Je, hii ndio mbinu mpya ya wanawake kujitongozesha?

Je, hii ndio mbinu mpya ya wanawake kujitongozesha?

harder king

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
3,968
Reaction score
6,920
Ipi hivi leo baada ya kufika kazini nikaona nitoke kidogo nikaingia mahali hili kuiweka akili sawa..

Nilipoingia nikakutana na dada mmoja (namfahamu) baada ya salamu akaniomba simu mimi nikampa nikijua labda kaishiwa salio au chaji kwenye simu yake na kuna mtu anataka kuwasiliana nae. Nilipompa nikawa namcheki tu,akaandika namba mara naona namba yangu inatokea kwenye simu yake(alijibeep)

Halafu akawa anaandika msg akaituma ikaingia tena kwenye simu yake,mimi namcheki tu.

Akanirudishia simu nilipokagua upande wa msg nikakuta alituma neno "mambo" nikanyamaza na yeye akaaga akasepa!

Baada ya kama lisaa napokea msg kwenye ile namba aliyojitumia "pw we nan" yaani kajitumia msg kwa simu yangu halafu badae anajijibu mwenyewe akifikiri sijagundua chochote

Sasa hivi ni anafululiza msg tu na simjibu hata moja!..

Naona hii ni mbinu mpya kwa dada zetu ili kutudaka kirahisi rahisi na tiyari tumesanukaa!!
 
Afadhali wewe umemshtukia mapema. ..haiwezekani Mtu awe ana kutumia text kibao ijapo kuwa haumjibu bado ana endelea tu....Huyo atakuwa anapaswa kupewa chumba milembe
Ukute na yeye Ni mmoja wapo sema kaona noma
 
Hebu lete hiyo namba yake kama kweli wewe umesanuka na huna mpango naye wengine hatujasanuka mkuu.
 
Umeona ehh
Afadhali wewe umemshtukia mapema. ..haiwezekani Mtu awe ana kutumia text kibao ijapo kuwa haumjibu bado ana endelea tu....Huyo atakuwa anapaswa kupewa chumba milembe
 
mwambie sikuhizi mambo si maguni ni kumtokea mtu na kumweleza unachohitaji then maisha yanaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom