Je, hii adhabu inanifaa?

Je, hii adhabu inanifaa?

chingaa

Member
Joined
Jun 25, 2017
Posts
86
Reaction score
77
Wapendwa sijawai andika uzi wowote umu ndani.. Lakini kwa yanayo nikuta imebidi niandike

Familia yetu imejariwa watoto watatu
Wawili ni wakike na mmoja ndiyo wakiume ambaye ni MIMI.. Baba yetu Alifariki angali nipo kidato cha Tatu
Hivyo mama ndiyo alibeba jukumu la kutulea

Nilipo maliza elimu yangu ya kidato cha nne sikufanikiwa kujiunga na kidato cha Tano maana maksi nilizo pata hazikuniruhusu kuingia kidato cha TANO.

Mwaka jana nikaamua kufanya mtiani wa kidato cha nne kama PC
Ishalla mungu akasaidia nikapata credit zote Tatu nilizo kuwa nazitafuta...

Mwaka huu mwezi Huu inabidi ningekuwa tayari nshaa Anza masomo... Lakini kuna tatzo lilijitokeza... Mwezi wa pili mwaka huu mpenzi wangu alidaka UJAUZITO..

Kutokana na familia yetu ilikuwa kwenye mihangaiko ya kuandaa HARUSI ya DADA ETU wa kwanza, sikuoni kama itakuwa vyema kuwapa taarifa mapema kwa kuhofia kuwapa STRESS.

MWEZI Huu taree 13 ilikuwa send off ya dada.. Na siku mbili mbele ikawa HARUSI YAKE. pia baada ya harusi ikapita wiki moja. Mpenzi wangu kwao wakaanza kugundua kwamba ni MJAMZITO.. Sikuwa na namna yoyote Ile zaidi ya kutoa taarifa nyumbani kwamba kuna mtu yupo na UJAUZITO WANGU..

Napia mpenzi wangu akaja NYUMBANI KWETU.. walimpokea vizuri tu.. Na pia tunaishi nae vizuri tu...

ADHABU INAYO NIKUMBA

MAMA yangu amekataa kunipeleka shule.. Na Juma Tatu ya taree 3/7/2017 rasmi inabidi nianze masomo yangu ya ADVANCE.. Ukizingatia sijawai fanya kitu chochote ambacho kimewai COST familia yetu gharama yoyote Ile wala mimi sio mtu wa vurugu,pia sio mlevi, mwizi, mkabaji wala sio mtu wa MAKUNDI

Ndugu na Jamaa wamejaribu kumuelekeza MAMA kwamba itakuwa sio vizuri kuto nipeleka shule et kwa sababu kuna binti ANAUJAUZITO WANGU,, Pia mimi nimemwomba msamaha mama ili tu nianze masomo yangu ya ADVANCE,
lakini amekataa.. Jamani kusema ukweri MOYO WANGU UNANIUMA
Ukizingatia mimi ni mwanadamu na makosa niliumbiwa.. Sijawai kataa kusoma pia hata mama anajua kuwa nia yangu ni kusoma... Lakini ndo ameshaa amua kuto nisomesha kisa kuna Bint ANAUJAUZITO WANGU..

JE ADHABU HIYO INA NIFAA???
NA JE NIFANYE NINI JAMANI??
 
wala mimi sio mtu wa vurugu,pia sio mlevi, mwizi, mkabaji wala sio mtu wa MAKUNDI
Bali ni Mzinzi, dah ungebaki na sifa zote hizo ukakosa hio ya Uzinzi, sasa hizo sifa zote nzuri hazina maana yoyote, Nadhani Mama yetu huyo atakua ni Mfuasi wa Blaza J aliyepiga stop Mabinti kurudi skuli, Mama yetu yeye kaongeza kidogo....
 
Pole sana kaka.
Ila kwakuwa ni mama yako mzazi sitosema chochote.
Ila endelea kumbembeleza naamin ni hasira tuu
 
Ume-join Sunday yaani juzi tarehe 25/06/2017 ulitaka uwe umepost nyuzi ngapi hadi sasa??

Hiyo haijarishi... Maana kuingia jamii forum na kusoma mambo yanayo endelea sio lazma kujiunga... Bali kupost nyuzi inabidi ujiunge na ndio maana nimejiunga ili nami nipost nyuzi mbali mbali na kutoa dukuduku nililo kuwa nalo
 
Hat ningekuwa mimi, nisingekusomesha. Siwezi kusomesha MZAZI. Ungekomalia shule na kuachana na mambo ya mademu
 
Aisee Enyi Wanawake badirikeni .. Utabebaje Ujauzito wa Mtoto Mdogo wa namna Hiyo... Ewe Kijana nawe Kuwa na Akili Timamu.. Japo Umeomba msamaha kweli kwa Umri wako Unaweza Mletea Mjukuu Mama yako Katika Ugumu huu wa Malezi? Wewe tu unahitajika kulelewa halafu ghafla akulee wewe na Mjukuu Juu tena na Mkwe Juu..

Ebu Kaa Tunza Mke Changa wako acha kuhamisha majukumu kwa Mama yako.. Angalia alivyohangaika na Kukulewa alitegemea wewe Uwe Msaada kwa U wa Kiume tu Pekee Yake na ndiye aliye na Uhakikaa wa kuendelea kuishi hapo Nyumbani Muda Wote. dada zako wataolewa na wataondoka ila wewe hautaondoka hapo ghafla unamletea Mzigo Mwingine ambao hakuutegemea kwa vinyege mshindo vyako.

Tafadhali Muonee Huruma Mama yako acha Kumzeesha bure.
 
Pole aseeh. Hizo ni hasira za mama tu nenda naye taratibu atakuja kukuelewa.

Mimi mshikaji wangu alishatengwa na pare joo.. alikuwa Cole imagine joo hata salamu ya familia ilikuwa haipo.

Wazazi wetu wanandoto zetu akilini mwao wanapoona tumeharibu huwa tunawaweka katika wakati mgumu saana. Endelea kumwomba msamaha atakuelewa. Tumia hata kikao cha familia.
 
Wapendwa sijawai andika uzi wowote umu ndani.. Lakini kwa yanayo nikuta imebidi niandike

Familia yetu imejariwa watoto watatu
Wawili ni wakike na mmoja ndiyo wakiume ambaye ni MIMI.. Baba yetu Alifariki angali nipo kidato cha Tatu
Hivyo mama ndiyo alibeba jukumu la kutulea

Nilipo maliza elimu yangu ya kidato cha nne sikufanikiwa kujiunga na kidato cha Tano maana maksi nilizo pata hazikuniruhusu kuingia kidato cha TANO.

Mwaka jana nikaamua kufanya mtiani wa kidato cha nne kama PC
Ishalla mungu akasaidia nikapata credit zote Tatu nilizo kuwa nazitafuta...

Mwaka huu mwezi Huu inabidi ningekuwa tayari nshaa Anza masomo... Lakini kuna tatzo lilijitokeza... Mwezi wa pili mwaka huu mpenzi wangu alidaka UJAUZITO..

Kutokana na familia yetu ilikuwa kwenye mihangaiko ya kuandaa HARUSI ya DADA ETU wa kwanza, sikuoni kama itakuwa vyema kuwapa taarifa mapema kwa kuhofia kuwapa STRESS.

MWEZI Huu taree 13 ilikuwa send off ya dada.. Na siku mbili mbele ikawa HARUSI YAKE. pia baada ya harusi ikapita wiki moja. Mpenzi wangu kwao wakaanza kugundua kwamba ni MJAMZITO.. Sikuwa na namna yoyote Ile zaidi ya kutoa taarifa nyumbani kwamba kuna mtu yupo na UJAUZITO WANGU..

Napia mpenzi wangu akaja NYUMBANI KWETU.. walimpokea vizuri tu.. Na pia tunaishi nae vizuri tu...

ADHABU INAYO NIKUMBA

MAMA yangu amekataa kunipeleka shule.. Na Juma Tatu ya taree 3/7/2017 rasmi inabidi nianze masomo yangu ya ADVANCE.. Ukizingatia sijawai fanya kitu chochote ambacho kimewai COST familia yetu gharama yoyote Ile wala mimi sio mtu wa vurugu,pia sio mlevi, mwizi, mkabaji wala sio mtu wa MAKUNDI

Ndugu na Jamaa wamejaribu kumuelekeza MAMA kwamba itakuwa sio vizuri kuto nipeleka shule et kwa sababu kuna binti ANAUJAUZITO WANGU,, Pia mimi nimemwomba msamaha mama ili tu nianze masomo yangu ya ADVANCE,
lakini amekataa.. Jamani kusema ukweri MOYO WANGU UNANIUMA
Ukizingatia mimi ni mwanadamu na makosa niliumbiwa.. Sijawai kataa kusoma pia hata mama anajua kuwa nia yangu ni kusoma... Lakini ndo ameshaa amua kuto nisomesha kisa kuna Bint ANAUJAUZITO WANGU..

JE ADHABU HIYO INA NIFAA???
NA JE NIFANYE NINI JAMANI??
Ninachoweza kukushauri,mmbembeleze mama na kumuahidi hutorudia makosa ya kugegeda tena,maana anaogopa usiije tia mimba nyingine kwa huyo binti kabla hujamaliza form six,pia anaogopa isije tia mimba denti mwingine huko shule uendako na ukaishia jela 30yrs kama alivyosema anko Magu.
Cha msingi nipo tayari kumlea huyo binti na ujauzito wake endapo kwako na kwenu kuna shida ya kumlea,na endapo utakubali hilo itabidi usiwe tena na mawasiliano naye wala lengo la kumgegeda,nataka nikusaidie usome ukiwa huna mawazo ya malezi!
Be Strong!
 
Aisee Enyi Wanawake badirikeni .. Utabebaje Ujauzito wa Mtoto Mdogo wa namna Hiyo... Ewe Kijana nawe Kuwa na Akili Timamu.. Japo Umeomba msamaha kweli kwa Umri wako Unaweza Mletea Mjukuu Mama yako Katika Ugumu huu wa Malezi? Wewe tu unahitajika kulelewa halafu ghafla akulee wewe na Mjukuu Juu tena na Mkwe Juu..

Ebu Kaa Tunza Mke Changa wako acha kuhamisha majukumu kwa Mama yako.. Angalia alivyohangaika na Kukulewa alitegemea wewe Uwe Msaada kwa U wa Kiume tu Pekee Yake na ndiye aliye na Uhakikaa wa kuendelea kuishi hapo Nyumbani Muda Wote. dada zako wataolewa na wataondoka ila wewe hautaondoka hapo ghafla unamletea Mzigo Mwingine ambao hakuutegemea kwa vinyege mshindo vyako.

Tafadhali Muonee Huruma Mama yako acha Kumzeesha bure.
Je ulitaka nimshawishi atoe hiyo mimba?? Pia najua nilifanya kosa lakini adhabu ya kuto soma ni sahihi.. Bola ninge kuwa naanza o level but ni advance brother...
 
Inakufaa sana,wewe ni baba wa familia unataka umwachie nani majukumu yako? Hatuna shule za wababa kuna za wavulana tu. Lea mimba hiyo na mtiti wa kujifungua your first born uuone, ukienda shule utatuletea mjamzito mwingine ukidai shetani kakuzowea.
 
Hat ningekuwa mimi, nisingekusomesha. Siwezi kusomesha MZAZI. Ungekomalia shule na kuachana na mambo ya mademu

Sikupingi....ila maamuzi ya busala ni ya msingi kuliko maamuzi ya hasira
Kila mtu duniani anakosea.. Na mimi hili ndilo kosa langu LA kwanza...
 
Pole aseeh. Hizo ni hasira za mama tu nenda naye taratibu atakuja kukuelewa.

Mimi mshikaji wangu alishatengwa na pare joo.. alikuwa Cole imagine joo hata salamu ya familia ilikuwa haipo.

Wazazi wetu wanandoto zetu akilini mwao wanapoona tumeharibu huwa tunawaweka katika wakati mgumu saana. Endelea kumwomba msamaha atakuelewa. Tumia hata kikao cha familia.

Thanks brother... Hata ivyo dada zake mama pamoja na wadogo zake wote wanajaribu kumshawishi ili tu nisome maana wote wanajua jinsi gani nataka kusoma... Na nimetereza tu
 
Ninachoweza kukushauri,mmbembeleze mama na kumuahidi hutorudia makosa ya kugegeda tena,maana anaogopa usiije tia mimba nyingine kwa huyo binti kabla hujamaliza form six,pia anaogopa isije tia mimba denti mwingine huko shule uendako na ukaishia jela 30yrs kama alivyosema anko Magu.
Cha msingi nipo tayari kumlea huyo binti na ujauzito wake endapo kwako na kwenu kuna shida ya kumlea,na endapo utakubali hilo itabidi usiwe tena na mawasiliano naye wala lengo la kumgegeda,nataka nikusaidie usome ukiwa huna mawazo ya malezi!
Be Strong!

Asante sana kwa moyo ulio nao..
Nyumbani tupo vizuri.. Kumlea binti na mtoto sio tatzo..pia huyu binti sio mwanafunzi..
 
uza minyororo hiyo uende shule maana hata pombe kasema hasomeshi wazazi
 
Back
Top Bottom