Je, hali hizi hutokea mwilini mwangu pekee?

Mar 24, 2020
44
87
Lengo haswa ningependa kushare kama kuna ambaye ana ufahamu au baadhi ya vitu ambavyo hunitokea katika mwili wangu tangu utotoni mpaka sasa na pia kama kuna mtu naye humtokea basi ningependa nifahamu.

Tukio la kwanza, ni pale ninapomaliza kula then nikanywa maji basi baada ya muda mfupi tu huwa naanza kukicheua kile chakula kwa hivyo inabidi nikitafune then nikimeze hali hii hujirudia mara kwa mara hata baada ya lisaa limoja baada ya kula kile chakula.

Tukio la pili ni pale, ninapomaliza kupiga miayo basi masikio yana zibuka hali hii husababisha usikivu kubadilika na sauti kuwa nene huendelea mpaka pale nitakapo bana pua kwa vidole katika sehemu ya chini ya pua na kuvuta pumzi kwa kasi kuelekea ndani ndipo hali hurudi kawaida.

Ninapouliza swali katika kichwa cha habari ni kwamba nimekuwa nikifanya uchunguzi wa hvyo vitu kama pale jirani yangu anapopiga miayo au hiyo ya kucheuwa na nagundua ni kama hunitokea peke yangu.

Karibuni kwa majidiliano.
 
Sijawahi Iona hiyo
Itakuwa ni kwako peke yako

Alafu chakula ukikicheua inabidi usimeze bhana kinakuwa na Radha ya uchachu unawezaje kumeza?
 
Hiyo ya kucheuwa niliwahi kuiona kwa Jamaa yangu Side yaani ni kama Mbuzi anaanza kukitafuna kile chakula upya.AAAAAGGGGGGHHH
 
Hiyo ya pili hata Mimi inanikuta sana...sijajua ina sababishwa na nini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom