KATEGUNDA63
Member
- Dec 31, 2015
- 21
- 9
Kwa kawaida kila siku asubuhi kuanzia saa 12, kuna foleni kuanzia Segerea hadi barabara kuu(Mandela). Kutokana na foleni hiyo, utakuta magari ya Serikali ya STK.. yanatanua tena kwa spidi! Leo asubuhi lilianza basi la Mahakama Kuu, lilichomoka pale Kristu Mfalme. Kabla ya kufika njia panda ya Mawenzi likakutana na gari la maji taka likakwama, haliwezikuingia kwenye foleni na gari la maji taka haliwezi kupita. Tukakwama zaidi ya robo saa. Kuelekea Muslim ikaja STK Toyota Cruiser imetanua mbio, baada ya kupita msichana mmoja maskini akakatiza anavuka upande wa pili wa barabara, ikachomoka STK nyingine kama mshale ikamvaa maskini! Hatujui kama amepona au la! Hivi wafanyakazi walio kwenye magari ya ST ndio wana uhalali na haki ya kutokaa kweye foleni? Hivi kwa yule dreva aliyemgonga yule msichana, hii ilikuwa ajalai kweli au ni ubabe tu?