SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,129
- 7,898
Embu tukumbuke sheria za mpira wa miguu zinasemaje kuhusu goli la kujifunga ili tujue kama mtu anayestahili kupewa credit ya goli la nne katika mechi ya jana ya Yanga vs Mtibwa ni Skudu au beki wa Mtibwa.
Skudu alipopiga mpira, kipa alianza kuruka kuufuata ule mpira ila kuna beki wa Mtibwa akaupiga kichwa na kuupeleka mpira juu zaidi ya eneo ambalo kipa alidhani mpira unaelekea matokeo yake akashindwa kuufikia. Ukiangalia vizuri utaona yule beki baada ya kujifunga alishika kichwa.
Angalia goli hili katika fainali ya kombe la dunia 2018, Ufaransa vs Croatia. Goli hili linafanana sana na hili la Skudu na lilihesabika kama goli la kujifunga kwa mchezaji wa Croatia aliyeuparaza mpira kwa kichwa.