kufanya hivyo nina uhakika hata ushiriki wako katika ununuzi wa kiwanja ungelikuwa 100%.

Unajua kilichokutokea wewe ni kukosa kujiamini tokea mwanzo pale mkeo alipoamua kukopa hela(sina uhakika kama mlijadiliana) hadi alipotafuta na kununua kiwanja.

Yote haya ni kwa sababu ulionyesha ushirikiano hafifu ndio maana leo hii upo mbele yetu moyo wako ukiwa unatweta kwa wasiwasi.

Mwisho wa siku kuonesha wewe ni mwanaume mbinafsi kiasi gani, ni hapo mwishoni hayo maswali unayotuuliza.

Hivi mkuu ulipata kweli mafunzo ya namna ya kuishi na mke na kuwa mume responsible???

Hizo nyanga ulizouliza si ulipaswa kukaa chini na mkeo mzijadili, maana mkeo kahangaika kutafuta hela lakini wewe ni kama unaanza kuweka mapozi..
 
Hapo issue syo majina kny makaratasi ila ni nani alitoa pesa in case mpo kny hali ya kutoelewana. Hapo anatakiwa kula kiapo-affidavit kuwa ni kweli alinunua kwa mkwanja wake ila ss nawe unakuwa na equal interest kny hyo kiwanja,hayo fanya mapema hata kabla hujapeleka tofar moja site.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Nadhani anzia kwake, mshirikishe hofu yako kisha ukiona mwitikio hasi ndipo uombe ushauri
 
na wewe kachukue mkopo halafu fanya hivi

1. Akipeleka mchanga wewe peleka kokoto (ratio 1:1)
2. akipeleka cement wewe peleka maji na makoleo na mbao na nondo (1:2)
3. Akipeleka mafundi wewe peleka watoto shule na lipa kodi ya nyumba (1:4)
4. Akipeleka tofali wewe peleka cement, bati na mbao za kuezekea (1:3)
5. .................etc
6. Ikikamilika leta wakili andikishieni urithi watoto 2 mlio nao (hafurukuti mutu hapa)...

sijasema mshindane bali

Wanawake wapendeni waume zenu VS Wanaume ishini vizuri/kwa akili na wake zenu
 
Hivi wanawake wanaotoka huko kwenye mlima mrefu wakoje? Maana naona kama unawahofia
 

Sioni tatizo hapa.

Kanunua kiwanja kwa mkopo wake mwenyewe --> hakuna shida.

Kuhusu wewe kuchangia ujenzi --> hakuna shida, ni mkeo huyo. Kwani mkiachana hutochangia kulea watoto wenu? Hiyo nyumba jenga, ni ya watoto wenu.

Unavituko wewe, yaani ukose usingizi kulala kwenye nyumba inayomilikiwa na mwanamke?
 

Kuna mambo mengi ambayo hayako wazi hapa, ila kwa kifupi ni kuwa inategemea na jinsi gani mnavyoishi na mkeo. Hata hivyo, kama hamkukaa na kukubaliana mtumie jina la nani katika umiliki wa hicho kiwanja, hapo kuna shida na ikiwezekana na wewe tafuta kiwanja chako uandike jina lako kila mtu ajenge kivyake kama ambavyo kila mtu anamiliki gari yake, utakuja kujuta!!
 
Hebu mshauri ama muandike majina yenu wote au muandike ya watoto halafu jubu lake litakupa dhamira halisi yake.
 
wakati taratibu za ununuzi zinafanyika,wewe ulikua wapi?
 

Nimekuelewa inaonekana pamojana kukaa ktk ndoa yenu mda wote uo ila sasa kuna tatizo kati yenu.
Kuna maneno umesema kuna mengi ila umeNza na ili
Wakati anaenda kuchukua mkopo hamkukubaliana vizuri ndio mana ata katika ati ameandika jina lake. Kwakuwa ata yeye hana imani na wewe na kwakua ella ni yake sio mbaya kuandika jina lake
[Chakufanya]
1 hacha kabisa kulizungumzia suala la kiwanja ili kuinusuru ndoa yenu isiingie kwenye migogoro
2 husiache kushiriki katika ujenzi kwani kutokushiriki kutaleta tatizo
Yaani kwakuwa kiwanja ni chake ndo mana hautaki kushiriki.
3 Na wewe sasa jibange kununua chako kwa kubalansi matumizi yako na ukinunua mshirikishe ila na wewe andika jina lako katika ujenzi akikusaidia sawa usimlazimishe sawa
[Angalizo mwanaume ameumba kutafuta sio kutafutiwa pambana]
 

take this advice
 
Kuna jambo moja najiuliza hayo magari kila mmoja alinunua kwa pesa yake iliyotokana na kazi?
Huo mkopo aliochukua bank ameuchukua kwa dhamana ya gari au kazi?
Huwa kuna kawaida ya kushirikishana katika mipango yenu ya kimaisha?

Kama atakuwa ameuchukua mkopo kwa dhamana ya kazi au gari basi amejipa haki ya kuandika hivyo kwakuona haunamchango juu ya hilo, na hii inatoka na ushirikiano kutokuwepo.

Jambo kubwa na la msingi ambalo tunatakiwa kujifunza walioko na ambao hawajaingia katika ndoa ni ushirikiano wa kupanga na kuamua mambo yanayo husu maisha yenu ya kila siku, hili jambo ni nyeti sana ambalo halipaswi kuegemea upande mmoja.
 


Cha mume ni cha familia. Cha mke ni chake si cha familia. Get it in your head!!
 
jibu ni kwamba usijenge na usimfiche mwambie wazi hofu yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…