Mwanzoni mwa mwezi wa Sita, 2014 niliingia kwenye website ya zoomtanzania.com
Katika tembea tembea zangu, nikakutana na tangazo hili la internship kutoka African Barick Gold. Lilikuwa linasomeka kama hivi:
Kwa sababu nilikuwa katika mchakato wa kutafuta nafasi za field, nilituma barua ya maombi. Baada ya wiki kama 2, nilipokea e-mail ifuatayo:
Baada ya kupata email hiyo, leo nimepokea ujumbe ufuatao kwenye simu yangu kutoka kwenye namba ya Mr. Bryson Kagenzi:
+255759352328: Ndugu, naendelea kufanya selection ktk nafasi za internship & field practice/ABG.so far zimebaki nafasi 9 tu, tusaidiane kitu, unitumie laki 1.5 then mm ntakupitisha ktk hizi nafasi, nakushauri usiache maana kw baadae wanalenga kutoa mikataba y kurudi kufanya kazi, after graduading unasemaje?
Nilipousoma ujumbe huo, sikuujibu.
Nikajaribu kutuma hela kwa kupitia M-pesa ili niangalie usajili, nikakuta hiyo namba imesajiliwa kwa jina hilo hilo la Bryson Kagenzi.
Baada ya hapo nikajaribu kupiga simu kwa kutumia namba nyingine, maongezi yakawa hivi:
Mimi: Hello, naongea na Bryson!?
Yeye: (Akashtuka kama vile hamfahamu huyo mtu)!!
Mimi: Naongea na Bryson Kagenzi?
Yeye: Basi utakuwa ume-wrong number. Mimi sio bryson!